Mzazi mwenzangu ananilaumu na kunitangaza kwa ndugu zangu kwamba nimekataa kumsomesha mtoto wangu!

Mzazi mwenzangu ananilaumu na kunitangaza kwa ndugu zangu kwamba nimekataa kumsomesha mtoto wangu!

Shamkware

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2013
Posts
1,750
Reaction score
2,283
Poleni na majukumu wana jamvi, Binafsi staki kuwachosha, Baali nina jambo ambalo naomba kushea nanyi ili hata kupata uzoefu au hata idea tu maana maarifa elimu na uwezo wa kufikiri niliona nao mimi haiwezi kuwa sawa na mtu mwingine.

Iko hivi mimi ni mwnaume na naishi dsm nina mwanamke ambaye nilizaa nae mtoto mmoja wa kike ana miaka 7 sasa, Tangu mtoto kuzaliwa mimi kama baba nilihakikisha anapata kila kitu ambacho kiko ndani ya uwezo wangu kutimiza mahitaji muhimu kadri ya uwezo ikiwemo bima ya afya. Mtoto alikua vizuri nashukuru Mungu kwa hilo.

Alipofikisha umri wa kwenda shule tukaongea na mama yake vizuri na tukakubaliana mtoto asome kwenye shule za kawaida kwa sababu ya uwezo na kipato tunachoingiza kwa mwezi. Mtoto akaaandikishwa shule ya msingi na akaanza darasa la kwanza, Ulipofika mda wa kuingia darasa la pili mama mtu akamhamisha mtoto bila hata kuniuliza au kunitaarifu tu, Akamtoa shule ya kawaida na kumpeleka shule ya private ambayo ada yake kwa mwka kipindi hicho ilikuwa ni 1,900,000/= (Milioni moja na laki tisa) kwa sasa ni almost 2,300,000/= million mbili na laki tatu).

Sasa siku moja nilimpigia simu bibi yake mtoto (yaani mama yake na baby mama) kama kumsalimia tu ndio akaniambia niandae ada mtoto amehishiwa shule ya private. Nikashangaa na kumuuliza mbona sina taarifa hiyo na imekuwaje mmefanya hivyo bila kunishirikisha? Akasema yeye hajui alijua nimejulishwa labda nimuuliza mama mtoto!

Nilipompigia mama wa mtoto kumuuliza why umehamisha mtoto bila kuniambia?! Akanijibu mtoto wangu hawezi soma Saint Kayumba hivyo nimeamua kumhamisha mwenyewe na nitalipa ada mwenyewe hata usipo lipa wewe haitanishinda! Nikamsihi mno na kumwambia kuhusu future na kumweleza kama atasoma shule ya kawaida tutakuwa comfortable kumtengenezea mazingira mazuri tu ya kufaulu vizuri asome kwa furaha! But akakataa kata kata!

Ilikuwa ugomvi na nikaambiwa mimi baba gani sijali na sina mapenzi na mtoto kwanini nimsomeshe shule za saint kayumba, But ukweli ni kwamba mshara wangu haufiki hata milioni moja na tayari na mimi nina familia so nilijua siwezi aford ukilinganisha na pesa niniayoipata kwa mwezi. Actually yeye ananizidi mashara pengine nikajua hiyo ndio inampa nguvu kusema yote hayo.

Mwisho wa siku mimi nikabaki na msimamo wangu wa kutoa pesa ya mahitaji tu amabayo nilikuwa naitoa kila mwenzi tangu mwanzo, kimsingi huwa natoa 100,000/= kila mwezi kama pesa ya mahitaji ya mtoto!.

Tukaenda hivyo kwa mda mcheche, ikafika kipindi akaanza kunisumbua kuwa nilipe ada ya mtoto, Binafsi nilimwambia sina na badala yake nikaendelea kutotoa pesa ya mahitaji tu ya kila mwezi na hyo nimekuwa nikitoa kwa mda wote na sijawahi kukosa kutoa. Nikamwambia alipe ada kama alivyosema anaweza wala hanitegemei! Ama adundulize hiyo nayotuma kila mwezi ada ikifika alipe kwani mimi sina pesa inyingine napo hakunielewa.! Sasa Imefika hatua anamwambia mtoto wangu kwamba baba yako amekataa kukusomesha, mara apigie simu ndugu zangu na marafiki na akilalamika na kuwaambia nimekataa kusomesha mtoto!

