Mwongozo wa ufugaji wa kisasa wa Mbuzi wa nyama na maziwa

TUANGAZIE UFUGAJI WA MBUZI KATIKA BIASHARA

Kwa ujumla ufugaji wa mbuzi ni biashara kubwa. Kama mfugaji atafuata na kuzingatia kanuni bora za ufugaji wa mbuzi hataweza kupata hasara.

Mara nyingi mbuzi husumbuliwa zaidi na magonjwa ya mapafu. Ugonjwa huu ikiwa mbuzi watacheleweshwa kutibiwa utawafanya wafe kwa wingi na kwa haraka. Dalili ya ugonjwa wa mapafu ni pamoja na kwamba mbuzi wanakuwa na homa kali, kukohoa, na vifo hutokea baada ya siku 1-2 tu. Ni muhimu kutambua mapema dalili za ugonjwa huo ili mbuzi wawahi kutibiwa kwa haraka.

Mbuzi ni tofauti na ng'ombe ni wastahimilivu sana dhidi ya ukame. Wanakula nyasi pia wanakula majani ya miti. Ikitokea nyesi zimekwisha au kukauka watandelea kuishi na kuzaliana kwa kula majani ya miti.Wakati wa kiangazi mmiliki wa mradi wa ufugaji wa mbuzi huwi na presha juu ya chakula cha kuwalisha mbuzi.

Thamani ya mbuzi imekuwa kubwa hasa mjini kutoka na watu wengi kuhitaji nyama choma ya mbuzi hivyo hutoa hakikisho la faida kwa mwenye mradi .Isiteshe mbuzi huzaliana haraka sana ndani ya muda mfupi na kufanya kundi lao liongezeka kwa kasi. Kwa wastani toka mbuzi ashike mimba hadi kuzaa(Gestation period) huwa inamchukua siku 150 sawa na miezi 5,ndani ya mwaka mmoja mbuzi anazaa mara 2.

Ukiwa na mbuzi 50 majike na madume 2 katika uwiano wa 1:25, ndani ya miaka 3 utakuwa na mbuzi majike jumla 200+madume 152 hawa ni wazazi na watoto wao +118 majike na 118 madume hawa ni watoto wa watoto. Kwahiyo jumla kuu utakuwa na mbuzi 588 hii idadi na ndani ya miaka 3 kati ya hao madume yatakuwa 270 na majike yatakuwa 318. Hii hesabu niliyofanya kupata hii idadi ya mbuzi jumla kwa miaka 3 ni hesabu kali sana. Unaanza na mbuzi hamsini unamaliza na mbuzi 588 ndani ya miaka 3.
 

Mkuu bado unafuga hao ng'ombe breed ya jersey?
 
Kama kuna wanaopenda kufuga wanyama hasa Mbuzi ( wa maziwa,nyama),njooni tuunganishe nguvu tufanye mambo.Inawezekana kabisa tukafuga kwa mafanikio sana. Kila kitu kipo ndani ya uwezo wetu.

I believe together we can go.
Hongera sana mkuu kwa maono yako kiukweli nimependa sana hillo wazo Na Niko tayari
 
Kaka Amani naomba nikuulize hizi aina za mbuzi ninazoziona hapa kwenye picha unazo ww!?

Pia naomba kujua bei!? Na anijulishe wanawezaje kufika mtwara kwa yule bimkubwa wetu!?
 
Kaka Amani naomba nikuulize hizi aina za mbuzi ninazoziona hapa kwenye picha unazo ww!

Pia naomba kujua bei!? Na anijulishe wanawezaje kufika mtwara kwa yule bimkubwa wetu?

Tafuta mbuzi aina ya Newala hawana utofauti na ujiji katika uzaaji wake na matunzo pia.
 
Mkuu hao mbuzi wana sifa gani na wanapatikana wapi?

Kwa uzazi mzuri na wa haraka, kwa mfano wale wangu walikuwa wananipa watoto 4 mpaka 6 kwa mbuzi mmoja kwa mwaka.

Changamoto yao ni moja tu sokoni watu wengi wanataka mbuzi wenye miili mikubwa badala ya uzito, nakushauri utumie dume aina ya Mallya au Solo.
 
Asante kwa elimu nyumbani kwetu kijijini ni wafugaji nipo kigoma kuna maeneo makubwa sana ya kufugia mbuzi, Aman nitakutafuta ili unisaidie kupata hao mbuzi
 
Wadau, mimi nimeanza ufugaji mdogo mdogo kwa malengo ya baadae kuwa wa kibiashara. Ninatafuta mbegu ya mbuzi wanaozaa mapacha wanne. Naomba kama kuna mtu anafahamu mahali niakoweza kuwapata au ni mfugaji ajitokeze tafadhali.

Asanteni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…