Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
“Sasa hivi naamini kwamba CCM... hawaamini kabisa kwamba wao ni chama na wako katika nafasi hiyo ya kuwa na serikali na kwa sababu ya sera zao ambao wameanza kuziacha.”
Ngoja nijizuie maana nitafungiwa @$&";?/('@&(/_'*"::!?&+#@%©£¥^π×§∆π√|~~£¥={}\\{Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa Taasisi ya Mwalimu Julius Nyerere, Mzee Joseph Waryoba Butiku, amesema anaamini kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeanza kupoteza uelewa wa nafasi yake kama chama kinachoongoza serikali, huku akidai kuwa baadhi ya sera zake zimeanza kuachwa.
Akizungumza kwenye YouTube Channel ya M&S Podcast, Mzee Butiku amesema:
Mkishafika hapo mmeacha kuwa chama cha siasa kuwa chama dola madola huwa haitoki iko wakati wote chama kinaweza kutoka kinaweza hata kikafutwa au kukaparaganyika lakini CCM wamefika mahali hawaamini kwamba Watanzania wanaweza kuwaacha wakachagua watu wengine".
Soma Pia: Mzee Butiku: Rais ameshachaguliwa, hatukubali wanaosema aondoke; sio rais wa CCM, ni wa Tanzania
Ahsante sana, nimeiangalia interview. Mzee Butiku amejitahidi kutembea katika ''Chaki''..Ni kweli Mzee Butiku amewahi kuwa dissapoint watu hapo kabla.
..Lakini ktk interview hii kwa kweli amejitahidi.
..sidhani kama ktk wazee wastaafu kuna aliyewahi kufunguka kama Mzee Butiku ktk interview hii.
..kama kuna aliyefunguka zaidi yake naomba mnielekeze nikamsikilize.
..Mzee Butiku amezungumza ukweli wa mambo mengi sana, na kwa kweli ana mengi kifuani.
..Tutamlaumu Mzee wa watu lakini amejitahidi kwa kadiri ya kiwango chake.
..Kumbe Mzee Butiku alijaribu kuwasuluhisha Magufuli na wapinzani / Chadema lakini Magufuli alikataa.
..Mzee Butiku amelaani vitendo vya mauaji, na amevihoji vyombo vya dola vitoe majibu.
..Mzee Butiku ktk interview amelaani ufisadi na tamaa ya mali waliyonayo watawala wetu.
..Wizi wa kura pia ameugusia na Mzee hakumung'unya maneno kwamba Ccm wanaiba kura.
..Kuna suala la vibali vya uagizaji wa sukari kumbe linahusiana na Ccm kutafuta fedha kwa ajili ya kampeni.
..Kwa kweli ni interview ambayo inastahili kusikilizwa.
Cc Nguruvi3, MALCOM LUMUMBA
Yes Butiku amefunguka vizuri . BBC wakati ule walieleza na jambo la kushangaza hakuna aliyekataa serikalini..Mzee Butiku pia ameeleza hisia zake kuhusu watoto wa maraisi wa Uganda, na Tanzania, yaani Muhoozi, na Abduli.
..pia kuna tukio la kihistoria kuhusu ugomvi kati ya Mwalimu Nyerere, na Prof.Yussuf Lule, Rais wa mpito wa Uganda.
..Ugomvi huo uliishia na Mwalimu kuamuru Yussuf Lule awekwe kizuizini Ikulu Dsm na kupelekea mabadilko ambapo Godfrey Binaisi aliteuliwa kuwa Rais wa mpito wa Uganda.
Cc Nguruvi3