Hapa hua tunakutana kwenye tangawizi na kahawa
Mzee juma kafika na kanzu yake swafi na baraghashia yake kama kawaida, Mzee juma siku hizi ana simu ya kupangusa vidole hivo anakua busy kwenye simu , sio kama zamani alipokua anatumia kitochi,
Hussein anamuuliza kiutani mzee J naona unaperuzi mtandaoni, Mzee Juma akastuka ikabidi awe makini na kundi letu pembeni,
Hapa Pana lopolopo mmoja anaitwa Dulla ndio kayazua kumbe Dulla anajua story nzima ya mzee juma kupigwa kama elfu 50 za vocha huko Facebook,
Dulla anasanua michongo yote anaanza hivi mzee Dulla wale watu wako wanaokuomba vocha za Tigo tena utume Tigopesa ili mkachat WhatsApp maana kule hawana bando bado unaendelea nao?
Watu tunastuka akilini tunajua mzee hapo hua anapigwa, Kaeleza kua alipata marafiki huko mabinti wadogowadogo akaambiwa atume vocha wakachat huko mwingine,
Wakihamia huko anaambiwa atume elfu kumi waongee video call, naye anatumia, Hapa naona kuanzia kesho mzee Juma hatokuja kijiweni hadi hali ipoe kidogo maana kila mmoja anamcheka.
Kupitia kisa cha mzee juma nimekumbuka baadhi ya mbinu za utapeli , mfano umpeleke hela zako zote zikalale kwa mganga na kesho unakuta hayupo na pesa kaondoka nayo. Kupigiwa simu za kuhusu tenda za ujenzi, uchimbaji wa visima, madawa ya kilimo na mifugo wote huo utapeli.