Mzee Mohamed Said - BAKWATA mwiba mzito kwa Waislam Tanzania

Mzee Mohamed Said - BAKWATA mwiba mzito kwa Waislam Tanzania

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
Sheikh Mohamed Said akitoa muhadhara kwa vijana wa kiislamu kufahanu historia ya taasisi za kiislamu Tanzania na michango ya taasisi hizi :

View: https://m.youtube.com/watch?v=IvodWTgWpSM
East African Muslim Welfare Society, migongano ya waislamu tanzania kwa kufuata asili ya mtu.

Mambo yakawa mazito 1968 muafaka miongoni mwa waislamu wa Tanzania ukashindwa kufikiwa.

Kina mama wa kiislamu watokwa macho kwa hali hii ya waislamu kuhitafiliana kwa kuangaliana asili, badala ya kuwa umma mmoja usio na chembe za kibaguzi .

Kuanzia hapo maendeleo na mipango ya waislamu ikavuzurugika, makundi ndani ya uislamu Tanzania yakaibuka

Wafadhili waliotaka kujenga Chuo Kikuu chini ya ufadhili wa Aga Khan wakatoweka kutokana na kutofautiana waislamu ndani ya Tanzania

Mzee Mohamed Said akaendelea na mudhara wake akawapa changamoto wanafunzi kama wanaelewa kwanini wanavaa hijabu, haikuwa kazi ndogo nitawaeleza ..
 
Sheikh Mussa Kundecha asimulia kashikashi nyingi alizopitia akiwa mwanaharakati Tanzania

View: https://m.youtube.com/watch?v=rDaa_3GLI2Y

Kiongozi wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu asimulia jinsi alivyopewa kesi ya mauaji baada ya kutoafikiana na Polisi waliolazimisha aongee mbele ya vyombo vya habari kituo cha Polisi awaombe Waislamu waliokuwa na mpango wa kuandamana wasifanye hivyo. ...

Wakati huo Polisi Dar es Salaam mkuu wa upelelezi mkoa ni RCO Abdallah Zombe anaongoza .... nikatupwa selo asubuhi mahakamani nikasomewa kesi ya mauaji ya watu wawili kwa risasi mmoja askari polisi na mwingine raia, kutoka hapo nikapelekwa rumande Segerea miezi 6 ....

Kuhusu siasa Sheikh Mussa Kundecha anasema huwezi tenganisha siasa na dini.

Upande wa elimu anaelezea umuhimu wa suala hilo ... nilisoma Tabora kisha kwenda nje Burundi, Kenya, Saudi Arabia kuongeza elimu nikarudi Tanzania nikafundisha Tabora, Arusha na Dar es Salaam mitaa wa Kiungi Magomeni pia Kinondoni Mkwajuni na msikiti wa Kichangani Magomeni.

Mihadhara ya MwembeChai iliyoshamiri kuanzia mwaka 1994 hadi 1997 jijini Dar es Salaam iliniletea matatizo miaka hiyo ikiongozwa na kina sheikh Mazinge na wengine ...

Pia nilifanya kazi ya kuunganisha waislamu ambao ni wasomi (professionals) wa elimu pana ya kisecular na masheikh wa wanaotoa elimu ya dini, kwani makundi haya mawili yaani professionals wa kiislamu waliona masheikh wao hawana ufahamu wa masomo ya elimu ya secular huku pia masheikh wakiona waislamu wasomi kuwa hawana ufahamu wa dini yao.

Harakati hizi zimeleta mafanikio kuna misikiti zaidi ya 3,000 na huku kuna shule zaidi ya 300 za waislamu kutokana na kuunganisha nguvu za waislamu ....

Mussa Kundecha anaulizwa sheikh ni nani hasa ... pamoja ya kuwa sheikh ni kama inatumika kuonesha kuwa ni mtu mzima isipokuwa katika utaratibu ....

Sheikh Mussa Kundecha akiangalia mbele kuhusu kupata elimu ya dini, anashukuru kuwa mazingira yanazidi kuwa mazuri vitabu vipo vingi tofauti na zamani hapa Tanzania kilikuwapo kitabu kimoja cha Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy .. sasa kuna vingi zaidi ...

Kuhusu BAKWATA - Baraza Kuu La Waislamu Tanzania kutokubaliwa na baadhi ya waislamu, Sheikh Mussa Kundecha anasema kila mmoja ana nafasi yake hivyo ...

