Mzee Akilimali anahurumia tumbo lake tu

Mzee Akilimali anahurumia tumbo lake tu

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Michezo ni furaha na furaha ni kushinda na kushinda ni mipango na sayansi ya michezo na mipango na sayansi ya michezo ni gharama kubwa ambayo mzee Akilimali hamudu hata kununulia wachezaji wa Yanga japo maji ya kunywa tu timu inapokuwa mazoezini licha ya kuwa kwenye mechi uwanjani. Zama za mpira wa ridhaa na kutegemea uchawi ili kupata ushindi zimekwisha. Timu ni Mashabiki na mashabiki wa Yanga wanataka ushindi ili wafurahi bila ya kujali timu inamilikiwa na nani

Mzee Akilimali nadhani hofu yake kuu ni kukosa kifungua kinywa kama timu ya Yanga ikiendeshwa bila kuhakikishiwa upatikanaji wa futali yake. Yuko tayari kutembeza bakuli kwa watu ili apate fedha za kununulia maji wachezaji na yeye kuambulia chochote.

Kote duniani club huwa zinauzwa ili kupata mafanikio ya kiuchumi, ushindi na furaha kwa wanachama na mashabiki wao, iweje Akilimali ang'ang'anie kuwaudhi mashabiki wanaotaka furaha kupitia Yanga?

Yanga ina mashabiki wengi sana, na sauti yao ni sauti ya Mungu, dua zao ni uchawi tosha.

Kama kuna tajiri bila kujali ni Manji au mwingine yule mwenye uwezo wa kutupatia furaha kupitia Yanga ni vema akapewa nafasi.
 
Si alishawaomba msamaha kwani bado yanaendelea?
 
Hii ishu ni mtifuano baina ya uchawi wa kiafrika na uchawi wa kizungu yaani
Pesa V/s Ndumba.
 
Michezo ni furaha na furahi ni kushinda na kushinda ni mipango na mipango ni gharama ambazo mzee Akilimali hamudu hata kununulia wachezaji wa Yanga japo maji ya kunywa tu timu inapokuwa mazoezini licha ya kwenye mechi uwanjani. Timu ni Mashabiki na mashabiki wa Yanga wanataka ushindi ili wafurahi bila ya kujali timu inamilikiwa na nani.

Mzee Akilimali nadhani hofu yake kuu ni kukosa kifungua kinywa kama timu ya Yanga ikiendeshwa bila kuhakikishiwa upatikanaji wa futali yake. Yuko tayari kutembeza bakuli kwa watu ili apate fedha za kununulia maji wachezaji na yeye kuambulia chochote.

Kote duniani club huwa zinauzwa ili kupata mafanikio ya kiuchumi, ushindi na furaha kwa wanachama na mashabiki wao, iweje Akilimali ang'ang'anie kuwaudhi mashabiki wanaotaka furaha kupitia Yanga?

Yanga ina mashabiki wengi sana, na sauti yao ni sauti ya Mungu, dua zao ni uchawi tosha.

Kama kuna tajiri bila kujali ni Manji au mwingine yule mwenye uwezo wa kutupatia furaha kupitia Yanga ni vema akapewa nafasi.

Mzee Akilimali anaweza kuwa ana makosa na pengine hata njaa anayodaiwa kuwa nayo...lakini kwa upande mwingine wale wanaomshutumu watafakari hoja zake kwanza...Je, mkutano ule ulioitishwa na kutoa maamuzi ya kukodisha timu ulikuwa sahihi kikatiba??? Je, kiongozi anaweza kuitisha mkutano na wakati huo huo awape wanachama wale muda mfupi wa kuamua kukodisha timu kwake??? je, hiyo ni sahihi kweli? Je, wanachama wale waliofanya maamuzi wanawakilisha wanachama wengine nchi nzima??? Ni kweli Mzee Akilimali anaweza kuwa ana njaa kama inavyodaiwa, lakini mzee yule ana akili sana, ana upeo mkubwa wa mambo licha ya kutoingia darasani...haya ni mawazo yangu tu, naweza nikawa siko sahihi...
 
