MySoka: The Home of Football Fans

MySoka: The Home of Football Fans

MySoka

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2018
Posts
209
Reaction score
297
This is special thread for all football best fans

News and rumors around the earth.

Kwa habari za kambumbu na tetesi za usajili kutoka kote ulimwenguni.Pitia hapa.

MySoka
 
Kiungo wa kati wa Aston Villa na England Jack Grealish, 25, huenda akasalia katika klabu hiyo msimu huu wa joto, baada ya Manchester City na Manchester United kushindwa kufikia bei ya Villa ya £130m, kulingana na nahodha wa zamani wa Villa Gabriel Agbonlahor. (Talksport)
 
Andrea Pirlo na kocha wa zamani wa Chelsea Maurizio Sarri wanawania nafasi ya ukufunzi katika klabu ya Everton. (Calciomercato, in Italian)
 
Kiungo wa kati wa Manchester City na Brazil Fernandinho, 36, na mshambuliaji wa Newcastle na England Andy Carroll, 32, wamejumuishwa katika orodha ya klabu zao za wachezaji watakaoondoka ambayo ilichapishwa na Ligi ya Primia. Hata hivyo klabu zina hadi tarehe 23 Juni kutuma orodha zao mwisho.. (Premier League)
 
Manchester City, wanakaribia kumsajili kiungo wa kati wa Fluminense Metinho,18, ambaye anafahamika kama "Paul Pogba wa Brazil". (Goal)
 
Chelsea hawajapinga uwezekano wa kumuuza winga wa Morocco Hakim Ziyech msimu huu wa joto huku AC Milan na Napoli zikionesha nia ya kutaka kumnunua kiungo huyo aliye na miaka 28 nafasi ikitolewa. (Calciomercato - in Italian)
 
Paris St-Germain wanapania kukatiza mpango wa Barcelona wa kumnunua kiungo wa kati wa Uholanzi Georginio Wijnaldum, 30, ambaye mkataba wake Liverpool unamalizika mwisho wa mwezi huu wa Juni. (ESPN)
 
Everton na West Ham wanamtaka mshambuliaji wa Lazio na Argentina Joaquin Correa, 26, baada ya klabu hiyo ya Italia kuonesha ishara ya kumuuza kwa karibu paundi milioni 30 ili waweza kufadhili mpango wa kuwasajili wachezaji wapya. (Italy24News)
 
Liverpool wanataka kumuuza kiungo wa kati wa Serbia Marko Grujic msimu huu. Hertha Berlin, ambako mchezaji huyo alikuwa kwa mkopo kati ya mwaka 2018 na 2020, sasa wanataka kumnunua baada ya bei yake kushuka hadi euro milioni 14 (£12m). (Berliner Kurier, in German)
 
Kiungo wa kati wa Barcelona na Bosnia Miralem Pjanic, 31, huenda akajiunga tena na Juventus msimu huu wa joto baada ya kujadiliana na Massimiliano Allegri, ambaye anatarajiwa kuchukua usukani baada ya Andrea Pirlo kupigwa kalamu. (Calciomercato - in Italian)
 
Kiungo wa kati wa Barcelona na Bosnia Miralem Pjanic huenda akajiunga tena na Juventus
 
Barcelona inajiandaa kukamilisha mchakato wa kumsajili mshambuliaji wa Lyon na Uholanzi Memphis Depay, 27, kwa mkataba wa miaka mitatu. (Sport)
 
Kocha wa Roma Jose Mourinho anajiandaa kuzihangaisha klabu za Uingereza kumpata kiungo wa kati wa Gambia Ebrima Darboe ,19, kuhakikisha haondoki klabu hiyo. (Il Tempo via Tuttomercato Web, in Italian)
 
Bayern Munich wanajiandaa kumsajili kiungo wa kati wa Atletico Madrid na Uhispania Saul Niguez, 26, kwa kima cha euro milioni 80 (£68.7m) baada ya Rodrigo De Paul, 27, ambaye walikuwa wakimnyatia kupigiwa upatu kujiunga na klabu na mabingwa hao wa La Liga (Radio Marca)
 
Mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 28, ameieleza Crystal Palace kwamba anataka kuondoka kabla ya msimu wa mazoezi kuanza. (Times)
 
Mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 28, ameieleza Crystal Palace kwamba anataka kuondoka kabla ya msimu wa mazoezi kuanza. (Times)
 
Kocha mpya wa Real Madrid Carlo Ancelotti yuko tayari kumtafuta aliyekuwa mshambuliaji wa iliyokuwa klabu yake Everton raia wa Brazil Richarlison, 24. (Football Insider)
 
Everton iko tayari kutoa ofa ya mkataba wa miaka mitatu kwa aliyekuwa kocha wa Wolves Nuno Espirito Santo, 47. (Nicolo Schira via Star)
 
Back
Top Bottom