pole kwa tatizo, ila hilo si jambo geni, ni moja kati ya vijimambo vya kuishi wawili, pana mambo kadhaa ya kuangalia.
Uelewe kwamba mwanamke anapoolewa anahitaji uhuru na nafasi ya kuthaminiwa kama yupo kwake, inawezekana kuwepo kwa ndugu kunafanya thamani ya kuwepo kwake isionekane anakuwa kama mtoto anayelelewa haina tofauti na alipokuwa naishi kwa wazazi, hivyo mpe nafasi mkeo, na umthamini na kumuonyesha kuwa ndugu wapo pale kwa muda tu ila yeye ndio mama!!
Je wanapokuwepo ndugu unakuwa na nafasi ya kukaa na kuongea na mkeo, au ukifika home basi wewe na ndugu tu na kusahau kuwa mkeo anahitaji kuongea nawe,
je ndugu wanamsaidia mama au msaidizi wa kazi majukumu ya nyumbani?
je mama ana uhuru wa kuwatuma au kuongea nao, au wao ndugu ndio wameshika hatamu kwa maana kila kilichopo ndani ni mali ya mwanamme ( ndugu yao) an hivyo dharau kwa mama!
Unaweza ukatafuta nafasi ya kuzungumza na mkeo kuhusu familia na kama paan lolote lililopo baina yake na watoto mnaoishi nao; au fanya uchunguzi wewe mwenyewe kwa kuangalia style ya maisha hapo ndani utagundua kama pana tatizo au la!
ila ushauri wa mwisho ni kama walitangulia, ndugu mara nyingi ni chanzo cha migogoro, na hatuwezi kupingana na maisha yetu ya extended family, ila kama unaweza kulizuia hili kwa kuwasaidia kwa kule walipo itakuwa ni vema na busara zaidi kuliko kuwa na familia kubwa, kuiangalia familia ya namna hii ni jukumu kubwa kwa mama, haswa kama ndio ndoa changa anahitaji muda mwingi wa kuwa na mumewe!!