Uchaguzi 2020 Mzee Membe uko pande zipi? Nini shida sikusomi kabisa.Umemsikia Bashiry Ally? Tupe ukweli

Uchaguzi 2020 Mzee Membe uko pande zipi? Nini shida sikusomi kabisa.Umemsikia Bashiry Ally? Tupe ukweli

hayaland

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2012
Posts
712
Reaction score
399
Mzee wangu Membe ulisafiri kwenda Dubai falme za Kiarabu kwenye vikao vyako vya kila mwaka,jamii ya kitanzania ilikusubiri kwa hamu ili kuanza kampeini katika maeneo mbalimbali nchini.Umerudi salama mungu ni mwema hujaonekana kabisa kwenye kampeini zako.

Kibaya zaidi katibu wako alikamatwa pale uwanja wa ndege JKIN kwa kile kinachosemekana alikuwa amebeba fedha nyingi kitu ambacho jeshi la polisi wanadai ni mwendelezo wa vitendo vya utakatishaji haramu wa fedha na bado anafanyiwa uchunguzi.Japo wewe ulikanusha kuwa hakuwa na pesa yoyote.

Sasa uko wapi mzee wangu.Kampeni vipi.Ndo umekosa pesa kabisa ya kufanyia kampeni.Umemsikia katibu wa Ccm Dr Bashir Ally Kakulwa jembe la kihaya akisema mtu akitoka CCM na kuhamia kwingine anakuwa kichaa je umekuwa kichaa kama anavyodai?

FB_IMG_15967025059890027.jpg
 
Membe eti kawa kichaa. Mji wa moto huu
 
Bashiru hakumtaja Membe, kasema mtu akitoka CCM anakuwa kichaa Kuna wengi wametoka CCM hata Nyalandu pia alitoka CCM .
 
Membe anafanya hesabu za Ankara,akimaliza atatoa majibu,nadhani Zitto alitegemea Membe atakisaidia chama kifedha.
 
Alienda Dubai kuchukua mpunga aje kula Bata wamezitia ndani za kwanza, katuma Tena msaidizi mwingine nae kadakwa! Sasa pumzi atatoa wapi?

CCM mnajifanya mnajua siasa sana, pambaneni na Lissu sasa hakuna kugawanya kura mwaka huu kama mlivyotegemea. Kachero mbobezi anaenda kwa mwendo wa kikachero tu hatangazi kumuunga mkono Lissu na hapigi kampeni.

Mitego yenu yote imeteguliwa kikachero,kama mnafikiri shida ni pesa za kamoeni mbona Zitto anazinguka kuwapigia kampeni wabunge bila kumpigia kampeni Membe.
 
Alienda Dubai kuchukua mpunga aje kula Bata wamezitia ndani za kwanza, katuma Tena msaidizi mwingine nae kadakwa! Sasa pumzi atatoa wapi?
Huyo ndio anaitwa kachero mbobezi[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mzee wangu Membe ulisafiri kwenda Dubai falme za Kiarabu kwenye vikao vyako vya kila mwaka,jamii ya kitanzania ilikusubiri kwa hamu ili kuanza kampeini katika maeneo mbalimbali nchini.Umerudi salama mungu ni mwema hujaonekana kabisa kwenye kampeini zako.Kibaya zaidi katibu wako alikamatwa pale uwanja wa ndege JKIN kwa kile kinachosemekana alikuwa amebeba fedha nyingi kitu ambacho jeshi la polisi wanadai ni mwendelezo wa vitendo vya utakatishaji haramu wa fedha na bado anafanyiwa uchunguzi.Japo wewe ulikanusha kuwa hakuwa na pesa yoyote.
Sasa uko wapi mzee wangu.Kampeni vipi.Ndo umekosa pesa kabisa ya kufanyia kampeni.Umemsikia katibu wa Ccm Dr Bashir Ally Kakulwa jembe la kihaya akisema mtu akitoka ccm na kuhamia kwingine anakuwa kichaa je umekuwa kichaa kama anavyodai?View attachment 1574972
Amepotea kabisa kweli Siasa hizi bila kuwa na utimamu wa akili utaokota makopo kabisa
Anakoelekea sio kuzuri kabisa Mgombea huyu.
 
Membe mlimdanganya kupitia mitandao ya kijamii kuwa anakubalika sanaaa,nae akajaa kichwa akiamini ni kweli...uhalisia wa kampeni unamtoa kwenye reli anataka kusingizia kuwa wanaungana
 
CCM mnajifanya mnajua siasa sana, pambaneni na Lissu sasa hakuna kugawanya kura mwaka huu kama mlivyotegemea. Kachero mbobezi anaenda kwa mwendo wa kikachero tu hatangazi kumuunga mkono Lissu na hapigi kampeni.

Mitego yenu yote imeteguliwa kikachero,kama mnafikiri shida ni pesa za kamoeni mbona Zitto anazinguka kuwapigia kampeni wabunge bila kumpigia kampeni Membe.
Hata mkiungana kula hazibadiliki, Lisu ana 14% na Membe ana %3 jumla ni 17% kwa hiyo bado saana.
 
Back
Top Bottom