Kwanini mnampakazia mzee warioba? Hivi alijifungia chumbani kwake kuandika rasimu? Hivi kuteuliwa kuwa mwenyekiti ndio nongwa hadi alaumiwe binafsi kuwasilisha maoni ya watu aliowauliza? Tumtendee haki.mzee huyu na tujue kuwa Nyerere sio Mungu na maneno na mawazo ya nyerere sio msahafu
Mwalimu Nyerere ambaye Le Mutuz anataka kuonesha kwa kuasisi Muungano wa kiini macho anastahili atukuzwe tu alishasema maneno haya:
Muundo wa Muungano, pamoja na kwamba hatutaki uwe ukitibuliwatibuliwa mara kwa mara, ni suala la sera,
si amri ya Mungu.Vyama vya siasa mbalimbali vinaweza vikawa na maoni mbalimbali kuhusu muundo unaofaa kwa Katiba ya nchi yetu.
Muundo utakaokubaliwa na wananchi walio wengi ndio utakaokuwa sehemu ya Katiba ya nchi yetu. uk 18
 
Labda ni vizuri kukumbusha kwamba shabaha ya baadhi yetu ilikuwa nikuunganisha nchi za Afrika Mashariki ziwe nchi moja. Na wakati Zanzibar na Tanganyika zinaungana, Kenya, Uganda na Tanganyika zilikuwa katikati ya mazungurnzo ya kutafuta uwezekano, wa kuungana. Kama jambo hilo, lingetokea,
nina hakika kabisa kwamba mfumo wa nchi mpya ambayo ingezaliwa ungelikuwa ni Shirikisho; au la Shirikisho la Nchi Tatu zenye Serikali Nne, na Shirikisho la Nchi Nne zenye Serikali Tano.Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili
- ya Zanzibar na ya Tanganyika - kuliko Tanzania yenye Serikali Mbili, ya Tanzania na ya Zanzibar. uk 11
link
Uongozi Wetu Na Hatma Ya Tanzania (by Nyerere)
Mwalimu alifanya kosa kubwa kuifuta(kuificha) serikali ya Tanganyika na baadae kufanya ukiini macho, mazingaombwe ya kulipoteza jina la nchi Tanganyika na kutuaminisha ni uhaini kulitaja au kuukosoa Muungano ambao siku zote umeonekana unaibua kero.
Kama umesoma hayo maneno ya Mwalimu hapo juu. Mwalimu alitambua mfumo sahihi wa Muungano unaoshirikisha nchi tofauti ni mfumo wa shirikisho na anaonekana kutubu dhambi ya kulifanyia mazingaombwe jina Tanganyika Kwa kusema kama Tanzania ina nia ya kuungana na nchi nyengine za Afrika Mashariki basi ni wepesi/rahisi zaidi kushirikisha serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar.
Na sio serikali ya Tanzania.