Mbunge wa Hai Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saasisha Mafuwe ameendelea na ziara yake ya Kata kwa Kata katika wilaya hiyo kwa lengo lakuwaeleza wananchi yaleyaliyofanyika kwakipindi cha miaka minne tangu ateuliwe kuwa Mbunge wa Hai.
Pia kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Kata hizo akishirikiana na wataalamu wa Halmashauri.
Hii ilikuwa ni zamu ya Kata ya Weruweru ambapo Mbunge Mafuwe alifika nakuwaeleza wananchi hao jinsi Serikali ilivyoleta maendeleo katika Kata hiyo ambapo wananchi hao waliridhika nakisha kumuombea Dua ya Afya njema Mbunge wao.