Hussein Massanza
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 1,016
- 2,195
Akihojiwa katika Kipindi cha Mkasi cha EATV mwishoni mwa mwaka 2014, Msanii Mkongwe wa vichekesho na mchekeshaji bora zaidi aliyewahi kutokea Tanzania, Amr Athuman almaarufu kama Mzee Majuto, alitoa ombi lake la kununuliwa Trekta ili kuweza kumudu kuendesha maisha yake ya uzeeni kupitia kilimo baada ya kuachana na sanaa ya maigizo aliyoitumikia kwa zaidi ya miaka 20 sasa.
Kwa msisitizo mkubwa, Mzee Majuto alimwomba Rais wa JMT, Mhe. Jakaya Kikwete kama anamsikiliza, amsaidie kwenye hilo na atamshukuru sana kwani atamrahishia kutimiza ndoto zake, ambazo ni kupumzika nyumbani kwake Tanga pindi atakapostaafu kazi yake ya kuigiza!
''Kama ananisikiliza, Namwomba Mhe. Rais aninunulie gari ya kulimia, ili namimi eeh. niweze kupata walau kulima nikiwa mapumzikoni huko nyumbani, kwani ndoto yangu ni kuja kufanya kilimo nikiacha kazi hii ya sanaa''. Alisema Mzee Majuto katika kipindi cha Mkasi EATV.
Mtangazaji Salama Jabir, kwa udadisi alimuuliza Mzee Majuto kama anafahamu bei ya hilo Trekta, Naye kuonyesha ni kweli anahitaji alijibu kuwa alifuatilia na kujua ni takribani Sh. Milioni 25 za Kitanzania.
NB: Huu ni Ukumbusho tu kwa Mheshimiwa. Kama atajitolea kumsaidia, maana bila shaka ametingwa na mambo mengi na Muda wenyewe ndo huu wa lala salama!