Kwa maoni yangu wakati Hayati Mzee Mkapa akiingia madarakani mwaka 1995 alianza na Mikakati ya kuweka mifumo mbalimbali ambayo hadi sasa imekuwa endelevu. Kipindi hicho ndicho kiliibua Maboresho katika Utumishi wa Umma.
Hii iliendana na dhana ya ajira kwa kuzingatia sifa pamoja na kuibua viongozi wenye vipaji,weledi na wabunifu na wazalendo kwa ngazi mbalimbali za Taasisi za Serikali na Mashirika ya Umma.
Sheria ya Utumishi wa Umma Na 8 ya 2002 ilitungwa na miundo na mifumo ya kupandisha vyeo ilipitiwa. Viongozi wengi kuanzia ngazi ya Rais, Mawaziri, Makatibu wakuu, wakuu wa Idara za serikali walioko serikalini na waliostaafu salama na wachapa kazi wengi wao ni zao la Mkapa. (Mimi ni zao lake pia)Kipindi hiki tulifanya kazi kwa bidii na maarifa ili kufikia Malengo tena yanayopimika na kwa kuzingatia Sera Sheria kanuni na taratibu. Aidha,Mindset za wafanyakazi zilibadilishwa na dhana ya uwazi na ukweli
Ndiyo maana nimesema kipindi hiki kilikuwa cha kutengeneza Mifumo na Uongozi wa baadaye ndiyo maana tunao Mhesh Rais J Magufuli,Kikwete nk. ambao nao ni zao lake. Hivyo,TUMUOMBEE na kama ilivyo kwa viongozi wengine nashauri tuwe na MKAPA DAY kama kumbukumbu endelevu kwa Taifa ie Siku ya Utumishi wa Umma Public Service Day iitwe hivyo. RIP MZEE WETU.AMEN