Wakuu JF Amani iwe Nanyi.
Tunapozungumzia katiba Mpya katika kipindi hiki ambacho Serikali 3 haziepukiki.
Binafsi nimekuwa nukijiuliza sana ni kwanini Mzee Aboud Jumbe Yuko Kimya sana.
Hii ni Seheme ya Wasifu wa Mzee Aboud Jumbe Kutoka Wikipedia
Inasemekana kuwa hata wazo la kuunga TANU na ASP Lilikuwa ni la huyu Mzee.
Huyu Mzee inasemekana kuwa alisalitiwa na Maalim Seif pale alipokuja na wazo la Serikali 3.
Si Mpango wangu kujadili issue ya Maalim Seif, Lakini kwa wanaojua Siasa za Tanzania wanajua kuwa hata Maalim Seif Baada ya kupewa Mikoba ya Uwaziri Kiongozi, haikumchukua muda kuyaona na kuyashuhudia yale Mzee Jumbe alikuwa ameyaona, hii ilipelekea hata Maalim kuwekwa kizuizini na kuachiwa wakati almost nchi iko kwenye Mfumo wa vyama vingi na kujiunga na CUF kuendeleza Mapambano.
Sasa kwa kuwa Maalim anasimamia yale Mzee Jumbe aliyoyaona, hivi hatuoni kuwa ni wakati Muafaka sasa wa Mzee Jumbe kutoa Maoni yake.
Naandika post hii nikiwa na imani kuwa Mzee Jumbe yupo buheri wa Afya.
cc
Barubaru ,
zanzibar huru, Mzee
Mohamed Said ,
Bobwe