Nimemwambia kama ameshindwa anipe mtoto wangu nimchukue na niishi nae mimi nimtafutie shule nyingine ambayo kidogo iko affordable pia hataki, yeye na mtoto wanaishi Mwanza mimi niko dsm na mtoto yuko darasa la tatu sasa!

Sasa ebu niambieni jamani nafanyaje katika hili na hasa kwa mama mtoto kama huyu na jeuri kiburi hasikilizi la mtu isipokuwa alopanga yeye!

Je, niapambane tu nilipe ada ama nikaze tu!
 
Poleni na majukumu wana jamvi, Binafsi staki kuwachosha, Baali nina jambo ambalo naomba kushea nanyi ili hata kupata uzoefu au hata idea tu maana maarifa elimu na uwezo wa kufikiri niliona nao mimi haiwezi kuwa sawa na mtu mwingine.

Iko hivi mimi ni mwnaume na naishi dsm nina mwanamke ambaye nilizaa nae mtoto mmoja wa kike ana miaka 7 sasa,
Je niapambane tu nilipe ada ama nikaze tu!
We endelea kutoa Hela za matumizi,mama yake alipe ada kwa sababu ana uwezo,Kaa na huo msimamo
 
Bahati Mbaya Wanawake wengi hasa WA mjini ndio wapo kama huyo shemeji yetu hapo.

Ninakesi za Aina hizo nyingi Mno.
Kuigaiga mambo na kutaka kujionyesha Kwa Watu ndio kunawatesa wengi.
Tena Hilo suala la English medium ndio tatizo,,yaani wadada tumekuwa Kama ma hamnazo......mtu huna uwezo,na mzazi mwenzio Hana uwezo unaforce,matokea katoto kila muhula kapo nyumbani for two weeks kamefukuzwa maskini ya Mungu
 
Tena Hilo suala la English medium ndio tatizo,,yaani wadada tumekuwa Kama ma hamnazo......mtu huna uwezo,na mzazi mwenzio Hana uwezo unaforce,matokea katoto kila muhula kapo nyumbani for two weeks kamefukuzwa maskini ya Mungu

Kabisa hivi tunaongea mtoto yuko nyumbani amefukuzwa ada
 
Kaka Hayo unayopitia hata mimi ni hivo hivo yaan ni copy and paste
Kwanza jisimamie na simamia kile unacho kisema na kukiamini, ujue wanawake hua wana tabia ya kujaribu. Na wengi wanateswa na wanao wazunguka kwamba watoto wao waishi, wavae, wasome kama watoto wa wengine.

Kama mimi ningekua wewe hata pesa ya matumizi nisingekua nampa.

Hawa wazazi wenza hua wanajiona hawana cha kupoteza kwa mwanaume ambae amesha oa, kwahiyo sasa niwewe kuongea na mkeo ili mumchukue mtoto wako na alelewe kama vile wewe unavyo taka.
 
Kabisa hivi tunaongea mtoto yuko nyumbani amefukuzwa ada
Nenda ukamchukue mwanao man, ukiona baba na mama wanaishi maisha yao tofauti then mtoto wanampeleka kwa bibi hilo ni kosa kabisa mkuu.

Kachukue mwanao na umlee vile unavyoona inafaa, huyo mama wa mwanao atakuharibia mtoto sababu atamlisha mambo ambayo mtoto hapaswi kuyasikia.
 
Hashauliki mkuu nishajaribu sana!
Acha kumpa matumizi na hana cha kukufanya, zaidi atakushtaki dawati au ustawi. Kule ukiitwa wenenda na ukasimamie kwamba unamtaka mwanao kwasababu mama yake ameshindwa kumlea na amempeleka kwa bibi yake.

Pia ongezea kwamba hauna imani na mama wa mtoto wako kwasababu haujui kama kweli pesa unazo mpatia anamhudumia mwanao.
 
Back
Top Bottom