May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Moja ya nyimbo kali zilizovuma zinazoongelea Muungano ni Wimbo maarufu wa Nguli wa Muziki Mzee Makasi. Wimbo huu unakumbusha vizuri sana tarehe ya Muungano hivyo ningetamani kuona CCM wanakuwa na utamaduni wa kuwakumbuka japo kwa kuwatambua tu haswa ifikapo maadhimisho ya siku ya Muungano, kwani Mzee wetu bado yupo. Ingawa kwa sasa Mzee ameshaachana na Muziki wa kidunia.
Mwaka sitini na nne Tanganyika na Unguja.
Nyerere naye Karume hawakutaka kungoja
Walifanya chini dede Tanganyika naitaja
kuwepo kwa ccm muungano umefana
Ni muungano wa kweli wa kuigwa Africa
Hauhitaji kibali kwamba utaghalifika
Mwanzo nini serikali sasa chama ni kimoja
CCM ni kikali lengo lake ni umoja
Nyerere naye barani hata kule visiwani
Wamwamini makini Kiongozi wa kanuni
CCM amebuni Muungano kaidhini
Kuwepo kwa CCM muungano umefana
Sasa Muungano kweli bara Pwani na Unguja
Baraza la Mapinduzi hata kule Visiwani
Limekataa upuuzi chama ndio darubini
Jumbe Mwanamapinduzi yupo kwenye usukani
*hapo kwenye red sina uhakika na hayo maneno...natamani mwenye kujua aseme maneno sahihi.
Mwaka sitini na nne Tanganyika na Unguja.
Nyerere naye Karume hawakutaka kungoja
Walifanya chini dede Tanganyika naitaja
kuwepo kwa ccm muungano umefana
Ni muungano wa kweli wa kuigwa Africa
Hauhitaji kibali kwamba utaghalifika
Mwanzo nini serikali sasa chama ni kimoja
CCM ni kikali lengo lake ni umoja
Nyerere naye barani hata kule visiwani
Wamwamini makini Kiongozi wa kanuni
CCM amebuni Muungano kaidhini
Kuwepo kwa CCM muungano umefana
Sasa Muungano kweli bara Pwani na Unguja
Baraza la Mapinduzi hata kule Visiwani
Limekataa upuuzi chama ndio darubini
Jumbe Mwanamapinduzi yupo kwenye usukani
*hapo kwenye red sina uhakika na hayo maneno...natamani mwenye kujua aseme maneno sahihi.