Mzee Magoma na wenzake wale wamechanganyikiwa

Mzee Magoma na wenzake wale wamechanganyikiwa

Sasa yeye kati anapeleka kesi kwenye mahakama za kawaida alikua anafikiria nin?
Hakutambua kama FIFA wapo?
 
Magoma hawezi kulipia wakili bali kapewa wakili na wale jamaa zake kwa gharama zao. Aliyepeleka Yanga mahakamani ni Magoma, viongozi wa Yanga wanajibu mashitaka yake tu mahakamani. Kwahiyo akina Magoma walitaka Yanga wasiende mahakamani kujibu hoja zao?

View: https://www.instagram.com/reel/C_tJofrqtqe/?igsh=bnFwbG16ajFmdWc1

Hakuna kukaa mezani na mjinga kama Magoma. Aende FIFA kupitia Simba na TFF, maana huwezi kwenda Moja kwa Moja bila kupitia Simba na TFF Kwanza
 
Hakuna kukaa mezani na mjinga kama Magoma. Aende FIFA kupitia Simba na TFF, maana huwezi kwenda Moja kwa Moja bila kupitia Simba na TFF Kwanza
Kama angetaka kabla ya kwenda mahakamani angeishitaki Yanga TFF na BMT kwanza.
 
...anatumika vibaya!simba a.k.a kolo hawezi kufanikiwa kama yanga hawatakuwa na migogoro!hivyo kolo wanamtumia bwana Magoma kujaribu kui-distablize yanga!
 
Mzee akumbushwe, huu ni mwaka 2024 mawazo ya '68 hayawezi fanya kazi!

Inawezekanaje wanachama wote washiriki mkutano mkuu wa mwaka?

Mbona hadai wote twende bungeni badala yake tunawakilishwa na mtu mmoja Kila Jimbo?
 
...anatumika vibaya!simba a.k.a kolo hawezi kufanikiwa kama yanga hawatakuwa na migogoro!hivyo kolo wanamtumia bwana Magoma kujaribu kui-distablize yanga!
Yule wakili wa Magoma amesema kabisa yeye ni mwanachama na mshabiki wa Simba. Hivi huyu mwanasheria anashindwa kuwashauri wateja wake kuwa kesi hii watashindwa? Au jamaa wametenga fungu kubwa sana la kesi hii? Hakuna kukaa mezani na wahuni.

Magoma anataka wanaYanga wooote wahudhurie mkutano mkuu wa Yanga. Hivi wana CCM wote kama wangedai kila mwanachama ahudhurie mkutano wao Mkuu pangekalika? Ni mwanasheria gaaaani msomi ambae hawezi kumshauri mteja wake kwenye mashauri dhaifu kama hayo? Magoma na wakili wake wanashindwa kujua kuwa Eng. Hersi hatakuwa rais wa Yanga milele, kama Mzee Magoma anao ubavu wa kuwa Urais wa timu aanze sasa maandalizi ya kugombea urais baada ya muda wa Eng. Hersi na wenzake kumalizika. Alipe gharama za kesi hasaka..
 
Mzee akumbushwe, huu ni mwaka 2024 mawazo ya '68 hayawezi fanya kazi!

Inawezekanaje wanachama wote washiriki mkutano mkuu wa mwaka?

Mbona hadai wote twende bungeni badala yake tunawakilishwa na mtu mmoja Kila Jimbo?
Aende akagombee ujumbe kwenye tawi lake ili apate sifa ya kwenda kwenye mkutano mkuu, simpo!! Hata CCM wanafanya hivyo, hawaendi wote kwenye Mkutano mkuu.
 
Kwani Simba Sports hapa Inaingiaje...?

Nyie Pambaneni na Mzee Wenu..Hoja kwa Hoja. Mbona Mzee anaeleweka tu.

Hivi hapo Yanga hakuna Mtu anayeweza Kujenga Hoja mfike Muafaka na huyo Mzee kweli?

Basi,Muiteni JK au Sande Wayamalize na huyo Mzee.
 
Muafaka ni mzee akae "mezani" na Hersi wamkamue ng'ombe pamoja. Na mimi nakwambieni kama Mzee Magoma angeshinda kesi na wazee wa Simba wangetoka mafichoni kwenda mahakamani pia kudai ng'ombe wao wa maziwa anaekamuliwa na mo. Wazee kama Magoma wako wengi mitaa ya Kariakoo.
 
...anatumika vibaya!simba a.k.a kolo hawezi kufanikiwa kama yanga hawatakuwa na migogoro!hivyo kolo wanamtumia bwana Magoma kujaribu kui-distablize yanga!
Simba wasifikiri akina magoma wako Yanga tu, hata Simba wamejaa wanamsikilizia Magoma wa Yanga kwanza, wanapata tuition.
 
Back
Top Bottom