“Wazazi na walezi, je, mnaona umuhimu wa mabinti wenu kujihusisha na siasa?
Je, mko tayari kuwaunga mkono katika safari hiyo ya uongozi na mabadiliko?
Tushirikiane mawazo!
Mimi mke wa mtu siwezi kumruhusu awe kiongozi.
Msimamo wangu ni tofauti kidogo na watu wengine na naamini Kwa mitazamo ya watu naweza kuonekana ni mtu wa ajabu lakini katika kuhakikisha thamani ya mwanamke inakuwa juu zaidi kulingana na Mila na desturi zetu za kiafrika Bado naamini mwanamke hawezi kusimama kuongoza watu(wanaume).
Ebu tuanze kuchambua kulingana na Familia, koo, jamii, na Dini zetu.
Kwenye familia zetu Bado tunaona baba ndie kiongozi wa familia.
Kwenye koo zetu Bado tunaona viongozi wa ukoo ni mwanaume na hata viongozi wa matambiko Bado ni wanaume.
Kwenye jamii zetu hasa tukihusisha masuala ya ndoa Bado tunaona wanaume ndo wanaooa wanawake na mwanamke ambaye ataolewa jina lake linabadilika na huitwa na kutambulika Kwa jina la mume wake na watoto atakao wazaa pia wataitwa Kwa jina la mume wake.
Kwenye Dini zetu hasa Dini ya kiislamu na kikristo Bado viongozi wa Ibada ni wanaume.
HITIMISHO: Sina lengo la kuvunja Nia na nguvu ya mwanamke Bali Nia na Lengo ni kuwaambia wanawake kwamba uongozi uanzie nyumbani katika ngazi ya mke na mume kama wanazani ni jambo halali na ni haki kwao.