Mzazi wako ndio mungu wako wa dunia

Mzazi wako ndio mungu wako wa dunia

Abuu Said

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2015
Posts
4,010
Reaction score
4,763
Heshima kwenu Maintelegencia wa Jf.
Katika huu Uzi kuna jambo moja kubwa linalojadiliwa na kukosa Jibu la moja kwa moja.
Kuna huu mjadala wa Mungu mkuu kiongozi wa ulimwengu watu wanajadili uwepo wake na ufalme wake.
In short Mzazi wako ndio Mungu wako wa Dunia hii yeye ndiye anaekupa baraka katika Maisha yako ya Duniani.
Mzazi wako ndiye anaekuonesha njia za kupita ili uishi kwa Amani na mafanikio ktk Dunia hii.
Huwezi kufanikiwa jambo ambalo mzazi wako hajaridhika nalo mafanikio ya mtu yanatokana na Mzazi wake.
Mzazi wako ndiye anaekuonyesha ni nani Mungu wako wa Ulimwengu wote kwa ujumla anataka nini na hapendi nini.
Mzazi wako anakuonyesha ni jinsi gani ya kumuabudu Mungu mkuu wa ulimwengu.
Fanya kile ambacho mzazi wako anataka ufanye acha kile ambacho mzazi wako hataki ufanye hapo ndipo utauona Ufalme wa Mungu hapo ndipo utakapofanikiwa Maisha yako kabla ya kifo na baada ya kifo.
Kama mafundisho ya mzazi wako yamepotosha basi yeye ndie wa kulaumiwa.
Katika ulimwengu wa sasa hakuna alieshushwa kila mmoja ametokana na Wazazi wake.
Nihitimishe huu mjadala wa Mungu hauwezi kuisha kwa kujadili maandiko ya Vitabu ambavyo hujui mwanzo wake.
Ili uishi vizuri duniani fuata yale ambayo Mzazi wako anakuelekeza.
 
Wengne wapotoshaj 2 tena wamekuwa chanzo cha matatzo meng yanayotokea ulmwengun mwamn mungu
 
Kwa hiyo ukifa unarudi tumboni kwa baba yako

swissme
 
Ufuate anayokuelekeza hata kama havikupi furaha??
Akuchagulie cha kusoma, akuchagulie kazi, akuchagulie mke/mume na atarun familia yako hakyanani. .
Wazaz ni kumthamini, kumuheshimu na kusikiliza ushaur wake but uwe una final say. .
Wazaz wengi wanaishi kwa macho ya watu, wakina Fulani watatuonaje sisi wewe ukifanya hivyo. . Ulimwengu wa sasa unahitaji daring people not safe players
 
Wengne wapotoshaj 2 tena wamekuwa chanzo cha matatzo meng yanayotokea ulmwengun mwamn mungu

Yeah, sio wazazi wote ni wazuri kwa watoto wao, ,na kadiri siku zinavyoenda tunashuhudia maovu mengi wazazi wanafanya kwa watoto wao, mf. kuwabaka, kuwalawiti, kuzaa nao, kuwachoma moto mikono, kuwaua, kuwafanya kitega uchumi kwa kuwauza kingono, kuwanyima chakula, kuwatelekeza n.k, sio wazazi wote ni wazuri, wengine ni wa hatari kwa maisha ya watoto wao.

Yaani mtu shukuru Wazazi wako wakiwa wema kwako, na waombee wale wanaotaabikabika kwa maovu wanayofanyiwa na wazazi wao.
 
Na wale wazazi wanaoroga watoto wao wasifanikiwe inakuwaje!? Tena akina Mama baadhi!
 
kwa habari ya Mungu nakushauri rudi darasani tena,kiipofu akijifanya anaona huku haoni ni balaa.
 
Heshima kwenu Maintelegencia wa Jf.
Katika huu Uzi kuna jambo moja kubwa linalojadiliwa na kukosa Jibu la moja kwa moja.
Kuna huu mjadala wa Mungu mkuu kiongozi wa ulimwengu watu wanajadili uwepo wake na ufalme wake.
In short Mzazi wako ndio Mungu wako wa Dunia hii yeye ndiye anaekupa baraka katika Maisha yako ya Duniani.
Mzazi wako ndiye anaekuonesha njia za kupita ili uishi kwa Amani na mafanikio ktk Dunia hii.
Huwezi kufanikiwa jambo ambalo mzazi wako hajaridhika nalo mafanikio ya mtu yanatokana na Mzazi wake.
Mzazi wako ndiye anaekuonyesha ni nani Mungu wako wa Ulimwengu wote kwa ujumla anataka nini na hapendi nini.
Mzazi wako anakuonyesha ni jinsi gani ya kumuabudu Mungu mkuu wa ulimwengu.
Fanya kile ambacho mzazi wako anataka ufanye acha kile ambacho mzazi wako hataki ufanye hapo ndipo utauona Ufalme wa Mungu hapo ndipo utakapofanikiwa Maisha yako kabla ya kifo na baada ya kifo.
Kama mafundisho ya mzazi wako yamepotosha basi yeye ndie wa kulaumiwa.
Katika ulimwengu wa sasa hakuna alieshushwa kila mmoja ametokana na Wazazi wake.
Nihitimishe huu mjadala wa Mungu hauwezi kuisha kwa kujadili maandiko ya Vitabu ambavyo hujui mwanzo wake.
Ili uishi vizuri duniani fuata yale ambayo Mzazi wako anakuelekeza.

Hii nadharia yako haina ukweli, kuna wazazi wengine wanawakosea sana watoto wao kwaiyo cha muhimu ni kujitambua na kufuata njia sahihi, na kuhusu Mungu fuata imani yako.
 
Back
Top Bottom