MWONGOZO: Zingatia haya unapoweka tangazo lako!

Bora mmetoa ufafanuzi maana humu watu huwa wanatoa matangazo ya biashara kama wanakimbizwa.
 
Mkuu naomba kuuliza nawezaje kuedit thread title?? au haiwezekani kufanya hivyo??
 
Naomba ufafnuzi wa hili "You have been banned for the following reason: We do not allow Spamming and Hotlinking[OFA YA MWEZI: Jipatie Website kwa Bei Nafuu!!!" hiyo ni akaunti ya jama microsafi imefungwa
Hiyo sababu uliyoitaja ipo kinyume na sheria za JF. Adhabu yake ndio hiyo(Ban)
 

Ujumbe huo hutumwa kwa mtu aliyeweka link ya kwenda kwenye site yake ama anayesambaza ujumbe mmoja mara nyingi (ndiyo maana ya spamming and hot-linking) ambako ni kosa kwa mujibu wa JamiiForums Rules

Asante.
 
Mkuu naomba kuuliza nawezaje kuedit thread title?? au haiwezekani kufanya hivyo??

Ni moderators pekee ndiyo wenye uwezo wa kufanya hivyo. Wapo online, watumie ujumbe kueleza suala lako.

Je, una swali lolote kuhusiana na Jukwaa la Matangazo?
Karibu..
 
Hiyo namba 2 na 3 ndo pasua kichwa kwa makanjanja, utaletaje tangazo bila bei, ikiwezekana muwapige ban kabisa
 
Pia naomba kuuliza baadhi ya matangazo licha ya kuwa yamekidhi vigezo huwa yanafutwa, ni kwanini na ukiangalia katika uzi husika hulikuti
 
Pia naomba kuuliza baadhi ya matangazo licha ya kuwa yamekidhi vigezo huwa yanafutwa, ni kwanini na ukiangalia katika uzi husika hulikuti

Matangazo ambayo huondolewa ni yale yanayokiuka vigezo tajwa hapo juu au yanavunja JamiiForums Rules..

Unaweza kutupatia mfano wa tangazo lililoondolewa ambalo unadhani limeondolewa kimakosa?!

Karibu..
 
Umefafanua vizuri sana. Wale wanaosema nifuate PM muwe mnawapiga ban kabisa. Tangazo la biashara linatakiwa kuwekwa lote
 
Mathalani, Tangazo langu na taka kulirejea wiki nzima yaani kwa siku mara 1, je uzi ule niliotumia naweza kuupataje
 
Ni moderators pekee ndiyo wenye uwezo wa kufanya hivyo. Wapo online, watumie ujumbe kueleza suala lako.

Je, una swali lolote kuhusiana na Jukwaa la Matangazo?
Karibu..
kwahyo kama nikitaka kuchange thread title naweza kuwaona moderators??
 
Sawa kwa muongozo,nina mswali mawili nahitaji majibu.
1)kwanini kufungua acc mnachelewa sana ku acept? Kuna ndugu anasubiri toka juzi na bado hakuna majibu.
2)nitumie njia gani kubadilisha jina langu humu na maombi kupokelewa haraka?
 
Kama mnafatilia swala la kuwekwa matangazo hapa jukwaani je ni hatua zipi nyinyi jamii forum mnazichukua endapo mtu akatapeliwa ama kuuziwa kitu feki...???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…