Achaneni na huyo mzee, fanyeni mambo kisasa watani zangu.
 
Yaani kama Yanga wanataka wapoteane mpaka kushuka daraja msimu huu ,basi wamchezee huyu mzee,hawa wazee ndo wanaojua Yanga Fc imelalia wapi.
 
Huo ni urasimu ambao unapingwa kila kona duniani. Akilimali na wengine wangetumia muda wao kuhakikisha na kusimamia kuwa mkataba wa kuikodisha klabu yao unainufaisha yanga badala ya kuhoji akidi na uhalali wa mkutano. matajiri kote duniani hawapaswi kudenguliwa wanahudumiwa kwa fast track na wanaheshimiwa. Akilimali anafahamu kuwa mpira wa sasa ni gharama katika nyanja zote kuanzia usajili makocha usafiri mishahara viwanja nk. Muda ule wa udalali wa kutafuta matajiri wa kununulia klab mipira, jezi na maji umekwisha.
 
Kuwa makini, unaweza kushitakiwa kwa kutishia usalama wa mtu.
inatia hasira wengi, haiwezekani timu azaliwe miaka 80 iliyopita iwe haina uwanja wake wala kushinda kombe lolote kubwa. Timu iendelee kutegemea ukingaji wa bakuli na "kamati za ufundi" kujiendesha. Hii inasababisha kila mchezaji asajiliwe na mtu wake ambae ndiye atakayekuwa na mamlaka ya kumuamulu acheze au asicheze vizuri kwenye mechi muhimu. Mara nyingi watu hawa wanaosajiri wachezaji wao kwenye vilabu huwa wanarudisha fedha zao hizo kwa kuihujumu timu wakati wa mechi muhimu kwa kupitia wachezaji wao hao. Mchezaji anapokea maagizo kutoka kwa bosi wake aliyemleta hapo badala ya kusikiliza maagizo ya kocha na uongozi wa timu. Wazee waliendesha maisha yao kwa njia hizo kwa miaka mingi sana, inafahamika kwa kila mtu. Hata hivyo watu hawa wanapaswa kuelimishwa sio kuwaangamiza.
 
Mzee Akilimali anaweza kuwa ana makosa na pengine hata njaa anayodaiwa kuwa nayo...lakini kwa upande mwingine wale wanaomshutumu watafakari hoja zake kwanza...Je, mkutano ule ulioitishwa na kutoa maamuzi ya kukodisha timu ulikuwa sahihi kikatiba??? Je, kiongozi anaweza kuitisha mkutano na wakati huo huo awape wanachama wale muda mfupi wa kuamua kukodisha timu kwake??? je, hiyo ni sahihi kweli? Je, wanachama wale waliofanya maamuzi wanawakilisha wanachama wengine nchi nzima??? Ni kweli Mzee Akilimali anaweza kuwa ana njaa kama inavyodaiwa, lakini mzee yule ana akili sana, ana upeo mkubwa wa mambo licha ya kutoingia darasani...haya ni mawazo yangu tu, naweza nikawa siko sahihi...
Jee Mkutano wa simba ulioitishwa kujadili hoja ya MO kuuziwa 51% ilikuwa ni sahihi kikatiba?????????????????
 
Wewe unaonaje mwenzangu??? Mimi sijazungumzia mkutano wa Simba...hoja haikuwa kuhusu Simba bali ilikuwa kuhusu YANGA...Ila kwa kukujibu swali lako SIMBA na YANGA haziko tofauti kiubabaishaji...wanachama na wapenzi wa klabu hizi hawajielewi...Kazi yao kupiga kelele tu na wala hawazisaidii klabu zao...Katiba ya YANGA iko wazi kuwa Klabu itakuwa na kampuni, sasa mtu anaitisha mkutano wa dharura na kutaka kukodisha timu, wenyewe wanashangilia bila kujielewa, hakuna tofauti na kilichotokea miaka kabla ya ukoloni ambapo Carl peters yule mjerumani alikuja kuwahadaa machifu walioingia mikataba fake...anajitokeza mtu anapinga (hata kama ni kweli ana njaa kama inavyodaiwa) basi huyo mtu anaonekana msaliti na kushutumiwa kila kona...Mkutano umeitishwa ni fake na hata maamuzi ni fake lakini bado watu hawashituki...Huko Simba nako mtu anajitokeza kuwa anataka amiliki klabu kwa asilimia 51 watu wanashangilia...yaani hata katiba inazungumzia nini hawajui...Yaani mtu akionekana ni tajiri basi huyo anajua kila kitu, serikali nayo kimya...Yaani watu hawajui kuwa masuala yanayogusa mamilioni ya watu ni hatari kwa usalama wa taifa...
 
