Mzao wa Tippu Tip uko wapi?

Duuh,umenifunza jambo hapa.mimi kaliua ndo home ila hizi mambo zilinipita kambo
 
Tupo pamoja mkuu 13 mega pixel lkn gwiji wa haya yote ni Mzee Mohamed Said tunasubiri atie neno lake ktk uzi huu!!Maana huyu ni Mmanyema huyu,babu zake walikuja Kkoo na misafara ya Watumwa na wapagazi(just kidding)
Barafu,
Mmoja wa kitukuu cha Tippu Tip ni dada yangu na nimeirusha
hii post uwani kwake ili akiamka kuanua nguo zake aione.

In Shaallah tumsubiri.
 
Barafu,
Mmoja wa kitukuu cha Tippu Tip ni dada yangu na nimeirusha
hii post uwani kwake ili akiamka kuanua nguo zake aione.

In Shaallah tumsubiri.


Kwa hiyo unaona hiyo ni sifa kuwa na uhusiano na huyo mchotara na muuwaji Tipp Tip? Mimi ningekuwa raisi wa JMTZ watu kama ninyi ningeweka ndani na kuwafilishi wote!
 
Kwa hiyo unaona hiyo ni sifa kuwa na uhusiano na huyo mchotara na muuwaji Tipp Tip? Mimi ningekuwa raisi wa JMTZ watu kama ninyi ningeweka ndani na kuwafilishi wote!
Barbarosa,
Wapi mimi nimesema kuwa naona sifa?
Hata hivyo mtu huwei kukataa asili yako kwa ajili ya historia.

Historia ina mambo ya kushangaza sana.
Soma historia ya uhuru wa Tanganyika.

Sykes Mbuwane aliingia Tanganyika kama mamluki wa Wajerumani
kuja kupigana na Chifu Mkwawa, Kalenga na Abushiri bin Salim,
Pangani.

Mtoto wa Sykes Mbuwane, Kleist Sykes akajakuwa mzalendo na
Mtanganyika aliyewasha moto wa kupambana na ukoloni 1929.

Watoto wa Kleist Sykes, Abdulwahid, Ally na Abbas wakaja kuasisi
TANU 1954.

Lakini ukiangalia nyuma asili ya hawa wote chanzo chao ni askari mamluki
aliyeingia Tanganyika mwisho wa 1800 wakiongozwa na Herman von
Wissman
amebaba bunduki kuja kupigana na wananchi wa Tanganyika ili
nchi hii itawaliwe na Wajerumani.

Angalia sasa ajabu ya historia.

Sykes Mbuwane alikuwa askari mamluki wa Wajerumani akapigana na
Chifu Mkwawa na Abushiri bin Salim wazalendo wa Tanganyika.

Kleist Sykes akapigana WW1 upande wa Wajerumani dhidi ya Waingereza
(1914-1918).

Watoto wake Abdul na Ally wakapigana WWII na Waingereza dhidi ya
Wajerumani (1938-1945).

Hapo chini ni kaburi la Bi Miski Simleleo.
Bi. Miski ni shangazi yake Chief Adam Sapi Mkwawa.

Maana yake ni kuwa Bi. Miski ni mjukuu wa Chief Mkwawa.

Huyu Bi. Miski ndiyo mama yake Bi. Mruguru biti Mussa Ngomangando,
kabila Mndengereko, ambae ndiye mama yao Abdul, Ally na Abbas.

Kwa lugha nyepesi ni kuwa akina Mkwawa na Sykes ni ndugu wa damu
ingawa hapo mwanzo Wazulu mamluki walipokuja Tanganyika walikuwa
maadui.

Hii ndiyo sababu fuvu la Mkwawa liliporejeshwa Tanganyika mwaka wa 1955,
Chief Adam Sapi Mkwawa alimualika Abdul Sykes na Dossa Aziz katika
sherehe ile iliyofanyika Kalenga.

Wanamajlis,
Mnasemaji kuhusu maajabu haya ya historia ya Tanganyika?
Wapi wanahistoria waonyeshe kidole cha lawama?


Kaburi la Bi. Miski Simleleo, Makaburi ya Kisutu
 
Mashaallah wallah historia ina maajabu yake. Mungu akuzidishie. Ila picha haifunguki.
 
Ummie-Mahfoudha Alley Hamid Hamid:

Wagonjwa hao.
Wape hadithi ya mwana kondoo na mbwa mwitu.

Asojuwa maana haambiwi maana.

I never argue with fools as people might not be able to tell the difference.
Being a descendant of Tip Tip does not shame me at all.

I'll always stand tall for who I am.

A lot of fibs and dramatization has been added in Tip's life to the extent that some people don't know where truth ends and fiction starts.

I don't want to enter into an argument with nincompoops some who have just managed to learn how to write their names.

Thanks brother but I retain you as my advocate if you accept a retainer of sisterhood love.
 
Asante sana Mzee wetu Mohamed Said ndio maana mimi nilisema historia haitakolea kama hatutakuita hapa barazani.Mimi nimetembela sana pale Kwihala Tabora,nikajifunza historia ya Tippu Tipu na vizazi vyake
 
Kwahyo we Barbarosa ulileta mada ili upate nafasi kukashifu watu? Uzuzu huo

Fundisi na Wanabarza,
Nimeweka picha (rare photos) kuhusu mada hii.
Ingieni tena hapa:

Mohamed Said: MAAJABU YA HISTORIA: BI. MISKI SIMLELEO SHANGAZI YA CHIEF ADAM SAPI MKWAWA BIBI YAKE ABDUL SYKES
 
Kwa hiyo unaona hiyo ni sifa kuwa na uhusiano na huyo mchotara na muuwaji Tipp Tip? Mimi ningekuwa raisi wa JMTZ watu kama ninyi ningeweka ndani na kuwafilishi wote!
Kaka acha kumlisha mtu maneno na ukamuhukumu,halafu mbona maalim hajajisifia? Hapa watu wsnatafuta ukweli kuhusu historia yetu wewe unaleta uchochezi,utafungwa shauri yako
 
Hakika maalimu,wewe ni historian wa ukweli,nichukue wasaa huu kukuomba unishirikishe katika kazi zako unazokusudia kuzifanya nipate kujifunza mengi kutoka kwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…