Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MZEE MOYO KATANGULIA KWENYE HAKI NA HAMZAH RIJAL
Anapotangulia mmoja kati yetu kwenye haki huzungumzwa marehemu kwa yale aliyoyafanya yakiwa ya kheri huzidi kupambwa, kuna wengine hufanya kila aina ya varange na fujo nao watu watatafuta hata jema mmoja wamzungumze.
Wenye kalamu wameandika kwa namna wanamvyojua Mzee Hassan Nassor Moyo, kuna waliokaa nae na kuna waliofanya kazi naye, kuna waliokuwemo kwenye harakati naye hao wote hawakusita wakachukua kalamu na kuzicharaza kama charahani kumuelezea mzee Moyo, mie sio kati ya wenye kalamu wala niliokaa naye au kufanya kazi naye.
Sasa yakiwa sio ya hayo kwanini naamua kuandika mistari miwili mitatu juu yake?
Nitamzungumzia labda kwa makataa 3 juu yake, mmoja mzee Moyo kuweza kunikutanisha na Maalim Aboud Jumbe aliokuwa Rais wa pili wa Zanzibar, pili kukutana naye Msikiti Gofu akiwa na mwenzangu tuliosma pamoja Skuli ya Darajani Primary School huyo sio mwengine, Abdalla Said Seif na mwisho juu ya Makala nilioiandika kuhusu Biashara za Nje (BIZANJE).
Mzee wangu Al-Marhoum Maalim Zubeir Rijal alikuwa mwenzake sana Al-Marhoum Maalim Aboud Jumbe, walikutana Makerere College ila mzee wangu alimtangulia kwa mwaka mmoja na wakaja kusomesha pamoja King George VI hii inayoitwa Lumumba College kwa sasa.
Mzee wangu alichukua mkopo kujenga nyumba mtaa wa Saateni alikuwa mwenyewe akililipa deni kama kawaida alitangulia kwenye haki na mapema sana katika mwaka wa 1969 akiwa na umri wa miaka 47.
Sasa tukatakiwa tuendeleze kulipa deni ikiwa ni mzigo mzito kwetu, kwahio nyumba ikabidi ikodishwe ikodishwe na Serikali ili limalizwe deni, bahati mbaya tulipotaka kujua juu ya deni ikawa sio kama ilivyo kuwa deni lilikuwa kubwa na mzigo ukawa mzito mno kuweza kulipa deni ili nyumba iwe katika miliki yetu.
Hapo nikawa natafuta njia ya kuweza kukutana na Marehemu Jumbe aweze kulisuluhisha hili jambo.
Niliwakabil watu walio wakaribu naye kama 4 na kila mmoja akiniahidi na mwengine kunambia haitowezekana kuonana naye.
Nikakata tamaa nikaiwacha hali ibakie ilivyo
Nilipokuwa nafanya kazi na East African Post and Telecommunication mji wa Wete nilichaguliwa kuwa mkuu wa kituo cha simu hapo Wete nikiwaunganisha wafanya kazi wa Wete na Konde mafundi na Maoporeta.
Siku hio nimekwenda kusali sala ya Magharibi Msikiti wa Hanafi uliopo Wete mkabala na ofisi za ZSTC natoka nje baada ya kumaliza kusali nakutana na mzee Moyo nikamuamkia nikajijulisa mie ni nani, nikamuambia mimi naitwa Hamza Z. Rijal sijaongeza neno yeye akanirukia ‘’hapa unafanya nini?
Unajua mzee wenu anakutafteni mara nyingi kishawahi kukutajeni sio chini ya mara mbili tatu.’’
Nikawa najiuliza hii ni ‘’Telepathy?’’ baada ya kusema hayo nikamueleza kuwa nataka kuona na Maalim Aboud kwa kadhia ya nyumba yetu.
Jawabu alionipa ilikuwa ‘’nitamuambia lakini kwa kesho haitowezekana tunashughuli nyingi za kikazi na tunaondoka kesho kutwa asubuhi na mapema, lakini nitamuambia usitaharouk.’’
