Lole Gwakisa
JF-Expert Member
- Nov 5, 2008
- 4,768
- 2,361
Mzee Kavana, aliyekuwa Captain Kavana mwaka 1964 na aliyechagulia na askari wa Tanganyika Rifles walioasi ili awe kiongozi wao badala ya wazungu, amefariki jana 9/8/2024.
Captain Kavana wakati huo alikuwa hana hili wala lile huku askari waasi wakishinikiza kuwa kwa vile tumepata uhuru, lazima tuongozwe na muafrika, wakati huo kuna wimbi la Africanisation ya sehemu zote za ungozi nchini.
Hili lilimletea matatizo mzee Kavana maana hakuhusika na maasi wala kuwepo kuyapanga , lakini askari wa chini ndiyo walipenda waongozwe na askari Ofisa mzalendo badala ya wazungu.
Mzee Kavana ameishi kwa utulivu na amani nyumbani kwake Chang'ombe miaka yote.
RIP Mzee Kavana
NB
Picha kwa msaada wa wachagiaji.
Na kunaradhi, cheo wakati wa maasai kwa mzee Kavana alikuwa Luteni.