Elections 2010 Mzee Malecela akubali matokeo

Elections 2010 Mzee Malecela akubali matokeo

Brooklyn

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2009
Posts
1,459
Reaction score
286
HABARI TOKA JIMBO LA MTERA LINASEMA MGOMBEA LIVINGSTONE LUSINDE AMEMSHINDA MH. JOHN SAMWEL MALECELA KATIKA KURA ZA MAONI NA ANATEGEMEA KUWA NDIYE ATAYEPITISHWA KUGOMBEA UBUNGE KWA TIKETI YA CCM KWA JIMBO HILO, KWA MUJIBU WA MATOKEO YALIYOTANGAZWA SAA 4 LEO
Source: Michuzi blog

Jamani hawa wazee mbona hawasomi alama za nyakati mpaka wanasubiri kuaibishwa namna hii??

.......wapi FMEs...!!

 
Is it true, and only true that Mzee Tingatinga kashindwa? Mbona siamini?
 
naona mzee kajiunga na Makweta na Mungai kwenda likizo ya 'lazima',ndo si ha sa hiyo!
 
Nafikiri miaka 10 ijayo tutashuhudia mabadiliko makubwa sana ya kisiasa hapa nchini, wananchi wameanza kuamka!!

Pongezi kwa Mh. Rais Kikwete kwa kuleta mfumo wa kidemokrasia zaidi wa kuchagua wabunge na madiwani ndani ya CCM.
 
Haya mageuzi ya ndani ya CCM yanaonesha ukomavu wa JK katika siasa.Hii ndiyo demokrasi ndani ya chama.pole Mzee Malecela.
 
Binadamu ndivyo tulivyoumbwa kung'ang'ania vyeo. Huyu mzee toka nikiwa shule ya msingia miaka ya 80 yuko kazini, na isitoshe kwa cheo chake cha Waziri Mkuu mstaafu ana pension ya kutosha tuu!!
 
Ndicho alikuwa anangojea kwani mtu kama ulishakuwa PM,makamo mwenyekiti hutakiwi kuwa namahangaiko yakisiasa!hii ndiyo malipo yake!!Unadhani Salim Ahamed Salimu,Warioba hawataki kugombania katika majimbo??wanaogopa fedhea kutokana na status waliyokwishafikia kuporomoka ghafla.
 
Ving'ang'anizi! Wenzao wabunge wa kule Rukwa walisoma dalili za nyakati wakaachia kwa heshima.
 
naona mzee kajiunga na Makweta na Mungai kwenda likizo ya 'lazima',ndo si ha sa hiyo!

Jamani hawa ni wabunge wastaafu....hamkumbuki kuwa Msekwa alibwagwa na bado anaitwa Spika mstaafu na anapewa marupurupu ya ustaafu?...only in Tanzania
 
Ndicho alikuwa anangojea kwani mtu kama ulishakuwa PM,makamo mwenyekiti hutakiwi kuwa namahangaiko yakisiasa!hii ndiyo malipo yake!!Unadhani Salim Ahamed Salimu,Warioba hawataki kugombania katika majimbo??wanaogopa fedhea kutokana na status waliyokwishafikia kuporomoka ghafla.

Kwa nzi, kidonda ni kitamu.
Kwa hiyo: Nzi kufia kwenye kidonda si halamu!
 
Haya mageuzi ya ndani ya CCM yanaonesha ukomavu wa JK katika siasa.Hii ndiyo demokrasi ndani ya chama.pole Mzee Malecela.

Hapana sio ukomavu wa kisiasa isipokuwa muda wa mabadiliko umefika. Nyerere alipokubali mfumo wa vyama vingi haukuwa ukomavu wa kisiasa isipokuwa wakati ni ukuta. JK ni jeuri na dictator wa siri siri, na wewe ngoja tu ashindwe kwenye kura October ndipo utakapoona sura yake halisi. Fikiria, wafanyakazi kutaka kugoma tu, akaleta mkuu wa majeshi na mkuu wa jeshi la polisi ili kuwatisha watanzania. Sasa ngoja uone mwezi October, Judge Lewis Makame atatangaza matokeo huku nyuma yake kuna mtutu wa bunduki, na JK ataapishwa usiku chapu chapu. Usicheze na JK.
 
Yaani huyu dogo aliyemshinda alikuwa na umri kama wa miaka 3 hivi wakati mzee mzima ni mbunge tayari!!!!!!!!!!!!!!!! Jamani hawa wazee wetu kwao msamiati wa kujiuzulu madaraka hawajui kabisa?? tusubiri sarakasi za NEC ndo tutakoma kabisa maana kuna watu wanacheka kwa sasa eti wameshinda wakati NEC inakaa 14 August 2010. CCM issue sio kushinda bali kutangazwa mshindi
 
Usichoamini ni nini? Kwani Malecela ni mara ya kwanza kushindwa kura za ubunge?

Nawapa pole wanaodhani Malecela kashindwa ubunge!! Ameshindwa kura za maoni tu. Anrudi bungeni mapema Nov'10. Shangaa!!
 
Mijitu ya ccm haijui kusoma alama za nyakati, aibu ilyoje , mende kuangusha kabati. Bado jk sasa.
 
Back
Top Bottom