Taib, nikiwa nimeondoka kazini kwa muda narudi naamabiwa ikifika saa saba ya siku ya pili baada ya jana natakiwa Ikulu ndogo Wete, wenzangu wote wakanambia jee umeshafanya uaafriti wa aiana gani tena?
Nikawaeleza kuwa wasitaharouk nakwenda kuitikia wito ikifika kwenye saa kumi sijarudi basi wawasiliane na District Service Officer wetu, Mr. Kadir lakini sitegemei hayo.
Nilifika Ikulu ndogo na kumkuta Mzee Moyo alionipokea nikaka naye sebuleni nikawa naangaza huku na kule, mara Maalim Aboud akatokea tukasimama nakumuamkia, akaniuliza ‘’mama yenu hajambo na wale ndugu zako wawili hawajambo?’’
Nikamjibu wote hawajambo na kuna mwengine wa mwisho akakumbuka akasema ‘’Omar bin Khatab?
Huyu jina kapewa na Mwinyi Baraka na yeye akimwita Bwansomo lakini kuna sahib yetu akimwita Omar bin Khatab.’’
Mara akaja mtumishi kueleza kuwa mlo tayari tukainuka sote kwa pamoja tukiwa watu watatu mie Maalim Aboud na mzee Moyo.
Meza imechafuliwa nikiwa wakati huo nipo mjane/kapera (Bachelor) nikasema ndani ya nafsi yangu shabash leo sio siku ya wali wa maji na mchuzi kwa jina mchuzi ninaoupika haya mambo ya leo ni minal ali.
Tukajipunguzia na nilijikhini nikaambiwa hapo nyumbani nijitipe nitakavyo, maliza mwenyewe.
Huku tunakula ndipo Maalim Aboud akaniuliza ‘’nasikia unashida, jee ni kitu gani?’’
Nikamueleza hikaya nzima juu ya nyumba, hapo hapo akamwambia mzee Moyo ‘’nyumba ni yao kuanzia sasa hivi kamilisha makartasi na kila kitu.’’
Nikaulizwa kuna jengine nikasema sina, hata kama nilikuwa nalo nisingelisema kwani nilihisi ni shujaa kwenye familia.
Maalim Aboud akanambia ‘’Maalim Zubeir hakuwa mwenzangu lakini alikuwa kama kaka yangu, siku zote nilikuwa ninaota nitamlipaje kwa wema alionionyesha katika nyakati tafauti, ameondoka mapema lakini bado namkumbuka leo kwangi nifuraha kuweza kusema labda nimelip sehemu ya mema aliopata kunifanyia.’’
Aidha akanambia nikiwa na lolote lile nimwambie mzee Moyo awe kiungo baina ya familia yetu na yeye mkuu.
Yakesha na kuaga na kuwaeleza nyumbani kuwa mambo yamekaa sawa.
Sasa mzee Moyo akanambia wambie ndugu zako wakachukue stakbadhi ya nyumba.
Badaye nikaja kuelewa kuwa Maalim Aboud hakutumia ulwa wake kulimaliza deni ila alitoa pesa mfukoni mwake kisha nikalijua hilo nikiwa nipo Makka, Ndugu Musadiq kunieleza kuwa ofisi yake ndio iliotengeneza Mikataba yote yakurejeshewa nyumaba yetu.
Hakuwa alioirahisisha njia iliokuwa nzito yakupigwa chenga na kila niliomuona kuwa atanisaidia isipokuwa mzee Moyo alinirahisishia hilo, hapo siku zote nilikuwa namzungumza mzee Moyo kama mtu mkweli na hakuwa anapindisha neno, miaka sio chini ya 5 nahangaika yeye alilisuluhisha nililokuwa nalitafuta kwa siku moja tu na kila kitu kikakaa sawa katika nyumba yetu ambayo ndipo ninapoweka ubavu hivi sasa na kusema ukinitaka utanikuta nyumbani, kwani sio kwangu ni nyumbani kwenye nyumba ya urithi.
Ikapita miaka zaidi ya 15 mie naye hatukoonana uso kwa macho.
