Mzee Majuto mgonjwa, akosa kitanda Muhimbili

nikiangalia issue ya wastara plus hii ya mzee baba king majuto naona bongo movie kuna tatizo, haiwezekani mtu awe kwenye game na aigize zaidi ya muvi 20 na bado akawa masikini! Mwakifamba kuna vitu haviko sawa anawafanyia wenzie
 
Hilo unalosema ni kweli chief, hicho kidogo wanacholipwa wanasahau kabisa kwamba kuna kesho.........
Yaani imeshakuwa kero hawa watu wanaojiita celebrity, kila mara kulalamika kuwa wametelekezwa na jamii wakati kwenye show zao tunaingia kwa pesa, pia kazi zao tunanunua
 
Bongo movie hawana mfuko wa dharura mwakifamba mbona anaponda sana raha na vimwana vp hawa jamaa wajitathmini
 
sasa na yeye si aende tu private...kwani lazima wote tubanane huku kajamba nani?yaan anakosa hela ya kwenda kutibiwa private??mzee katoa filamu kibao,kapiga sana matangazo azam,ivory nk au walikuwa hawamlipi??.dah bongo kwel hakuna ishu!!
 
Mkuu naona unakoelekea ni kutaka kusema nina ID mbili eee?huyo uliyemjibu sio aliyeleta bandiko la mzee majuto kukosa kitanda muhimbili. Acha pupa. Na sijaona sehemu kama kuna mchango umeombwa na majuto au nduguze kumuuguza.

Jiangalie kijana na kashfa zako za kiboya
 
mzee majuto nenda kwa wachungaji huwa wanaponya watu kila jumapili wahi
 
Magufuli alituambia Muhimbili kuna vitanda vingi kuliko wagonjwa, sasa inakuwaje mtu kama Majuto anakosa cha kulalia?
 
nikiangalia issue ya wastara plus hii ya mzee baba king majuto naona bongo movie kuna tatizo, haiwezekani mtu awe kwenye game na aigize zaidi ya muvi 20 na bado akawa masikini! Mwakifamba kuna vitu haviko sawa anawafanyia wenzie
Jamani tatizo lake ni pesa au kitanda?
 
Sasa ulitaka aseme kuwa apata kitanda wakati hajapata?
 
mbona sijaona mahali mzee wa watu kaomba msaada wa mtu?
 
Majuto mwenyewe kasema alikuwa anataka akalazwe VIP ward , lkn ikatokea kutokuelewa baina ya mlinzi na mkewe so ndio wakaambiwa na huyo mlinzi wanachokitaka hakipo. Kwa busara Majuto akaamua kurudi nyumbani. So ishu haipo kama wewe unavyodanganya kuwa ni pesa. Soma vizuri sio kila kitu kulaumu bila hata kufuatilia. Ndio maana unaambiwa kitu cha kuambiwa ongeza na akili zako. Mimi naona hukutaka kutumia uwezo wa akili yako kufikiri na kutafuta ukweri badala yake ushabiki na dharau vilikuongoza kuandika upumbavu na ujinga.
 
Sanaa ya bongo inatengeneza maskini wenye majina makubwa
Juzi niliona kwenye taarifa ya habari (TBC) kijana mmoja toka iringa anataka auze figo yake ili aweze kutoa filamu yake...

Nikashangaa sana, maana kuna watu wametoa filamu zaidi ya 100 lakini wana hali mbaya, yy filamu moja anataka kuuza figo
 
Juzi niliona kwenye taarifa ya habari (TBC) kijana mmoja toka iringa anataka auze figo yake ili aweze kutoa filamu yake...

Nikashangaa sana, maana kuna watu wametoa filamu zaidi ya 100 lakini wana hali mbaya, yy filamu moja anataka kuuza figo
Ni umaskini wa fikra hajui vizuri kuhusiana na Sanaa ya bongo hiyo akitoa ya kwanza asipouza filamu vizuri si atatoa nyingine tena
 
Legend achangiwe pesa apate matibabu
Pesa yote anayoingiza kwenye matangazo na sinema
Mm Nlijua Mzee majuto akaunt yake haikosi Mln 400 Hivi....hawa wasaniii watakuwa wana matumizi ya ziada si bure wao wakiumwa kutwa kutaka kichangiwaa tu
Wakiwa wazima mbwembwe nyingi tu
Wakati umefika kwa wasanii wajifunze wasiishi kwa kuiga
Mfano Leo usikie daimond kapata ugonjwa gafla alafu atake kuchangiwa hayo si maajabu wakati mtu anakuambia show yake moja analipwa Mln 200

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…