Mzee Kikwete: SGR iliasisiwa na Hayati Mkapa na Mimi wakati namkabidhi Madaraka hayati Magufuli nilimsihi aanze Utekelezaji wa mradi!

Kwani 2025 anagombea?
 
Kwani 2025 anagombea?
 
TRA ilianza 01 July 1996

Kabla ya Hapo haikuwa na Commissioner General ila walikuwepo makamishna 3 Income tax, Sales tax na Customs ambao waliwajibika direct Kwa Waziri wa Fedha

..iko hivi.

..Bunge lilipitisha Sheria ya kuanzisha TRA mwaka 1995.

..Raisi Mwinyi akamteua Melkizedeck Sanare kuwa Kamishna wa kwanza wa TRA.

..baada ya hapo kukawa na kipindi cha mpito ambapo mambo kadhaa yalifanyika kama vile kuajiri watumishi wa TRA.

..ilipofika July 01, 1996, wakati Mkapa yuko madarakani, ndipo tulipoachana na idara za Income Tax, Sales Tax, na Customs, na TRA ikaanza kazi rasmi.
 
Haha wazo la mkapa halafu yeye akaangalia Tu miaka 10 akamaliza bila kufanya chochote [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] mzee anazeeka vibaya sana
 
Sasa kama Marais wawili walikuwa na plan kichwani lakini uwezo au uthubutu wa kutekeleza hawakuwa nao kuna haja gani kuwataja? Rais Mwinyi alikiri mbele ya kadamnasi kwamba Magufuli ametushinda wote. Mfano mzuri ni kuhamia Dodoma au daraja la Salender. Tumwache JPM apumzike kwa amani alituonyesha kwamba yeye ni mtendaji sio bla bla mara coco beach mara Lugumi maskando kibao
 
Haha wazo la mkapa halafu yeye akaangalia Tu miaka 10 akamaliza bila kufanya chochote [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] mzee anazeeka vibaya sana

..inawezekana ni kweli.

..Mkapa alipoingia tulikuwa na madeni makubwa ambayo ilibidi ayalipe kwanza kabla wakopeshaji hawajarudisha imani kwa Tanzania.

..Hii mikopo ambayo serikali inakopa huku na kule imewezekana kutokana na kazi kubwa iliyofanyika wakati wa Mkapa kuweka nidhamu ktk matumizi ya serikali, kukusanya mapato, na kulipa madeni ya nje.

..Wakati wa Mkapa kulikuwa hakuna uwezekano wa serikali kupata mikopo mikubwa kutekeleza miradi kama SGR, au Stieglers hep. Uwezekano kwamba miradi kama hiyo iliachwa kwenye makabrasha ni mkubwa.
 
..sasa mbona mawaziri wake waliomsaidia ktk wizara ya fedha, kwa maana, Daniel Yona, na Basil Mramba, wakaishia kwenye kushtakiwa kwa ufisadi?
Haya mambo ya kesi za ufisadi wa mawaziri, tena wa fedha achana nayo.
Unakumbuka kesi ya Prof C. Mahalu!!!!???
Ndugu JokaKuu unakumbuka I. Msabaha na "bangusilo"!!??
 
Hujamuelewa ndugu JokaKuu .
Ni kweli JK alikuta nchi ipo "stable" hazina,lakini kwa mujibu wa ndugu JokaKuu (ambapo ndio uhalisia),hiyo stability ilifanywa na Mkapa.
uongo, kikwete alikuta au alirithi a very healthy and stable economy, alikuta foreign reserve kubwa, export ziliongezeka hasa mining dhahabu to be specific, hazina aliikuta ikiogelea kwenye fedha …
 
Ufisadi upi na upi ambao ni "mkubwa sana" kwenye awamu ya Mkapa ukamsumbua Kikwete!!??
Ufisadi ulikuwepo,Ila kumsimbua kikwete,Hilo sielewi kivipi,lakini mkapa alijimilikisha kiwira, kikwete akampora na kuirudisha ' serikalini ',mrabaha wa 3% kikwete kahangaika kidiplomasia mpaka kuweka sheria ya 16%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…