Katika mwezi wa Ramadhani huhudhuria darsa nyakati za alasiri Msikiti Gofu, kuhudhuria darsa hii nikutokana na mzee mwenyewe kufwatana naye tangu mdogo kuhudhuria darsa hio na nimeiendeleza na watoto wangu wawili wakiume nao nimewachukua tangu wadogo hadi sasa nahudhuria nao darsa hio ambayo imedumu zaidi ya miaka 100 na ushei. Tukimaliza darsa hukaa nje tukasalimiana na kuzungumza ya hapa na pale, mara nikiwa na Sheikh Muhammad Salum, mara Hajii Yusuf na wenzake, mara vijana kunizonga na mazungumzo yao.
Nikamuoma mzee Moyo siku hiyo nikamuamkia akanambia ‘’mbona hizi sura nazikumbuka?’’
Nikamuambia mie nani, akafurahi sana akataka kujua nafanya nini siku hizi?
Haakika alikuwa tayari anataka kunisaidia kama nina tatizo, nikamuleza nafanya kazi na Idara ya Mazingira, akanambia ‘’hakuna kinachomuudhi kama taka kuzagaa ovyo na mashaka ya kunguru.’’
Niliweza kumfahamisha ikawa kila akija darasani akitoka humuamkia na yeye hunita na kunambia ‘’Zubeir unasemaje?’’
Huko nyuma nikiitwa kwa jina la baba yangu lakini miaka hii imekuwa Rijal, Hamza Rijal atafahamika zaidi koliko Hamza Zubeir.
Safari mmoja niliandika Makala juu ya Biashara za Nje kutamani shirika lile lirejeshwe yaani BIZANJE, kabla ya hapo nilikwenda Malaysia kwa safari ya kikazi nikamueleza mmoja katika tuliokuwemo kwenye huo msafara akiwa mwenye nafasi katika serikali, akanambia niachane na hizo fikra kwani sasa serikali inataka kuondokana kabisa na kuendesha mambo ya biashara ipo katika kukusanya kodi na kufanya miradi ya maendeleo.
Nakutana na Mzee Moyo nakumbuka alioniambia ‘’ Zubeir hadi umeniosha kwa ile makala yako ulioiandika katika gazeti la An-Nuur juu ya BIZANJE, unamjua aliokuja na fikra ile, aliniuliza’’ Jawabu nikamjibu mara mmoja kuwa ni Dr. Ahmed Rashid, akanambia ‘’yule mtu alikuwa anaona mbali alikuja na mawazo madhbuti, bahati mbaya kufa kwa Shirika lile na maduka ya Serikali nikutokana na watu wetu kukosa uelewa.’’
Akaniulize suala ‘’Wewe umesoma wapi?’’ Nikamjibu Libya, akanambia ‘’hatokuwa mtu kasoma kule akawa na fikra mgando (static) lazima awe na sifa za kimaendeleo, Ghadafi kajitahidi kuwa mzalendo wa bara la Afrika kama kina Nkurumah, Modibo Keita, Ahmad Seketoure, Jamal Abdulnaseer na wengineo lakini watu wameshindwa kuwafahamu.’’ Akanitaka nimchapishie hio makala ya BIZANJE nimpe Abdalla Said Seif.
Nitachosema mzee Moyo alikuwa kitu kusaidia na kuona mabadiliko ndio ilikuwa dira yake kuendesha marekebu ya maisha yake.
Mie nitamkumbuka na kumuombea Allah amlaze pema Peponi na kuwa kati ya wale watakayoipata Janatul Firdaws.
Naambiwa alipokuwa anapelekwa hospitali baada ya kuzidiwa waliokuwa naye walishaona ndio anaelekea kukata roho wakawa wanasoma ‘’Ashhadu An Lailaha Ila Llah Wasshahdu ana Muhammad Rasullah’’ naambiwa akifwatisha kalima hii hadi anakata roho.
Hadithi ya Mtume SAW inasema ‘’Mwenye kutamka kalima hii kabla ya kukata roho ataipata pepo.’’
Tumuombe Allah nasi kabla ya kukata roho iwe ndio kalima yetu ya mwisho duniani, Ameen.
Kutoka Chama cha Wafanyakzi, ASP, CCM, kuasisi muwafaka, hatunaye tena Mzee Moyo.