Mzee Kissinger wa Mtaa wa Congo: Chuo kikuu cha historia

Mzee Kissinger wa Mtaa wa Congo: Chuo kikuu cha historia

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Mzee Kissinger huniambia, ''Wewe Mohamed mimi nimekusomesha wapi?''

Mimi huwa simjibu kitu nashukuru na kama nimefuata kujua kitu kutoka kwake nitamuuliza na palepale mwalimu wangu ataniangusha ''lecture'' ya maana.

Vijana wengi wamekuwa wakija kwangu wakitaka kufahamu historia ya kweli ya wale waliounda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Tatizo wanasema kuwa historia ambayo wamesomeshwa shule imeachana kwa mbali sana na historia ambayo wameikuta kwenye kitabu cha Abdul Sykes na katika maandishi na mazungumzo wanayosikia kutoka kwangu.

Mimi siku zote ushauri wangu huwaambia waende wakazungumze na Mzee Kissinger yeye ni mjuzi wa historia hii kunishinda kwani mimi nimesoma mengi kutoka kwake.

Mwandishi chipukizi Hafidhi Kido kaenda kukutana na Mzee Kissinger na amesema kajifunza mengi sana kutoka kwake.

Angalia picha mwanafunzi alivyokunja goti mbele ya mwalimu wake anasomeshwa tarikh kwa rejea na nakala zenye ithibati.

Katika ujuzi wa Mzee Kissinger ni kule kujua hadi haiba na maisha ya wale anaowazungumza.

Iko siku alikuwa ananisahihisha makosa katika maandishi yangu akaniambia, "Sikiliza Mwalimu Nyerere asingeweza kumpa yule wizara ile kwani hakuwa mtu makini alikuwa mpuuzi kidogo. Ile wizara alipewa fulani."

Kufika hapa akanyamaza uso kaukunja kama ishara ya kukasirika akikumbuka vitendo vya yule mtu. Kisha akaendelea kunisomesha.


 
Back
Top Bottom