Mzee alivyotukosesha mamilioni ya Mjerumani

Hamumu

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2021
Posts
1,439
Reaction score
3,587
Hapooooo....

Nadhani tuko fresh bhandugu. Leo nimewiwa kuwapa stori hii ambayo hadi kesho sitokaa nisahau kisa hiki cha aina yake.

Kuna siku nilikuwa kwa mganga wa jadi katika harakat za kuiseti mipango iende kama ninavyotaka (kulingana na imani yangu), nilikutana na jamaa mmoja wa umri kati ya 30 hadi 35 ambaye nilibahatika kupiga nae stori mbili tatu tukiwa tunamsubir babu aamke atutatulie matatizo yetu. Katika stori ilifika point tukaanza kusimuliana kilichotupeleka pale. Binafsi nilimweleza yangu na yeye akanipa mastori yake.

Jamaa alikuwa katika harakati za kutafuta zile sarafu za zamaniiii almaarufu RUPIA, ambako aliahidiwa kupewa mpunga mrefu endapo atapata hio kitu. Basi bwana, stori zake zilinivutia sana an nikatamani niijue inafananiaje. Baada ya muda babu aliingia akatuita wote na kutupigia ramli. Mimi nilipewa dawa nilostahili kuipewa halafu nikatulia ili nione yule jamaa anateta nini na mganga.

Jamaa alimwomba yule babu amuuzie rupia au la amwoneshe ni nani anazo ili mwamba aendelee kujaribu bahati yake ya kwenda kuiuza kwa mjerumani.

Babu alimkazia huku akiingia ndani ya chumba chake kidogo chenye kiza na kutoka akiwa ameishika mkononi. Alitusimulia mambo kadhaa kuihusu ile rupia, ikiwa ni pamoja na kazi zake za kiganga na sometimes uchawi.
Tulibaki tukiduwaa kwa muda kisha akairudisha ndani. Tuliondoka na yule jamaa hadi mahali ambako kila mtu alishika njia yake. Ila nilimwomba namba yake kwa ajili ya kujaribu kutafuta taarifa zaidi za ni wapi hizo rupia huuzwa. Nilirudi nikaendelea na mishe zangu za kila siku huku tukiwasiliana kwa nadra sana.

Nilijaribu kuulizia kwa watu ni wapi nitapata rupia bila kujua hata nikiipata nitainunua bei gani na nitaipeleka wapi😄. Katika mastori mtaani nilisikia kuna bibi kizee mmoja mkoani manyara anazo rupia 3. Nilifanya research hadi nikafika kwake. Nilienda kama mtu ninaetafuta mashamba ya kukodisha kwa msimu. Alinipokea kisha tukapiga sayu za hapa na pale then nikaulizia mashamba. Kwa muda ule hapakuwa na hata hekari moja ilokuwa free. Tukaachana na mashamba nikaamua kumchana ukweli ili kama ataniroga na aniroge dadeq zake.... (hela hizi)....

Nilivyoulizia tu alinikazia macho halafu akaanza kutetemeka. Alihoji nimejuaje kama kwake zipo na ninahitaji kwa ajili gani. Nlijieleza kwa kina bila kujua hata naongea nini juu ya rupia. Aliniuliza ikiwa nina ufahamu juu ya rupia ya kweli na ile feki. Nilijibu kuwa naelewa kila kitu kisha akanitaka niondoke na nirudi baada ya siku 7. Sikuona uvivu, nikasepa ila nikamsihi sana anipatie hio rupia kwa gharama yoyote ile atakayoitaja. Hakujibu kitu zaidi ya kuniaga tu.

Bas nilivotoka pale nilimpigia yule jamaa nikamwambia kuna kama 50% hivi za kufanikiwa kuipata rupia. Alinisihi sana nimwambie nilipo lakini sikufanya hivo. Nilimwambia apange safari baada ya siku 7 tukutane mahali nimpeleke ilipo ile mali. Toka siku hio yule mwamba alikuwa akinijulia hali kila baada na nusu saa🤣, simu kibao, usiku mwema kwa sana, vocha za kutosha hadi nikapata hofu. Uzuri ni kwamba sikumwambia ninapoishi. Huenda angekuja anilinde kabisa. Sasa bwanaa siku 7 zikakata, nikamwelekeza tukutane hospitali ya hydom then tuchukue boda tuzame maporini alipo yule bi kizee. Tulifanikiwa kufika na tulimkuta akiwa nje akiandaa mboga za majani kwa ajili ya mlo. Alitukaribisha kwa kutupatia viti kisha akanitazama na kuuliza ikiwa nimefuata ule mzigo. Nilimjibu kwa ujasiri kuwa ni hicho tu.

