Mzee Lowassa alisafishwa lini na Zitto alisamehewa lini?

Amani Msumari

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2016
Posts
1,830
Reaction score
972
Amani kwenu,

Leo sina mambo mengi sana, nina mambo mawili.
Kwanza ni ombi

Pili ni hoja ya leo ambayo kimsingi ni msisitizo wa maswali yangu yaliyokosa majibu kwenye uzi wangu wenye kichwa cha habari "wapinzani Msitufokee Watanzania Sio Wasahaulifu Kiasi Hicho".

Ombi langu ni kuwa wachangiaji wajikite kwenye hoja angalau kwa 50%

Kuhusu Jana, niliuliza kuhusu mzee Lowassa kuitwa fisadi na kufurushwa kwa Zitto kwenye Chama Cha Demokrasia na Maendeleo.
Kwakuwa CHADEMA na viongozi wake waandamizi akiwemo mgombea wao mh.Tundu Lissu walizunguka Tanzania nzima wakituaminisha kuwa Lowassa ni fisadi tena fisadi papa. Hatahivyo, ghafla wakampokea na kumfanya mgombea wao na hapo ndipo kumuita mzee Lowassa kuwa ni fisadi kukakoma.

SWALI
Je, hawaoni kuwa sasa ni wakati muafaka wa CHADEMA kumsafisha Mzee Lowassa?
Je, kumuita mtu fisadi na baadae kumfanya mgombea bila kutoa maelezo yoyote haiwezi kutafsirika kuwa ni kukosa msimamo na ghiliba kwa wananchi?

Viongozi wa CHADEMA kukaa kimya akiwemo mgombea wao mh. Lissu hakuoneshi kuwa viongozi hao hawana msimamo thabiti kwa kauli zao na mapambano dhidi ya rushwa?

Tuambieni, Mzee Lowassa mlimsafisha lini?

Viongozi wa CDM wakiongozwa na mwanasheria wao wa wakati huo, wakili msomi Lissu walimfukuza chamani ndugu Zitto Kabwe kwa madai mengi ikiwemo usaliti na kupokea hongo. Hatukuwaona viongozi hao wakitoka hadharani kumsafisha Zitto au Zitto mwenyewe kuomba radhi kwa makosa hayo aliyotuhumiwa nayo. Sasa tumesikia wanataka kushirikiana.

Je, kushirikiana kwenye mambo mazito ya nchi Huku vyama vikiwa na itikadi tofauti na viongozi waliotuhumiana sio kuwa ni uchu wa madaraka?

Ukisema fulani ni msaliti halafu mkashirikiana naye, nyie wote hamuwi wasaliti?

Ndugu zangu, tuwapime viongozi Hawa kwa kauli na matendo yao. Hawa hawatufai

2020 kura yangu kwa John
 
Zito anapaswa kuunga mkono juhudi za CDM mwaka huu akifanya hivyo atakuwa ametumia hekima yake vizuri na nchi itapata mabadiliko tunayoyataka.
 
Back
Top Bottom