Wateja wengi wa Islamic Banking Tanzania ni wale wasio waislamu na wamewapita kwa idadi kubwa huku waislamu wakiwa wachache hivyo ni jambo jema la kijamii kwa wasio waislamu kuwa wengi sana kwa idadi ktk Benki za Kiislamu ...anabainisha Sheikh Kundecha
 
KONGAMANO LA KIMATAIFA | NAFASI YA MSIKITI KTK KUITENGEZA JAMII

SKIA ALICHOSEMA AFANDE MSIKITIN, HAYA MAMBO YAPO KULIKO POLISI



View: https://m.youtube.com/watch?v=SrGlycVzLhE


Naye Sheikh azungumzia masuala mengi ikiwemo Haiba ya mtu mmoja mmoja na umma wa waislamu kwa ujumla .. taasisi za misikiti . .. ya masuala stratejia ... minyororo ya kubaki katika umasikini ... kukasimiwa madaraka .... siyo kuburuzwa .... tuna mfumo ... na qisa kadhaa baina madola ..

View: https://m.youtube.com/watch?v=RDDZxjUCrxU
 
Kwa undani :

Toka maktaba:

Simulizi za Mjukuu wa Mfalme Mlinganaweka AleiwaLunga wa maeneo ya Wamachinga Pwani ya
Tanzania

Simulizi za wazee wetu : Waasisi wa madhehebu ya Ma- Shia nchini
Tanzania na kwanini dhehebu la Shia lina kanuni la kukubali vijana wao kuuliza maswali (tabligh) wakati Sunni hukataza vijana wao kuuliza maswali na kulazimishwa kuwa mkubwa ktk imani yaani sheikh / Imamu / Maalim akisema basi yeye ndiye anafahamu ilm yote ya dini

(NZIMA)-SIMULIZI YA MAREHEMU SHEIKH ABDALLAH SEIF (1939 -2020) - HISTORIA YETU part 1



KIU YA ILMU, SHEIKH ABDALLAH SEIF ILIMPELEKEA KUSOMA KWA MIAKA 11 MFULILIZO KATIKA NCHI ZA IRAQ, LEBANON NA IRAN (1968-1979)

Sheikh Abdallah Seif Linganaweka anatujuza kuwa Wenyeji wa Lindi jina Lao la asili ni Wakudewe kwa sasa almaaruf wanafahamika kama waMachinga wa pwani ya Lindi.

Babu yake Babu Abdallah Seif alikuwa mfalme Mlinganaweka AleiwaLunga mwenye watumwa baada ya kuwazidi wanyonge majirani kuja kuwatumikisha kujaza vyakula. Mfalme Alei(Ali)waLunga.. wa Lindi.

Baada ya kuja mkoloni Muingereza nchini Tanganyika, aliua ufalme na kubakiza uchifu. Sehemu za pwani ziliathirika kwanza kwa kupoteza ufalme mapema kabla ya watu wa bara.. Pwani wakabakia na usheikh na uchifu... usiokuwa na nguvu kama falme za asili za maeneo yao Lindi / Kilwa kabla ya kuja ukoloni...

Sheikh MbogaBure mjuzi wa lugha ya Kiarabu, dini pia mmoja wa waanzilishi wa madhehebu ya Shia Tanzania amuunganisha Mzee Abdallah Seif kupata scholarship kwenda Baghdad, Iraq mwaka 1968 kusoma zaidi dini...

Kijana Abdallah Seif mwaka 1968 alipokwenda Kijijini ashutumiwa kupotea kwa kuukumbatia u-Shia mojawapo ya madhehebu ya dini ya KiIslamu, wakati wengine wote ni Sunni. Lakini babu yake msomi wa dini madhehebu wa Sunni anayetambulika Lindi na Kilwa hakuwa anatoa shutma zozote alikuwa msikivu na kumtia moyo Abdallah Seif asome zaidi na ili kuifahamu dini vizuri zaidi.

Kilichomsukuma Sheikh Abdallah Seif kuvutiwa na u-Shia ni namna masheikh wa ki-Shia walivyokuwa wazi (tabligh) kukaribisha maswali tofauti na madhehebu mengine ya KiIslam ambapo kijana hakuruhusiwa kuhoji na pia kuuliza maswali ilikuwa inachukuliwa ni utovu wa nidhamu kwa waalimu au masheikh wake.

Safari ya Sheikh Abdallah Seif wenzie vijana wakiwemo kina Sheikh Isihaka Pingili kwenda Iraq kwa meli iliwachukua mwezi mzima kupitia bandari mbalimbali za Zanzibar, Tanga, Mogadishu, Bahrain na kuishia Basra nchini Iraq na kutua katika chuo cha Hawza mji wa Najaf Iraq

Ujio wao Basra, Iraq ulileta tafrani kwa mwenyeji wao Mpakistani mfanyabiashara mkubwa nchini Iraq enzi hizo na kupelekea Saadam Hussein kumshutumu mfanyabiashara huyo tajwa kuleta majasusi wa kiAfrika ikumbukwe ndiyo kwanza Saddam Hussein na chama chake cha Baath walikuwa wanajaribu kushika hatamu za kuongoza nchi baada ya mapinduzi nchini Iraq. Mpakistani huyo alinyongwa mwaka 1969 pamoja na wafadhili wengine kama kuna Bakri Sadr waliowezesha ujio wa vijana wa kiAfrika kuingia Iraq kwa dhumuni la kusoma dini.