Alitoka nje ya mji wake kwa dk kama 40 hivi huku akituacha mimi na yule jamaa pale nje. Baada ya muda alirejea akiwa na mzee mmoja hivi labda ni age mate wake, japo mzee alikuwa amechoka zaidi. Tulisalimiana kwa muda kisha wakaingia ndani wakateta kwa muda kisha wakatoka na kasha la kiberiti.

Yule bibi alikuja mbele yangu akakifungua kile kikasha akatoa ile rupia kisha akanipatia niikague. Jamaa anininong'oneza kwa kusema " ni yenyewe kaka". Niliitikia kwa kichwa kisha nikampatia tena bibi. Alikirudishia ndani ya kiberiti then akampatia mzee yule na kumwambia nenda nao wakupe hela nyingi. Mzee aliitikia kwa sauti yake ya kufifia sana.

Tulitoka nje ya ule mji kisha yule mzee akauliza kuwa kuna umbali gani hadi mahali hela zilipo. Nilimwachia yule jamaa jukumu la kujibu maswali yale. Alipiga simu kuwa mzigo upo hivyo waje wauchukue. Sikujua ni akina nani hao na sikujali hata. Kikubwa wanikatie changu nijikatae. Tuliondoka na yule mzee hadi Basoutu (mji flan hivi umechangamka kidogo) manyara. Baada ya maelekezo mengi hatimaye ilikuja gari flani kama yale yanayobebaga dawa. Wakafungua mlango wa nyuma tukaingia kwenye ile bodi ya nyuma.

Wote walokuwa mbele walikuja nyuma pia, tukawa kama vile tupo kwenye ka kikao kadogo. Sikuwaza coz mishe zote ni mchana na ni pale pale mjini kati. Yule mjerumani alimuuliza jamaa hawa ndo wenye mali? Jama akasema huyu mzee ndo ana mali ila huyu dogo ndo alonisukia mpango wa kuipata. Alinipa tano ya ngumi akasema safi kijana.

Waliongea na mzee kwa muda kisha akaomba aione. Mzee aliitoa kisha akampatia. Wakaipima kwa vitu vyao kisha wakampatia mzee na kumwomba awauzie. Mzee alisema nipatieni pesa nyingi sana bila kutaja kiasi. Aliulizwa apewe box ngapi? Alijibu nataka box 8 bila kujua kila box lina kiasi gani. Yule mjerumani alisema "Tumpe 2 BILLIONS" kisha akaamuru box 10 zishushwe.

Wazee, sikuwahi kuona ela nyingi kama nilizoziona ndani ya ile gari. Ni nyekundu tupu hadi nikahisi kufa kufa. Kwa akili yangu nikaanza kuona bonge la jumba la gorofa, gari kaliiii na mwanamke mrembo sana na vitoto vyangu viwili tukiwa ndan ya ile nyumba ya ndoto za mchana.

Huwezi amini yule mzee alizimia. Wakahangaika nae hadi akaamka. Alipoziona akaomba atoke nje kidogo. Aliruhusiwa huku washkaji wakimsapoti kushuka pale. Yule jamaa angu alinambia sisi tutapewa sio chini ya 200millions. Nikatokwa jasho na mimi.

HUWEZI AMINI YULE MZEE ALISEPA AKIGOMA KURUDI KWENYE GARI.

wasaidizi wa mjerumani walirudi garini na kuichukua ile rupia na kumpelekea kisha wakasema mzee amedata. Kakataa kabisa kuitoa mali. Hawakujali wakafunga box zao wakazipanga kisha tukatoka nje ya gari. Yule mjerumani alimpa yule jamaa angu laki 6 na kumwomba aendelee kutafta rupia nyingine. Jamaa alinipa laki 4 kisha na yy akaniachia maagizo yaleyale kuwa tutafute mali nyingine ya mtu jasiri.

Nilichukua boda hadi kituo cha mabasi ya mikoani nikarudi zangu chuga. Ila siku sikulala mazee. Nilimtukana yule mzee kimoyomoyo. Hadi leo simpendi japo sijajua ikiwa yupo au alikufa na wenge la hela.

Sikuhangaika tena kutafuta rupia nyingine japo simu ni ka.a zote kutoka kwa yule mwana.

YULE MZEE AMENIFELISHA SANA MCHONGO WASHKAJ ZANGU
 
Hii toli unatubongea umeiboresha chalii, hii iliwahi tumika siku za nyuma kwa utapeli, sijajua Leo lengo ni kubonga tuu au ndio unatukamatia mafront ili tujikute kwa Target
 
Ni sheria ako chali angu, na haipingwi an
 
Back
Top Bottom