Mzazi wako alikutelekeza wakati wa malezi na makuzi ana stahili zipi kutoka kwako?

Mzazi wako alikutelekeza wakati wa malezi na makuzi ana stahili zipi kutoka kwako?

Braza Kede

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
3,840
Reaction score
6,844
Huyu ni mzazi wako halali ila tu ndoivo hakuhusika na malezi wqla makuzi yako ukiwa mdogo.

Anaweza kuwa ni baba au mama yako halali kabisa ila hakuwepo wakati wa malezi na makuzi yako.

Bila kujali sababu za kutokuwepo kwake cha msingi hakuwepo na wala hakuhusika na malezi wala makuzi yako hadi unafika hapo ulipo sasa una meno 32.

Kwa sasa mzazi wako huyu ni mtu mzima sana au mgonjwa, kifupi hajiwezi tena.

Je mzazi wako halali wa aina hii anastahili zipi hasa? maana hakuna ubishi kuwa wewe ni mbegu yake halali toka maungoni mwake.

Je ni wa kupatiwa posho ya kujikimu kimaisha huyu?

Je anastahili kutunzwa kwa malezi mema mfano matibabu n.k maana saizi yeye hajiwezi tena?

Je anastahili kujengewa huyu kama hana pakujistiri?

Je ni wa kukarabatiwa nyumba yake iliyochakaa huyu?

Je huyu ni wa kupetiwapetiwa na kuchekewa kwa bashasha bana maana saizi kaishajirudi kitabia anacare?

eti wakuu?

ila mimi nazan anastahili ivyo vyote na hata vya ziada kama vipo maana mzazi ndo baraka yako mbinguni.
 
Mzazi ambaye hajawajibika kumtunza mtoto bila sababu za msingi hana haki yeyote ya kudai fadhila kutoka kwa mtoto.
Hata hivyo yote yanakuwa chini ya maamuzi yako ukitaka unaweza kumsaidia usipo taka unamuacha ww fanya kitu kitakacho kupa furaha.
 
Unaweza kumsadia kadiri ya uwezo wako.
Ikiwa tutawatendea wema wanaotutendea wema hapo tunakua tunalipa wema. Ikiwa tutawatendea wema wasio tutendea wema tunafanya wema mkubwa sana.

Ikiwa tunawasaidia watu tusiowajua kabisa nadhani kumsaidia huyo ambae unajua ni baba yako ni Jambo jema.
Mambo mengine yaliyotokea nyuma tunayaacha maana hatujui sababu ni nini na huenda akipewa nafasi nyinginee ambayo hana angejirekebisha na kuwa mtu mwema.

Tenda wema usiige ubaya.
 
Naunga hoja
 
Mzazi ambaye hajawajibika kumtunza mtoto bila sababu za msingi hana haki yeyote ya kudai fadhila kutoka kwa mtoto.
Hata hivyo yote yanakuwa chini ya maamuzi yako ukitaka unaweza kumsaidia usipo taka unamuacha ww fanya kitu kitakacho kupa furaha.
🤝🙏asante mkuu ushauri muruwa
 
No matter what mzazi ni mzazi kama una uwezo wa kusaidia fanya kile unaweza
 
Kwenye Dini yetu,mzazi ana nafas kubwa mno tena mno eidha amekosa au hajakosa as long as ni mzazi.. Asee nafas yake ni kubwa kubwa mnoo….
Lakini pia kwenye hio dini mzazi alikuwa ana jukumu la malezi kwa mtoto wake, kipi kilicho tokea hata alikimbia jukumu lake kwa mwanawe/wanawe?. Wakati huyu mtoto anakuwa yeye alikuwa wapi?. Kwanini ajitokeze Wakati yeye anahitaji msaada kama mzee lakini hakujitokeza
Wakati mtoto anahitaji msaada kwa mzee wake?.

Ama tudin tudan
 
ila ubaya ubwela

kwani wewe ulipo acha kukuhudumia ulikuwa vp, nawe acha pia atasaidiwa na wengine

lakini ukiacha na mzazi akafariki hutakuwa na aman maisha yako yote

msaidie kadri ulivyo jaaliwa
 
Wakati mwingine huwa dharau za mama wa mtoto.unaweza kuwa unatoa matuzimizi vizuri ila haitaji kushirikisha kwa lolote anahitaji kwako ni pesa tu
 
Zingatia wanaosema aonewe huruma ni jinsia 'me. Sijui nirudie mara ngapi, finali uzeeni ndio hii. Kuchezea watoto wa watu na kutelekeza watoto hamjambo, uzee ukipiga hodi unadai fadhila. Zikatafutwe huko huko zilikotapanywa
 
ko kwa lugha nyepesi umesema kama mbwai iwe bwai
 
Binafsi sikutengwa, ngumu kuzungumzia situation ambayo hujawahi pitia.
 
Binafsi sikutengwa, ngumu kuzungumzia situation ambayo hujawahi pitia.
 
Back
Top Bottom