Kutokana na hilo ikabidi Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine wa kiAfrika waondoke Iraq mwaka 1970 kwenda Lebanon kwenda kuendelea na azma yao ya kusoma dini.

Sheikh Abdallah Seif wakakaa Lebanon kuanzia mwaka 1970 mpaka 1978 ambapo mara nyingine masomo ya dini yakaingia changamoto baada ya vita baina ya Wapaletina waliokuwa kambi za ukimbizi Lebanon na waLebanon wenye nchi na kuzua vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mwaka 1978 Ikabidi Sheikh Abdallah Seif na wenzie wahamie nchi ya jirani ya Iran kwenda katika mji wa Qom city kuendelea na masomo yao ya dini. Iran ilikuwa imetulia nchi ya amani chini ya utawala wa mfalme (Shah) Mohammed Reza Pahlavi Historic Personalities of Iran: Mohammad Reza Shah Pahlavi miaka 7 waliakaa Iran wakiendelea kusomeshwa.

Wakati wa likizo Iran wengine wenda Ufaransa kuchuma zabibu mashambani au kufanya kazi sehemu za utalii wa ndani wa Iran au kuchukua mabusati ya kushona ya Iran yanayosifika Uarabuni kote kwenda kuyauza ktk nchi mbalimbali za Arabuni ndivyo mwanafunzi kama Sheikh Abdallah Seif na wenzie vijana walivyojiongezea fedha za kujikimu na kupeleka kiasi cha pesa nyumbani Tanzania.

Hatimaye mwaka 1980 baada ya kusoma kwa miaka 11 nje ya Tanzania ,walitunikiwa shahada ya baccalauréat ya masomo ya dini na kurejea Tanzania. Kwa miaka hiyo 11 ughaibuni pia waliweza kusoma elimu ya secular kiwango cha sekondari kwa njia ya posta masomo ya nchi ya Uingereza kwa msaada mkubwa wa swahiba wa kiongozi wa kijeshi wa Nigeria Jenerali Yakubu Gowon. Swahiba huyo alikuwa mfanyabishara wa vituo vya mafuta na makazi yake Uingereza.

Mahojiano haya yanakuja kwa hisani kubwa ya Ammar Dachi aliyemshawishi Mzee Abdallah Seif kufunguka historia ya mapito yake, ukoo , ilmu na utafiti wa mafuta 1955 na pia ujio wa madhehebu ya Shia nchini Tanzania


HISTORIA YA ABDALLAH SEIF (1939 -2020) Part - 2



Sheikh Alhaj Sheikh Abdallah Seif Linganaweka mzaliwa na mwenyeji wa kijiji cha Mnan’gole sehemu za Dimba mkoa Lindi Tanzania anaendelea kusimulia kazi kubwa aliyofanya ya kujitolea ya kueneza dini.

Sheikh Abdallah Seif anasisitiza umuhimu wa ilmu na elimu kwa wanazuoni wote wa KiIslamu.

Anasema ili sheikh awe mwanazuoni aliyekamilika kufundisha chuoni lazima kusoma ilmu ya dini kwa angalau miaka 15.

Anakumbuka alivyokuwa mjini Qom Iran akisoma chuoni alionana na wazee wenye umri wa miaka 70 wakijiendeleza na kuwaambia wao vijana kuwa inahitajika jumla ya miaka 35 ili kuielewa dini nje ndani kwa ufasaha. Wazee hao walicheka waliposikia vijana Sheikh Abdallah Seif, Sheikh Isihaka Pingili na vijana wengine toka Afrika wakisema wanataka kusoma dini kwa miaka 5 mpaka 10 tu ilihali wametoka Afrika na kuwaambia bila kupepesa macho kuwa ili wawe wabobevu wafikirie miaka angalau 15 ya ilmu ya dini ngazi ya chuo.

Hivyo akiwa amepikika kwa elimu tosha ya kidini baada ya kufanya kazi kwa takriban miaka 11 nchini Tanzania, mwaka 1990 sheikh Abdallah Seifu alikwenda Nampula jimbo la Cabo Delgado nchini Mozambique kufanya kazi ya dini.

Kisha sheikh Abdallah Seif alishuka mpaka mji mkuu wa Maputo Mozambique na alisaidia kufungua taasisi rasmi inayotambulika na serikali na kupewa leseni iliyosajiliwa Maputo Mozambique kwa ajili ya taasisi ya Shia Ithna-Asheri Muzdalifah . Sheikh Abdallah Seif anazungumza lugha za Kiswahili, Kiarabu, Kiingereza na Kireno.

Source : Asadiqmedia

RAMBIRAMBI NA WASIFU - Marhum Sheikh Abdallah Seif



Source : Asadiqmedia
 
Kupitia simulizi zake zilizojaa chuki dhidi ya uKristo sijui vijana wa kiislam wanafahidi nini ?.
 
Back
Top Bottom