Mwongozo wa ufugaji Bora wa ng'ombe wa maziwa

Mwongozo wa ufugaji Bora wa ng'ombe wa maziwa

Harry Mapande

Senior Member
Joined
May 18, 2020
Posts
109
Reaction score
363
Kumekuwa na maswali kwenye jukwaa hili kuhusu ufugaji wa ng'ombe wa maziwa ,Mimi ni mfugaji wa muda mrefu nimeamua nitoe mchango wangu juu ya ufugaji wa ng'ombe wa maziwa.

Hapa nchini Kuna aina tatu maarufu za ng'ombe wa kisasa wa wa maziwa pia Kuna aina nyingine ila katika mizunguko yangu mikoa mbalimbali hasa ya nyanda za juu kusini nimekutana na aina 3 aina hizo ni 1. Friesian huyu anakuwa na mabaka ya rangi nyeusi na nyeupe, 2. Ayrshire anakuwa na mabaka mekundu na meupe, 3. Jersey and rangi ya kahawia isiyokolea mpaka iliyokolea Sana.

Binafsi simshauri mtu afuge chotara au wa kienyeji kwa ajili ya maziwa kwani wanatoa maziwa machache.

Ng'ombe Hawa wanahitaji chakula cha kutosha (Majani) wanakula mchana na usiku, maji, wanga-pumba, protini-mashudu ya mbegu mafuta, madini-mifupa iliyosagwa au jiwe la kulamba na vitamin.

Wafuge ndani usiwachunge Hawa ng'ombe asili yao ni nchi za Ulaya zenye baridi sasa ukiwachunga unakuwa unawapa shida kwa kupigwa na jua.

Jenga banda bora weka gypsum au ceiling board ukiweza weka feni,usishangae feni Qatar ng'ombe wao wanawawekea air condition.
Ukitaka mbegu watembelee wafugaji wazoefu au ulizia kwa madaktari wa mifugo Ila kabla hujanunua fuatilia historia ya ng'ombe husika hapa wafugaji wengi hawapendi kuuza ng'ombe mzuri huwa wanauza ng'ombe mwenye matatizo au mzee,usiwe na haraka ya kununua, pendelea kununua ndama au mtamba halafu wakuze mwenyewe.

Bei za ndama,mtamba na ng'ombe inategemea upo wapi mf.nimeona nyanda za juu kusini Bei ni ndogo kulinganisha na Arusha.
Magonjwa ukiwa unawapa kinga hawasumbui sana kwenye magonjwa.

Uliza swali la kawaida nitajibu usiulize maswali yanayotakiwa kujibiwa na Profesa wa SUA.

Pia nina kitabu kizuri kinachoitwa Mwongozo wa ufugaji bora wa ng'ombe wa maziwa atakayekihitaji tuwasiliane 0621004820.
Kitabu hicho ndiyo ninakitumia Kama Mwongozo katika ufugaji.
 
Mkuu hujataja bei ya hao ndama ni kiasi gani.
 
1. Changamoto kwenye ufugaji wa ng'ombe wa maziwa haswa ni zipi ukiacha chakula kipindi cha kiangazi?

2. Njia gani ni bora kupandikiza mbegu kwa sindano? ama kwa njia ya kawaida? (kupandisha na dume)

3. Ni vitu gani vya kuzingatia zaidi ili kupata maziwa ya kutosha kwa ng'ombe mkubwa au kumlinda ndama akuwe vizuri?

4. Vitu gani vya kuzingatia unapojenga banda la ng'ombe wa maziwa?
 
Back
Top Bottom