#COVID19 Mwongozo wa Serikali kwa Shughuli za Michezo na Matamasha ya Muziki kukabiliana na UVIKO

#COVID19 Mwongozo wa Serikali kwa Shughuli za Michezo na Matamasha ya Muziki kukabiliana na UVIKO

Informer

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,606
Reaction score
6,672
Serikali kupitia Wizara ya Afya, leo imesema Mazoezi na shughuli zote za michezo ni sehemu muhimu katika kuimarisha afya na kujikinga na magonjwa mbalimbali.

Hata hivyo, imesema shughuli hizi zinatakiwa kufuata mwongozo wa kuzingatiwa kuendesha shughuli za michezo katika kipindi cha Mlipuko wa covid 19 nchi kwa lengo la kudhibiti maambukizi ambao ulitolewa na Wizara ya Afya Mei 2020.

Kwa matamasha ya muziki, burudani na sanaa nyingine na ambayo yameidhinishwa na BASATA waandaaji watahakikisha kuwa matamasha hayo yanafanyika zaidi kwenye maeneo ya wazi (viwanjani), ambapo kabla ya kuingia uwanjani waandaaji watahakikisha kuwa washiriki wananawa mikono kwa maji tiririka/kutumia vitakasa mikono na kuvaa barakoa uwanjani.

Kamati za ulinzi na usalama za Mikoa katika kuridhia matamasha haya, zitajiridhisha kwanza na uzingatiaji wa masharti haya.

Aidha, kwa shughuli zote za sanaa zinazolazimika kufanyika ndani ya kumbi waandaaji watahakikisha zitazingatia Kanuni zote hizi na ile ya kuhakikisha watu wanakaa umbali wa mita moja.
 
Nchi inachanja mbuga
Kisha atoke gaidi kuvuta shati hakika hatovumilika
 
Safi sana tunaona utekelezaji wa kushindo🤣
IMG_20210725_145216.jpg
 
Back
Top Bottom