Mzee Azim Dewji: Arajiga akichezesha najua Simba wataonewa

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mdau mkubwa wa michezo nchini na Mwanachama wa Klabu ya Simba, Mzee Azim Dewji amefunguka kuhusu waamuzi ambao watachezesha Dabi ya Kariakoo.

Wakati huo huo, kamati ya Waamuzi nchini inemtangaza Ahmed Arajiga kuwa ndio mwamuzi wa mchezo wa tarahe 8 pale Dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Your browser is not able to display this video.


 
Mzee aambiwe ukweli simba wakazane waongeze wachezaji kama watano ndipo watashindana na Yanga.

Shida ni Kijana wake ambaye ni mjomba Bahili sana kutoa hela, Hajawahi kununua wachezaji yeye ni kusubiri Maghalasa ya Free Agent.

Atasingizia Refa huku timu haina no 10
Yanga wana
Pakome
Aziziz
Chama
Max
(Mudadhiri (nabi)
je simba ana nani?????
 
Dewji umeongea uongo Kwa kiwango kikubwa. Hiyo Mechi anayoisema mpaka halftime Simba ilishafungwa 4-0 na hakukuwa na goli la kuonewa hata moja. Mgogoro wa malipo kwa Wachezaji ndo uliosababisha Wachezaji kucheza chini ya kiwango. Marehemu Mansour Magram angekuwepo angekuumbua maana alikuwa hataki unafiki.
 
Hao wote uliowataja hapo haluna namba 10 wa kumzidi Ahoua

Number zinaongea

MVP wa Ivory Coast msimu uliopita, usidhani kua yupo hapo kwa bahati mbaya ni Uwezo wake ndo ulimweka hapo
 
Wewe nenda kwenu indian hapa siyo kwenu simba siyo ya mamaako nenda kwenu huko indian we nani nchi hii
 
Lakini hii video ni ya zamani mkuu sio ya mwaka 2025.

Inasemekana imeokotwa maktaba.
Ilikuwa ya misimu kadhaa iliyopita.

Thanks.
 
Huyo mzee Alisababisha Tusibebe Ubingwa wa Caf 1993.
kama Vp Akachezeshe yeye.
 
Hao wote uliowataja hapo haluna namba 10 wa kumzidi Ahoua

Number zinaongea

MVP wa Ivory Coast msimu uliopita, usidhani kua yupo hapo kwa bahati mbaya ni Uwezo wake ndo ulimweka hapo

Duh mahaba kitu kibaya sana, ndio maana watu wanajiua kisa mahaba. Pole sana
 
Siyo Kweli...binafsi nilikuwepo uwanjani siku ile...hakuna goli lilifungwa siku ile...halftime ilikuwa 0-0 kipindi cha pili Simba hakurudi uwanjani...kipindi cha kwanza mpira ulikuwa unachezwa eneo la Simba Mara Kwa Mara...Simba walikuwa wanafanya faulo za kijinga na za wazi ili wapewe red lakini kadi haikutoka...mpango ulikuwa kwamba wakipewa red watoke uwanjani Kwa kisingizio cha kuonewa..inasemekana Hafidhi aliwaambia wachezaji uwanjani kwamba hatatoa red Ila kufungwa watafungwa...kipindi cha pili hawakurudi...nakumbuka kapteni WA Simba siku ile alikuwa Method Mogella ambaye baadaye alijiunga na Yanga..
 
Ngoja tuwaulize tabora utd
 
Huyu hajaleta taharuki na uchochezi au Kwa vile ni mahindi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…