Baada ya mvua kusababisha utelezi uliotuletea maumivu makali hapo Chang'ombe kwa mzee wa Lupaso, ghafla nimemkumbuka sana shemeji yenu Mariah Carey. Tangu mechi iishe nimejifungia huku uwanja wa ndani taifa nasikiza nyimbo zake.
Kama hamjui acha niwajuze, tangu nikiwa shule ya msingi nilikuwa na ndoto za kuja kuishi na Mariah Carey. Ndoto hiyo ikanidokeza kuwa nilichotakiwa kufanya ni kujifunza muziki, hususan upigaji wa drums na magitaa, jambo ambalo lingenipa umaarufu mkubwa ambao ungemfikia nyota huyo na kuanza kuhaha kutafuta contact zangu.
Ndoto hiyo ikaendelea kunitanabahisha kuwa, Mariah angepata contact zangu baada ya kupata tabu sana. Kisha angenibembeleza sana niwe meneja wa bendi yake huku nikisimamia zaidi kitengo cha drums na upigaji wa vyombo vya muziki.
Usiriaz wangu kwenye kazi ukichanganya na utanashati wangu, vingemvutia Mariah Carey kiasi kwamba yeye mwenyewe angeniomba tuwe wapenzi. Na hapo ndoto yangu ingetimia rasmi.
Vibao vyake na sauti yake tamu vikawa tiba yangu. My All, Butterfly, Without you na We belong together, vikatupa umaarufu mkubwa duniani. Kina Eminem, P Diddy, na mashalobaro wengine kule Marekani wakaanza wivu na figisu, lakini msimamo wa shemeji yenu haukuyumba kamwe.
Mpaka naamka kutoka usingizini, mahusiano yangu na Mariah yalikuwa gumzo ulimwenguni. Watu wanaulizana, kampendea nini yule mswahili?
Miaka mingi baadaye nikaamua kumsimulia mke wangu ndoto hii niliyowahi kuota zamani, kwamba ashukuru, mke wangu alitakiwa kuwa Mariah Carey.
Sikutegemea! Mke wangu alikasirika sana, akataka kunipiga kofi, nikafanikiwa kulikwepa na kukimbilia nje. Tangu wakati huo mke wangu kafuta nyimbo zote za Mariah Carey kwenye simu yangu. Na ikitokea tunatazama TV pamoja halafu ikapigwa nyimbo ya Mariah Carey huwa anasonya na kwenda kuzima Main Switch![emoji24][emoji24]
Sasa najiuliza kosa langu ni lipi hapo? Ni wivu wa kawaida kweli huu? Wakati mwingine huwa nashtuka usiku wa manane, nakuta yupo macho na ananitazama kwa hasira. Nikimuuliza kulikoni mke wangu, anadai roho inamuuma sana kuhusu swala langu na Mariah Carey na hajui afanyaje. Inabidi nianze kumbeleza ndipo tunafanikiwa kulala[emoji27][emoji27][emoji27]
Sasa leo tangu mechi iishe, nimemkumbuka tena mke wa ndoto yangu, Mariah. Ninahisi sitarudi nyumbani. Nitakesha nikisikiza zile whistle notes zake. Ndiyo namna pekee ya kupona maumivu ya waarabu, na kusaka mzuka mpya wa kupindua meza kule Algeria.
Atakayeonana na mke wangu, amwambie mimi ni miongoni mwa wale mashabiki waliovunja geti wakati wanakimbilia tiketi za bure hapo taifa, na bado tumeshikiliwa rumande na polisi. Tena mmwambie polisi hawataki kuona mtu kituoni!
Always Be My Baby Mary