Hoja ni ile ile ila kwa simba inaonekana sawa na kwa yanga figisu figisu. Nielewavyo ni kwamba hoja ile ilizungumzwa kwenye mkutano mkuu maalum na kimsing ikaridhiwa na ukaachiwa uongozi uwasilishe hoja hiyo kwa wadhamini wa yanga nao waiangalie[ kwa kutumia wataalam] halafu matokea yake yawasilishwe tena kwa wanachama kwa maamuzi.
Kabla mchakato huo haujafika popote pale ndipo mzee Akilimali akaanza kuropoka.
Kwa maoni yangu ni kwamba process bado inaendelea na itakapokamilika wenyewe wataitana na kuamua.
 
Nadhani tumalize mjadala huu kwa sasa...ila kwa taarifa yako pembeni mwa kompyuta yangu nina katiba ya YANGA ya mwaka 2008 na ile ya mwisho ya mwaka 2010...
 
Wewe unaonaje mwenzangu??? Mimi sijazungumzia mkutano wa Simba...hoja haikuwa kuhusu Simba bali ilikuwa kuhusu YANGA...Ila kwa kukujibu swali lako SIMBA na YANGA haziko tofauti kiubabaishaji...wanachama na wapenzi wa klabu hizi hawajielewi...Kazi yao kupiga kelele tu na wala hawazisaidii klabu zao...Katiba ya YANGA iko wazi kuwa Klabu itakuwa na kampuni, sasa mtu anaitisha mkutano wa dharura na kutaka kukodisha timu, wenyewe wanashangilia bila kujielewa, hakuna tofauti na kilichotokea miaka kabla ya ukoloni ambapo Carl peters yule mjerumani alikuja kuwahadaa machifu walioingia mikataba fake...anajitokeza mtu anapinga (hata kama ni kweli ana njaa kama inavyodaiwa) basi huyo mtu anaonekana msaliti na kushutumiwa kila kona...Mkutano umeitishwa ni fake na hata maamuzi ni fake lakini bado watu hawashituki...Huko Simba nako mtu anajitokeza kuwa anataka amiliki klabu kwa asilimia 51 watu wanashangilia...yaani hata katiba inazungumzia nini hawajui...Yaani mtu akionekana ni tajiri basi huyo anajua kila kitu, serikali nayo kimya...Yaani watu hawajui kuwa masuala yanayogusa mamilioni ya watu ni hatari kwa usalama wa taifa...
Nadhani kwa hali na historia za YANGA na SIMBA zilivyo nguvu nyingi ingewekwa kwenye contents za mikataba ya ukodishaji na ununuzi wa hisa sio kwenye wazo/pendekezo la MO na Manji. Unavyosema wewe ni sawa na kujigamba kuwa Tanzania ina gesi nyingi kwenye maji ya kina kirefu baharini lakini hatuna uwezo wa kifedha na technologia ya kuichimba gesi hiyo. Gesi ipo lakini ni maskini. SIMBA na YANGA kwa aina hii ya AKINA Akilimali zimeshindwa kuwapa mashabiki wao furaha kwa zaidi ya miaka zaidi ya 80 nyuma, kuna ubaya gani kuona hiyo miaka 10 ya Manji au MO itafananaje? kama matimu makubwa na makongwe mithili ya Liverpool. ManU, Real Madrid yamekabidhiwa matajiri tena ambao sio wazawa kabisaaa, sembuse Manji na MO ambao wamezaliwa hapahapa! Huo ni woga wa kijinga tu lakini vilabu hivi vingekuja na ile sera ya "Hands off eyes on" tuwape hawa mabwana mikataba ambayo ina indicators ambazo zinaonyesha do,s and dont's na vitu (thresholds) ambavyo vinaweza kusababisha wenye vilabu wavunje mikataba hii na kuvirejesha mikononi mwao tena.
 
