My wife has spoiled my day!!


whaaat! mkeo asipokupa talaka basi ana bwana mwingine, lol
 
Ingekuwa ni kule kwa wenzetu wala huo mda wa kuja kuandika hii habari yake JF asingeupata, angekuwa tayari yupo jela!.

Mwenyewe kaona sifa halafu kuna mwendawazimu mmoja nae kamsapoti eti anakupanda kichwani pigaaa. Siku hizi kuna watu wanaoa kufuata mkumbo bila kuelewa maana ya ndoa. Pole yake huyo mkewe, naombea amwache huyu bwana.
Kwavile yuko bongo ndo kapata muda wa kutuhabarisha usikute kawaambia na washkaji zake kujiona kidume..shwaiin kabisa!!
 
ke**ge asiye na manyoya .........yani unaona hili ndio lakuleta hapa si ushampiga hujafurahi bado halafu unadhubutu sema yy ndio kaharibu siku yako
 
We Swts Jumapili hii shetani yuko zake bize makanisani akitafuta waumini alifikaje huko Club...Hivi hamuoni na yeye ana zambi za kumtosha mpaka mumtwishe na za kwenu? Imeandikwa kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe..

naona ata mtoa mada kajificha,PetCash ucku mwema,nipo bigbrother
 
Last edited by a moderator:
We Balaa blue, how is ur wife,and how is urday
 


Kupigana ni mambo ya kizamani, na haswa yanafanywa na walevi au watu wasiokwenda shule, sijui wewe ni mmoja wao? Hakuna atakayekusifu kwa ujinga wa kumdhalilisha mkeo na inawezekana ulimdhalilisha mbele ya watoto na house girl. Usiseme kua uyaone, ila wewe bado hujakua, ungekuwa umekua usingefanya mambo ya kitoto. Mambo ya kitoto wanafanya watoto na wanaona fahari kusimulia kama wewe ulivyofanya. Elimika...
 

You have spoiled my day too. Unampiga mwanamke?? Marafiki zako ni muhimu kuliko familia? Get well soon. Nafsi itakusuta na siku zako utaziona chungu kuliko uchungu wa kuzaa.
 
Kwa hali hii kuna umuhimu wanawake baada ya kichenpati twende judo.ngumi mkononi hakuchapi mtu.hehehe

Judo mbali! Kwani we huna kastuli chumbani mwenu? Huna mazoea ya kuweka walau glass moja juu ya stuli? Alafu katika zile chupa zinazoisha vinywaji usiwe unaziondoa zote, jitahidi uwe unabakiza hata moja kwa sababu ya kazi!!
 
Nakushangaa maswali rahs majibu magumu or maswali magumu majb rahs. Unadhani kwnini amekule ej hz hbr asubh? Inaonekana ulipewa chakula cha ucku ukawa kibogoyo ukaishij kukipaka mate wkt c kawaida yk. Fungua akili acha kutumia nguvu yatakukuta ya yanga 5-0
 
Kwanini haukumwambia mtoke wote???

yaani wy ulienda mwenyewe??? kwani alikuwa busy au???

Sijaelewa kiswahili cha mwishoni ila kama ulimpiga, wewe ni nani kumpiga mtoto wa watu? tabia mbaya sana, tena inabidi akushitaki kwa kumpiga ufundishwe adabu na ssytem. Nyie ndio wanaume msiohitajika duniani.
 
Judo mbali! Kwani we huna kastuli chumbani mwenu? Huna mazoea ya kuweka walau glass moja juu ya stuli? Alafu katika zile chupa zinazoisha vinywaji usiwe unaziondoa zote, jitahidi uwe unabakiza hata moja kwa sababu ya kazi!!

Yata kukuta ya mtoto lulu ohooo! sisi vidume tunajidai wababe sana ila wengi wabovu, gusa kidogo jumba bovu likuangukie.
BTW hivi wanandoa wa skuhizi bado wana pigana pia? kweli wakti wangu bado haujafika.bado niponipo mama.
:israel:
 
Analysis yangu ya huyu Blue Balaa; huyu ni mtoto wa watu na alikuwa anamuwahi BF wake na huyu mkewe kisha mstukia, alipoulizwa katika kujitetea, mkewe akagonga Ikulu kwa kumwambia kama ulikuwa huna mwanamke basi ulikuwa unamuwahi basha wako, hapo sasa! Mamaa kagonga Ikulu, kujitetea na kujifanya yeye ni rijali sana ndio ikabidi aangushe "kipondo".

Kwa mtazamo wangu Blue Balaa ni chakula ya wenzake, hakuna mwanamme anaeweza kuja humu kujisifu eti katowa "kipondo" kwa mkewe.
 

Amekosea kukuhisi, ni bora angekuja ahakikishe, ila siku hizi wataalam wanasema ukiona mkeo kila saa anatuhumu una mtu, ujue anatafuta sababu ya kuhalalisha vyake

Ila kupiga soo mshkaji:wacko:
 
Ungejisikiaje mkeo na mimi nakuibiaaaaa......wacha tamaa!!!!
 
Ndoa za vijana hizi,kazi sana!
 
Mungu na aiamshe akili yako utambue ulivomkosea mkeo na urekebishe na ujiapize kutorudia tena,jitahidi kukotrol hasira zako na kutumia busara zaidi kumsoma mkeo je anapokubali jambo hua anamaanisha ndio au hapana!
 
mmh, kwa hiyo unatamani umpige tena akitoka kanisani kwa sababu amekuacha peke yako nyumbani
 
Blue,
Mwombe radhi mkeo.
Kipigo sio utatuzi wa matatizo ambayo inaonesha umeyasababisha wewe mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…