Mzee kifimbo, charaza mboko hawa...!

Mzee kifimbo, charaza mboko hawa...!

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Posts
16,199
Reaction score
8,761
Jana (20/09/09) nikiwa naangalia kipindi cha Maisha Plus, MASOUD KIPANYA na Wenzake wakiwa Mkoani Mbeya, walikuwa wakiandika maneno kwenye makaratasi na kuwaonyesha wale vijana wanaoingia kwenye usaili ili wasome maneno hayo kwa usahihi.

Lakini kilichonisikitisha ni pale walipoweka neno PHNEUMONIA, ambalo halipo kabisa katika lugha ya Kidaktari au kwenye dictionary!
Nadhani hawa ndugu walimaanisha PNEUMONIA. Matokeo yake , wakawafanya wale vijana washindwe kulisoma neno hilo, na hatimaye waone usaili ni mgumu kuliko ilivyotegemewa!

Wale vijana wanaonekana kuwa na Matumaini ya juu sana na ule usaili, na wanaweka hadi senti yao ya mwisho, wakitumaini kusonga Mbele! Lakini, kwa makosa kama hayo ya akina Masoud, wanakuta ndoto zao zinagonga mwamba. Mnasemaje waungwana?

MUNGU SAIDIA VIJANA HAWA!..........WOTE SEMENI `AMINA`.
 
aleluya. Tunagawana umaskini tu. Kipofu kuongoza kipofu mwenzake.
 
Ni hilo tu kuhusu unaloliita neno la kidaktari au kuna jingine? Mimi nilitembelea website ya Ikulu ya Uganda nikakuta eti wameandika kwamba aliyekuwa rais wa kwanza Tz, JK Nyerere alifariki mwaka 2000. Siamini kama wao ni mbumbumbu kiasi hicho ila ni typing error ambayo hata wewe mtoa mada PakaJimy unaweza kufanya!
 
Back
Top Bottom