Nimekuelewa lakini nadhani hujawaelewa hao wanaozitaka Simba na Yanga....mmmoja anataka asilimia 51 ya timu na wala hajazungumzia suala la mkataba...anataka akubaliwe kwisha, na akatoa sh. 100 milioni sawa na wakoloni walivyotoa shanga na nguo kwa machifu na elites wengine wa Enzi hizo...mwingine anataka akodishiwe timu kwa miaka 10 na apewe logo na yeye atachukua faida asilimia 75 na asilimia 25 ndiyo klabu....yaani tayari ameshaweka masharti...Yeye ni kiongozi na anaitisha mkutano wa dharura na kutoa masharti kwa wanachama 'wachache' ili watoe maamuzi kwa muda mfupi...Yaani yeye ni kongozi na ana interest na anaongoza mkutano huku mabasi yakiwa nje ili kuwapeleka wanachama mpirani...Yaani tayari ameshaamua kuwa atapewa logo na asilimia 75 haya ndiyo masharti yake....Hii inatokea karne ya 21 na watu wanashangilia...wanachama hao hao kazi yao kupiga kelele hawawezi hata kulipa ada ya mwaka ya uanachama, wakati mwingine wanalipiwa..

Ni kweli ni aibu kwa klabu ya miaka 80 kuwa katika hali hiyo....but who is to blame????Ni akina nani walifanya registration ya logo?? Lengo lilikuwa zuri lakini je, lengo lilitimia? Kwanini watu wakiwemo wasomi wenye progressive minds hawadumu Yanga na Simba???? Katiba za klabu zimetengenezwa kwa kuzingatia maelekezo ya FIFA , kwamba kuwe na sekretariati zenye mamlaka za kiutendaji....Je, Simba na Yanga kuna sekretariati zenye mamlaka za kiutendaji hivi sasa???? Kama hakuna ni kwanini???? Yaani kinachotokea Simba na Yanga kiuongozi mtu huwezi kuelezea ni nini, ni mchanganyiko wa uongozi wa miaka ya 60 na 70 na uongozi wa kileo na maelekezo ya FIFA.... Yaani ni vurugu, sijui kuna kamati za wazee nazo zikiamua eti maamuzi yana nguvu, sijui kuna vijana eti nao wana nguvu kimaamuzi, sijui kuna matawi eti nayo yana nguvu kimaamuzi...kuna viongozi wa kuchaguliwa (na ambao nadhani wapo kufanya rubber stamping wa maamuzi fulani) na mtu akileta hoja anafukuzwa na the so called mkutano wa wanachama na ambao umeitishwa kinyume na katiba..kuna viongozi wa kuajiriwa, sijui wanaarijiwa vipi na kama matangazo yao ya kazi yanatolewa wapi...Sasa mtu huelewi ni nani wenye mamlaka ya uongozi au utendaji je, ni sekfretariati yaaani wale wa kuajiriwa au wale wa kuchaguliwa...wale wa kuajiriwa wanawajibika kwa nani je ni kwa Mwenyekiti, Kamati ya utendaji au wanachama....yaani mtu huelewi...serikali ipo... TFF nayo ipo na ambayo nayo ina madudu yake....hahahahahhaha, soka ya Tanzania......tehtehtehtehteh...Yaani wasemaji wa klabu wanakuwa ni wana-mipasho, na watu wanafurahi na kuchekelea mipasho.....Yaani wanakaa vijiweni na kupongezana je, umemuona na kumsikia fulani alivyowasema jana wana-mikia ????umemsikia fulani alivyowasema vyura????? Duh, kazi ipo kweli kweli.....
 
Back
Top Bottom