My Father. Our Hero. Who is your Hero?

Analyse

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2014
Posts
17,637
Reaction score
47,413
Jana nilikuwa naongea na Mzee, maana ni mgonjwa. Maongezi yetu yalinirejeshea kumbukumbu fulani ambayo nimeamua kuiweka hapa.

***** ***** ***** ***** ***** *****

Maisha home yalikuwa tight sana, mzee ikabidi asepe kijijini akasogea mjini (familia ikabaki kule, binafsi sikuwa nimezaliwa bado).

Alipofika town, baada ya muda akaivuta familia kwenda kule, japo life bado lilikuwa la kusua sua. Mambo kidogo yalikuja kukaa poa, then ndio tukazaliwa sisi wa mwisho mwisho.

After that life likawa tight mbaya, kiasi kwamba msosi ukawa shida. Zikaanza pasi ndefu kwa wakubwa, ila mimi na dogo tunakula asbh, mchana na jioni. Hapo mama ni ticha, ila elimu yake ilikuwa certificate tu nadhan na bado hakuwa na ajira rasmi, mshua ni mtu wa kuunga unga. Ilifikia kipindi chai tunakunywa na kiporo cha ugali, na kuna baadhi ya siku ugali tunachovya kwenye maji ya chumvi au tunalia ndimu (ugali na ndimu au limao)

Katika mihangaiko yake, kuna siku mzee alibahatika kupata vihela fulani hivi, sasa utata ukawa ni hiyo hela ifanyie kitu gani? Hapo wanadaiwa sehem kibao, kodi pia mwenye nyumba anadai, home mahitaji mengi hakuna n.k. Wakajadiliana sana wao kwa wao, mama akawa anasisitiza walipe kwanza madeni ili kutengeneza mazingira ya kukopa tena siku zijazo, ila mshua akawa anasita. Baadae mshua akamuuliza mama "Hivi ule mpango wa kujiendeleza na elimu bado unao?" Mama akaitikia ndio. Mzee akasema "Hii hela itasimamia elimu yako, japo haitoshi, ila huko mbeleni nitapata kiasi kilichobakia"

Nakumbuka mama alikataa kata kata, ila mzee nae akamwambia mimi ndio nishaamua na itakuwa hivyo, cha msingi uzingatie tu mazingira ambayo hii hela imepatikana. Huo mzozo ulikuwa mkubwa sana, mama akiangalia hali ya nyumbani na watoto tunavyopata tabu, akasema hawezi kwenda kusoma kipindi hicho. Mzee nae anasema hakuna wakumbadilisha alichoamua, japo hakuwa na uhakika na uhamuzi wake.

Hatimae mama alienda kusoma ( alienda chuo kipo Mhonda/Morogoro japo kumbukumbu hazijanikalia sawa), ila huku nyuma japo mshua alijitahidi kutupigania ila mambo yalikuwa tight sana.

Kutokana na ugumu wa maisha, mama alikuwa anashindwa kurudi home kipindi cha likizo. So alikuwa anafanya vibarua huko huko walau apate hela za kujikimu. Almost 2 years bila kuonana nae wala kuongea nae, maana hakukuwa na simu, sana sana tulikuwa tunapokea barua zake mara chache chache.

Kama kuna siku nilifurahi sana katika maisha yangu, basi ni ile siku ambayo mama alirudi tena home baada ya kumaliza kusoma. Nyumba nzima ilikuwa na furaha. Pure Happiness.

Mama alifanikiwa kupata kazi (kipindi kile walimu walikuwa hawasoti). Japo mshahara wake haukuwa mkubwa, ila walau uliweza kuendesha shughuli za kifamilia. Miradi ya mzee aliyonayo mpaka leo, yote ilianzia kwenye mikopo aliyokuwa anachukua Mama. Baadae walifanikiwa kujenga nyumba yao, then tukahamia huko. Maisha yalisonga na tulisomeshwa vizuri tu(japo wengine tulikuwa watukutu).

Right now wazee wangu wote ni wastaafu, na bado wapo pamoja kila sehemu.

Huwa namtaniaga mara kwa mara Mzee wangu kuwa kati ya wanaume waliobahatikaga kupata wanawake wazuri basi ni yeye. Nikimwambiaga hivyo huwa anachekaga sana. Mzee wangu huwa ananiambiaga kuwa wanaume ndio huwa tunaharibu mahusiano siku zote.

Jana nilikuwa naongea nae, akawa anasema "Nasikia vijana wa siku hizi mnasema wanawake ni vivuruge, hebu niambie wanawarugaga kivipi, then nitakuonesha wapi ulikosea" Then akaendelea kusema "MWANAMKE ANAWEZA AKAKUADHIBU LEO, KWA KOSA ULILOFANYA MWAKA JANA". So usije ukadanganywa na lile tabasamu unaloliona usoni mwake, kama ulimkosea au kuna sehemu ulikosea basi hakikisha umesolve ilo jambo kwa kuliongelea na kukubali ulipokosea.

Maana naona vijana wa siku hizi mkikosana, mara umemletea zawadi za maua au kumpeleka out then imetoka. Hayo yote yatasaidia kumrudishia mood yake tu, ila usije kujidanganya kuwa uliyofanya yamefutika, yatakurudia tu mbeleni. Women are bright since they are always driven by instincts, they need men as their guidence, so ukiweza kumguide mwanamke na ukaplay your role vizuri, utakuwa happy man"

******* ******** ********

Conversations zangu na mzee huwa nazifurahia sana, ila ugumu unakujaga kila mwisho wa maongezi lazima aniulize naoa lini. [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28].

My Father My Hero

Who is your Hero??

#Baharia_wa_nchi_kavu.

Analyse.
 
Yeyote aliyeplay vital role kwa wewe kuwa hapo. Hata kama ni wengi. Just tell us why him/her.
 
Kwa leo napita kimya ila ni best inspirational uzi kwa mwaka 2021.

Kichwa cha uzi wakati naanza kusoma huu uzi nikakumbuka kuna uzi wa mshikaji mmoja alikimbia nyumbani akapambana na mambo yakaenda ndivyo sivyo ndipo alipokutana na mshua wake kwenye msoto na mshua akamkazia hadi hatakaporudi home.

Ila ni moja ya nyuzi bora sana pia yenye maudhuhi kama haya.
 
Mkuu ndie huyuuuu Analyse
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…