Mzee Maxwell na Historia ya TANU 1950s

Mzee Maxwell na Historia ya TANU 1950s

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MZEE MAXWELL NA HISTORIA YA TANU

Mzee Maxwell kaniona mimi toka udogo wangu labda hata sijaanza kutembea.

Nimemjua Maxwell kwa jina lake hili moja.
Maxwell alikuwa pamoja na Dome Okochi Budohi na Martin.

Hawa walikuwa wametoka Kenya wamekuja Tanganyika kutafuta maisha.

Hawa wote watatu waliingiliana na wazee wangu na ndiyo kisa cha Maxwell kunijua mimi.

Nakumbuka Coca-Cola yangu ya kwanza alininunulia Okochi Budohi kwenye duka la Mwarabu lililokuwa nyumbani kwa Mama Kilindi Mtaa wa Kipata na Swahili.

Ilinipalia.
Nakumbuka kama jana vile.

Dome Budohi akanifundisha namna nzuri ya kunywa Coca-Cola ni kuacha itulie kwanza ndipo chupa uipige tarumbeta.

Dome Budohi alikuwa na baiskeli na wakati mwingine akinipakia mbele kwenye frame na kunizungusha mtaani.

Wakenya hawa wote walishuhudia kwa macho yao TANU ikiasisiwa na Dome Budohi alikuwa ndani ya TAA kama kiongozi.

Dome Budohi alikamatwa kwa tuhuma za kuhusika na Mau Mau akarudishwa Kenya kufungwa kisiwani Lamu mwaka wa 1955.

Huu ulikuwa msako maalum dhidi ya Wakikuyu na makabila mengine kutoka Kenya.

Mzee Maxwell yeye hakurudi kwao Kenya alibakia Dar es Salaam na kwa miaka yote niliyomjua ukubwani alikuwa akifanya biashara ya madini.

Mzee Maxwell yeye ndiye aliyenipa anuani ya Dome Budohi na nikamwandikia.

Ilikuwa katika msako huu wa Mau Mau Tangayika ndiyo Dome Budohi na Wakenya wengi waliokuwa wanaishi Tanganyika walikamatwa.

Nilipokutana na Dome Budohi Nairobi mwaka wa 1972 alinieleza kuwa yeye kilichomkamatisha hasa ilikuwa barua kutoka Kenya ambayo Martin aliwaonyesha makachero wa serikali.

Dome Budohi anasema hawakuwa wanajua kuwa Martin alikuwa kachero wa Waingereza.

Kisa cha kukamatwa kwa Dome Budohi nimekieleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.

Kwa hakika ni kisa cha kusisimua kikianzia Central Police jengo ambalo hivi sasa linatazamana na Railway Station.

Kutoka selo za Central Police akiwa katika minyororo alisafirishwa na wafungwa wengeni hadi Handeni wakiwa ndani ya mabehewa ya kusafirisha ng'ombe.

Hapa Handeni ndipo ilipokuwa kambi ya Mau Mau kituo cha kwanza Tanganyika kabla hawajapelekwa Kenya.

Hapo Handeni alikuwapo Rashid Mfaume Kawawa kama mtumishi wa serikali ya kikoloni ndani ya kambi ile.

Kisa cha Dome Budohi nimekieleza kwa kirefu katika kitabu cha Abdul Sykes.

Dome Budohi alinieleza mengi.

Katika hayo ni masikitiko yake kushindwa kuonana na Julius Nyerere baaada ya Kenya na Tanganyika zote kuwa huru.

Dome Budohi anasema alifanya juhudi kubwa akutane na Julius Nyerere mtu ambaye walikuwa wanafahamiana vyema kabisa kila Nyerere alipokwenda Nairobi kuonana na Jomo Kenyatta lakini hakupata kufanikiwa.

Mwalimu alikuwa akipata salamu zile lakini hawakukutana.

Siku zote najiuliza ingekuwaje wazalendo hawa wawili wenye kadi za TANU No. 1 na No. 6 wangekutana na kukumbushana yale yaliyopita.

Ingekuwaje kama wangepiga picha ya pamoja Julius Kambarage Nyerere na Dome Okochi Budohi na pengine historia yao hii ikachapwa katika magazeti ya Kenya na bila shaka ukurasa wa mbele kwa maandishi meusi yaliyokoza.

Ingekuwaje?
Bila shaka hii ingekuwa "Big Story."

Siku zote huiuliza nafsi yangu ingekuwaje?

Ingekuwaje kwa hakika historia ya Dome Okochi Budohi Budohi Mluya kutoka Kenya kutambulika kuwa alishiriki katika kupigania uhuru wa Tanganyika na kadi yake ya TANU ni No. 6.

Ingekuwaje?

Picha: Mzee Maxwell tumesimama Mtaa wa Mafia na Ukame jirani na Msikiti wa Manyema.

Picha ya Dome Okochi Budohi.

1720237111714.jpeg

1720237151275.jpeg

View attachment 3034691
View attachment 3034692

"alisafirishwa na wafungwa wengeni hadi Handeni wakiwa ndani ya mabehewa ya kusafirisha ng'ombe"! Naona kama haiko sawa hii, hii ni Handeni ya wapi ya Tanga haikuwa na reli ila barabara ya kwenda Tanga ilipita huko ukitoka Iringa, Morogoro na Dodoma.
 
Alikuwa Mzee Sikukuu nae Alikuwa Mluya nadhan ndiye muasisi WA huo mtaa wa Sikukuu . Amefariki 2020 kama sikosei
 
"alisafirishwa na wafungwa wengeni hadi Handeni wakiwa ndani ya mabehewa ya kusafirisha ng'ombe"! Naona kama haiko sawa hii, hii ni Handeni ya wapi ya Tanga haikuwa na reli ila barabara ya kwenda Tanga ilipita huko ukitoka Iringa, Morogoro na Dodoma.
His...
Dar-es-Salaam hadi Korogwe kwa treni kisha Handeni.
 
Back
Top Bottom