My wife has spoiled my day!!

Analeta wivu wa kubomoa huyo na anataka akupande kichwani,pigaaaaaaa.....
Kuna wanaume wengine wanaoharibu sifa ya kuwa waume, moja wapo ni wewe. oa wako piga ua halafu tukukute Segerea ukinyea debe. Unaharibu sifa za ukoo wa Lasway
 
Kumnunulia zawadi ni sawa na kumrubuni akusamehe. Omba msamaha wa kweli na wa dhati. Ila kama hukukusudia do not waste your precious energies because in her eyes you are a very different man na kamwe hutoweza kurudisha pendo lile alilokuwa nalo hapo kabla ya kumdunda.
 
Kwa kumpiga mkeo sikuungi mkono hata kidogo maana si jambo ziri kwa jamii ya ss.....ila kama alikuuliza uko wapi na ukamwambia na kumwambia kuwa uko huru kuja na hakuja sioni sababu ya yeye kulalamika,km alihisi uko na mwanamke mwingine ingekuwa vyema aje hapo achukue nafasi yake au aje akuchukue mrudi,maana agekuwa amepata majibu yote na kukuzuia ww usiwe na mwanamke mwingine bila kusema chochote.....wasiwasi wangu isije ikawa ni mbinu yake ya kutaka kwenda mahali kwa kupitia ugomvi ambao ameuazisha na ww bila kujua umeumwagia petrol na kuwa mkali zaidi...usipotengeneza mapema na mkeo wenzio watamgonga utaona amefurahi na kesi imeisha kumbe wenzio ndo wamemfurahisha....take care kaka
 
Katika yote ya kusimulia ningekuwa mimi kwa aibu hiyo sehemu ya 'kumpa kipondo' mkeo nisingeweza kuisimulia, yani unaonekana una ego ya kizamani mshkaji wangu. By the way, jitahidi kutojibizana na mwanamke wako itakuondolea matatizo madogomadogo kama hayo. Na ukome kumpiga mkeo.
 
Kweli nijijitahidi sana kumuelezea hakuelewa ilichofuata ilibidi nitoe KIPONDO. Shida ya wanawake wetu wa kiswahili wanaishi kwa kuhisihisi tu.

hivi wanawake, wanaume wa aina hii mnawatoa wapi?
Mkew asipokuonea wivu wewe amuonee wivu nani? Shamba boy?
Halafu unamwita 'mwanamke wa kiswahili'?
Hivi unampenda na kumthamini mkeo kweli?

Shame on you.....

Kama una nguvu sana kwa nini usingechukua jembe ukaenda kulima? Angalau ungepanda kunde ungepata mboga?

Endelea kumshushia vipondo mkeo siku akipata wa kumbembeleza na kuuthamini mwili wake utakuja hapa kuomba ushauri.

Mwisho mwanamke hapigwi ngumi, na hapigwi na khanga maana ina maneno, mwanamke anapigwa na vits au rav 4.
 
Kwa style hii umuhimu wa jando na unyago ndo unaonekana....


 
We Swts Jumapili hii shetani yuko zake bize makanisani akitafuta waumini alifikaje huko Club...Hivi hamuoni na yeye ana zambi za kumtosha mpaka mumtwishe na za kwenu? Imeandikwa kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe..
 
Last edited by a moderator:
Mi nafikiri mtu ukishakuwa na familia, mambo ya club inabidi uache pembeni. Sasa we umerudi home na mkeo badala mkae chini mpumzike mjadiliane mambo ya family we unawahi club. hapendezi kabisa kabisa kwa baba wa nyumba, sijui watoto wanajifunza nini toka kwako!.
 
Mkuu kwa heshima zote zikustahilizo, that's not the way to go.
a) Mpaka saa 4 uko club, na ndoa/familia utailea saa ngapi? Kwa sababu kama mkeo anaona waume wengine wakilea zao saa hizo hakosei akishangaa wewe unamlea nani usiku huo(Its only logical akikuhisi una mwingine).
b) Hivi unajua mkeo alipokuwa kwao alifuzu kozi ya kuwa mtu mzima ndo maana wakakubali aolewe? Watu wazima wakikosa hushtakiwa kwenye vyombo sahihi kisheria, we ni nani alikuchagua kutoa adhabu hiyo ya kipondo?
c) Tafakari kisaikolojia ukimpiga mkeo hasara anayoipata ni kubwa na pia inareflect on you too...Kwa sababu unarudije kusema unampenda ilhali umeshamshushia heshima yake mbele ya wanaomzunguka? Na je in all this wewe huna kosa?
d) Mkuu narudia tena kwa heshima yote inayokustahili; You are very immature. You need to learn how to become a family leader. Nyie ndo mliosababisha wanawake wa sasa hivi hawana tena imani na uongozi wetu wa kifamilia..
 
Hivi kwa nini huwa mnatoa kipondo ?
hiyo sio solution..
 
ningemfaham mkeo ningemtafuta bpopote valipo nimliwaze baada ya hicho kichapo chako...women like to be cared bwana na siyo vipigo...kwa kuwa nina huruma kwa wanawake ningemfariji...
 
Ningekuwa mm ndo mkeo, hupati huduma yoyote hata salamu mwaka mzima, me nshamwambia mr wangu, cku ukinyanyua mkono ukanipiga tena, mana alikuwa ana tabia ya kunipiga vibao vya kijinga, co kipigo cha nguvu, itakuwa ndo mwisho we2, na naondoka na watoto, tangu hapo hajanigusa tena, anaongea mpaka anachoka. Ila kumpiga co suluhisho, akianguka afe, c utafungwa.
 
Pole ndugu yangu ila inasikitisha kumpiga mkeo nijuavyo Mimi ktk jamii ya kistaarabu wanawake hawapigwi, ila nahisi wewe ni mgeni na mashori hawa watu huwa hawataki kuambiwa ukweli. Ili uishi nao kwa Amani wanataka kudanganywa kwa akikuuliza upo wapi hata Kama upo gest ukiwadanganya wanaridhika
 
Kuna mtu alisema, kumpiga mwanamke ni sign ya weakness!

Ulivyokuwa unampiga ulitegemea mpigane au?

Ukimpiga ndio ataacha kuhisi kuwa unakuwa na wanawake wengine?

Ungekuwa kidume kweli, hata boss wako akikuudhi ungenpiga! Yes, boss wako si amekuudhi!

Yaani wanaume design yako bora usagwe na mwanamke mwenzio! Pfuuh!
 
Huoni hata haya kusema umemshushia mkeo kichapo! We ya kanumba na lulu hayajakufunza tu?
 
kaka,kaka,kupiga sio sifa kabisaaaa,next time usihadithie watu mambo ya kipondo, ni aibu sana! halafu uwe na tabia ya kupenda kutoka na mkeo,au kama unahitaji siku na rafiki zako na yeye mpe nafasi ya kuwa na rafiki zake. Rekebisha hali hiyo haraka sana kwa sababu wewe ndio umespoil siku yake.
 

Maneni matamu kweli kweki haya SWTS, nimeyapenda natamani niambiwe mimi.
 
Hukufanya vizuri kabisa kumpiga mkeo. Na kwa nini ukusirike anapokuhisi vibaya na kukuuliza? Huoni kuwa hasira inamanisha there is something you are hiding? Kama humcheat kwa nini ukasirike?

Na mwisho hapo ulipo hujisikii vibaya umempiga mwenzio, afu yy yupo kanisani. Huoni unajitengenezea laana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…