Mzee kutoka Damu wakati wa Haja ndogo - Msaada tafadhali

Utingo

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
10,266
Reaction score
8,085
Heshima wakuu; Nina mzee jirani yangu mwenye umri karibu miaka 70 sasa. Amepata tatizo la kutoka damu wakati wa haja ndogo hasa anapomaliza. Vipimo vya mkojo na hata kichocho vimeonyesha negative (hakuna tatizo) na hana home wala malaria wala ugonjw amwingine wowote na hasikii maumivu yoyote.

Naomba msaada nini kinaweza kuwa tatizo na hatua zipi achukue kwa sasa.

cc MziziMkavu
 
Last edited by a moderator:
Aende pia kupima Ini na figo huenda ana matatizo kwenye hizo sehemu mbili moja wapo. Muulize aliwahi kuuguwa ugonjwa wa kichocho zamani? Au aliwahi kuogelea katika madimbwi na ziwa n.k.

Tatu, inawezekana madhara ya kemikali za viwandani hasa iwapo aliwahi fanya kazi kiwandani, au kuishi kutumia maji ambayo yanaweza kuwa yamechanganyikana na kemikali za viwandani!

Kuna vitu vingi vinavyoweza kusababisha matone/damu kutoka katika uume. Lakini kwa maelezo yako, inaonyesha/inaonekana

tatizo ni la muda mrefu! Ningemshauri aende Hospitali kuu ya muhimbili kule kuna wataalam wanaweza kujuwa ni kitu gani kinachosabishwa huyo mzee kutokwa na damu wakati anapokojowa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…