Mzee Kinana
Salaam, shalom!!
Ndani ya chama Cha MAPINDUZI CCM, umewafundisha siasa vijana wengi sana, inawezekana wamefaulu machache kati ya mengi uliyowafundisha,
Somo linalohusu uwajibikaji wa pamoja umelifundisha sana tena Kwa vitendo, imekuwa mjenga HOJA mzuri, umejiuzulu mara kadhaa pale ulipoona mapungufu ndani ya chama Ili kuonyesha uwajibikaji wa pamoja.
Vijana ndani ya CCM, Nape, Makamba, Bashe ,Mwigulu, Kigwangala, nk nk somo hili wamegoma kulielewa na hawataki kulisikia!!
Swali: Ulikosea wapi katika mafunzo Yako Mzee Kinana, maana unaondoka bila kurithisha ubora wako Kwa vijana waliopo Hasa katika somo la uwajibikaji, nini kifanyike?
Karibuni 🙏
PIA SOMA
Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti (CCM) Ajiuzulu, Rais Samia Suluhu Aridhia