My vision: kocha Robertinho hastahili kupewa mkataba (kandarasi) ya muda mrefu kwa sababu zifuatazo

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Sijaona sababu ya Simba SC kuendelea na kocha ambaye.

Kaipokea timu kutoka mikononi mwa kocha Mgunda na kuishia Robo fainali katika michuano ya CAF tena robo ambayo imezoeleka kila mwaka.

Robertinho kashindwa kuchukua hata kombe la kufutia machozi kwa mashabiki wa Simba kombe la shirikisho Azam kaishia nusu fainali kwa kichapo Cha mbili bila.

Kila nikimtazama Robertinho kwa mbinu zake naona kabisa Mashabiki wa Simba wanakwenda kulia kilio kingine (kilio Cha ukiwa) kisicho na kombe ndani ya kabati.

Nilichokiona kwa kocha Robertinho ana talent kubwa ya kujua kushangilia tu.
 
Huwa nashangaa sana pale mwana Yanga kindaki ndaki kama wewe, ndo aiamlie Simba ni kocha gani anafaa, Labda nikukumbushe huyo anayemsema, hajawahi kufungwa mechi yyte ile na yanga, awe na Vipers au Simba, hivyo mpe heshima yake hlf anahitaji muda kujenga kikosi chake, hlf maswala ya kocha bora ungekuwa mwana Simba ndo utoe maoni yako, kwa hiyo unataka Simba ilete kocha ambaye Yanga itamfunga?
 
Kwani yanga ilifungwa na Robertinho au mangungu??

Nipe jibu la hili kwanza.
 
Dahhh

1. Ila Kuna watu ni MABINGWA WA KUANDIKA pumba.

2. INAWEZEKANA kweli wenye akili wakawa ni wawili tu.

3. Hivi HUONI kwamba unajaza server za Jamii Forum kwa kuandika PUNGA.

JARIBU KUANDIKA UZI AMBAO UTAACHA ALAMA.
JIFUNZE kwa AKINA
pascal mayala,
Robert herier.
Mshana Jr
Jack will Power.
Nk.

UKIPATA NAFASI UWE UNASOMA NA VITABU VINAONGEZA SANA MAARIFA.
 
Vijana WA KIMASIKINI siku NZIMA wanabishana Simba na yanga.

WATOTO WA kitajili wanapelekwa shule kubwa, na WANALAMBA vyeo.

ENDELEENI KUSHINDA VIJIWENI KILA DAKIKA SIMBA YANGA.
 
Vijana WA KIMASIKINI siku NZIMA wanabishana Simba na yanga.

WATOTO WA kitajili wanapelekwa shule kubwa, na WANALAMBA vyeo.

ENDELEENI KUSHINDA VIJIWENI KILA DAKIKA SIMBA YANGA.
Sawa mtoto wa bakhresa wasalimie huko Tanganyika schools.
 
Mbona sijaona jina lako hapo nikasome maarifa yako .
 
Pilipili usiyoila yakuwashia nini???


Au kwasababu unajua Nabi atabanduliwa back to back next season????maana hana history ya kumfunga wala kupata sare...

Bado yupo sana
 
Pilipili usiyoila yakuwashia nini???


Au kwasababu unajua Nabi atabanduliwa back to back next season????maana hana history ya kumfunga wala kupata sare...

Bado yupo sana
Uzuri post Kama hii ipo tu.
 
Nenda kashtaki CAS.
 
Sikubaliani na yote uliyoandika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…