Mzee Mtambuzi wa Jf amepata ajali asubuhi hii.

Status
Not open for further replies.

Cantalisia

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
5,221
Reaction score
2,930
Habari za asubuhi wadau,napenda kuwajulisha kuwa Baba yetu Mzee Mtambuzi amepata ajali asubuhi ya saa kumi na mbili leo ya kugongwa na gari daladala T.837 AUK na wakati akivuka barabara maeneo ya Tabata mawenzi ambapo daladala hilo lilingia kushoto gafla likiovertake daladala lingine kuwahi abiria ndipo lilimkuta baba na kumgonga.Katika ajali hiyo baba amevunjika mkono wa kulia na yuko Amana hospitali kwa matibabu,mpaka naandika hii taarifa alikuwa bado anasubiri kufanyiwa kipimo cha x-Ray nakujua amevunji

UPDATE 26,Oct.
Habari za asubuhi wapenda,napenda kuwajulisha Mzee anaendelea vizuri na anawashukuru kwa salam zenu na maombi yenu,Asubuhi hii Daktari wake ameshaconfirm kuwa operation itafanyika leo saa kumi jion,na mzee bado yupo amepumzishwa pale regency hospital chumba cha casuality kilichopo karibu na chumba cha x-ray

UPDATE 26,Oct.
Wapendwa napenda kuwajulisha kuwa kwa habari za mda huu ile operation ya Mzee Mtambuzi imeairishwa mpaka kesho saa kumi na moja alfajiri,hii ni kutokana na kuwa na wagonjwa wengine ambao kesi zao ziko sirias sana na zinahitaji operation ya haraka zaidi na madaktari ni wachache wamezidiwa, hivyo mgojwa ataendelea kuwepo hapo regency mpaka kesho akisubiri zamu yake ya kufanyiwa operation.

UPDATE 27,Oct.
Habari za asubuhi waungwana,napenda kuwajulisha kuwa Mzee hakufanyiwa tena ile oparation ameendelea kupigwa kalenda asubuhi hii wamemwambia itakufanyika jion ya leo,inasemakana daktari alikuwa na appointment nyingi kule muhimbili,bado yuko pale regency hospital.


UPDATE 28.Oct.
Habari za asubuhi wadau wa jf,napenda kuwajulisha kuwa Mzee Mtambuzi alifanyiwa operation saa sita usiku wa kuamkia leo baada ya mkono kuvimba sana,kwa sasa anaendelea vizuri kwan oparation ilifanyika kwa ufanisi mkubwa,bado yuko regency anamsubiri Daktari wake aje kumkagua na km hakutakuwa na tatizo lingine basi atafungwa POP na kuruhusiwa kurudi nyumbani,kasema ana wamiss sn na anashukuru kwa ushirikiano wenu kwa ujumla.
 

poleni sana cantalisia
 
ooooh, Poleni sana. Mungu atamsaidia tu, kueni nae karibu mmpe moyo. Dereva wa dala dala na tajiri wake wamekubali makosa na kuchukua hatua yoyote?
 
Poleni sana!

Namwombea apone mapema na kurejea katika shughuli zake za kila siku za ujenzi wa taifa na familia yake.

Sikujua: Kumbe mtambuzi ni "mzee na ni baba yake Cantalasia?"

Yes babu ni mzee na kwa umri wake km unavyoona avatara yake mimi nastahili kuwa mwanae na ndio maana namwita baba,ila co baba mzazi!
 
ooooh, Poleni sana. Mungu atamsaidia tu, kueni nae karibu mmpe moyo. Dereva wa dala dala na tajiri wake wamekubali makosa na kuchukua hatua yoyote?

Yes dereva amekubali kosa na baada ya ajali walishirikiana kumchukua mzee Mtambuzi na kumpeleka hospital na bado wako nae na wamekubali kushirikiana mpaka atakapopona.
 
Yes babu ni mzee na kwa umri wake km unavyoona avatara yake mimi nastahili kuwa mwanae na ndio maana namwita baba,ila co baba mzazi!
Poleni, mpe salam zetu kuwa tunampa pole sana na kumtakia afueni arejee katika hali yake ya kawaida.
 
poleni sana. Apone haraka.

Jamani hamma dr wa amana humu amuassist. C mnajua hosptl zetu zilivyo.
 

Poleni Cantalisia, I hate madereva wapumbavu kama hao, mimi huwaita malimbukeni, najaribu ktumia maneno laini, but I really hate them.
 
poleni sana. Apone haraka.

Jamani hamma dr wa amana humu amuassist. C mnajua hosptl zetu zilivyo.

Ameshaanza kupatiwa huduma na sasa wako njian wanampeleka Regency hospital kwa ajili ya x-ray.
 
Dah!! Pole Sana Mtambuzi, Cantalisia asante sana kwa taarifa naomba uendelee kutujuza maendeleo yake hapo Regency Hospital
 


Ee MUNGU wa Rehema na Huruma nyingi,
nakuomba umpe uponyaji wa haraka Mtumishi wako,
ili arejee kwenye kazi zake.
 
mhh pole yake
god is greta i knw he wil do da best 2him
get wel soon jamna
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…