Kiungo wa kati wa Manchester City na Brazil Fernandinho, 36, na mshambuliaji wa Newcastle na England Andy Carroll, 32, wamejumuishwa katika orodha ya klabu zao za wachezaji watakaoondoka ambayo ilichapishwa na Ligi ya Primia. Hata hivyo klabu zina hadi tarehe 23 Juni kutuma orodha zao mwisho.. (Premier League)