Solo Thang alipasuka ya moyoniPamoja sana mkuu. Ndo waamke sasa
Kwabahati nzuri gazeti lako halichoshi mkuu,,nimekuelewa sana..Asanteni kwa mchanganuo wenu wa hoja hii. Ukitaka kujua kwa undani malalamiko ya wasanii naomba pata muda wa kusikiliza mashairi ya Solo Thang katika wimbo wa "MTAZAMO" wa Afande Sele/Prof. Jay, na wimbo wake mwenyewe Solo Thang wa "KILIO CHANGU". Afande Sele kwenye wimbo wake wa "Karata Dume" kagusia suala la kahimiliki, ingawa anaogopa kuwataja wahusika. Suma G pia kuna wimbo wake mmoja kalalamikia kupewa laki kwenye mauzo ya milioni!
*****************************************************
Kuna wakati nilikuwa nasikiliza redio moja maarufu ya kwa vijana hapa mjini, producer wa AY na Mwana FA bwana Hermy B aliliongelea kwa undani sana suala la copyright (hakimiliki). Kwa aina ya umbumbumbu walio nao wasanii wetu, si rahisi sana kukwepa maswaibu kama ya dada Saida. Hermy B alisema kwamba, kwa kila kazi inayotoka studio kwake, yeye lazima achukue asilimia fulani (hakuweka wazi ni % ngapi anachukua) kila kazi ya msanii aliyemrekodi inapotumika popote pale, iwe kwenye show, matangazo ya redio, tv ama magazetini. Hapo bado meneja wa msanii nae hajachukua mgao wake. Hii ina maana kwamba, kama msanii ana kipaji na hana pesa za kumrekodi, studio nyingi wako tayari kumrekodia na kumtafutia meneja wa kumsambazia kazi zake, provided atasaini mkataba wa kuachia haki za kazi zake zimilikiwe na hao wanaomtoa, Nadhani hata ugomvi wa Hermy B dhidi ya AY na FA ulitokana na vipengele hivi kandamizi. Huenda hata ile kesi ya Tigo dhidi ya Mwana FA/AY kuna mtu aluchukua mgao wa zile ringtones bila wahusika FA na AY kupewa chochote. Kuna haja kwa washauri wa kisheria kupitia upya mikataba kandamizi ya wasanii wetu ili angalau waishi kutokana na jasho lao, na si jasho lao kufaidisha mameneja wao ama ma-producer wao. Ugomvi wa Muumini Mwinjuma/Ally Choki na African Stars Band una harufu za masuala hayahaya ya hakimiliki. Ally Choki/Muumini anakuwa mwajiriwa wa African Stars Band na kulipwa pesa kulingana na show, ingawa Asha Baraka mmiliki wa bendi hajaimba wala kupiga kinanda. Mwisho wa siku album zinamilikiwa na ASET. Ndicho kilichotokea kwa Marehemu Banza Stone, nae kapitia bendi hii na kuishia TOT, nadhani mpaka kifo kinamkuta alikuwa fukara wa kutosha tu, hata pesa za kununulia dawa mpaka watu wapitishe bakuli. Mauzo ya album za TOT na Twanga Pepeta hayakumsaidia kwa sababu yalichukuliwa na wamiliki, ingawa nyimbo katunga yeye. Kwa maana hii, Choki na wenzie wasipojiongeza basi wataishia kulipwa mishahara huku album walizoimba tangu 2000 zikiwa zinauzwa sokoni na mauzo yanaenda ASET, ihali walioimba wanaishi kuwa maskini.
Nini kifanyike?
Samahani kwa kuandika gazeti refu, ila nimejifunza mengi sana
- Wasanii wana umoja HEWA ambao unawasaidia kwenye kuzikana tu, wajiongeze na kutafuta mwanasheria wa kuwasaidia ku negotiate mikataba yao.
- Wasanii hawapendani kabisa, hata ukisikia nyimbo zao wanatukanana sana. Waamke na kupambana na wanyonyaji wao pale inapobidi, sio lazima wafanikiwe wao, hata watoto wao wanaweza kufaidika huko mbeleni.
Hivi Muta na Ruge ni ndugu? Naomba nifahamishwe mkuuSaida karoli ni dadangu na Muta Mutahba ni kak yangu....hawa ndugu zangu ni wajinga pengine kuliko wajinga wote Tanzanania niliowai kuwashuudia.
Kwani wanaopanda bajaj wakoje?Tumsaidie jamani Saida Si MTU wa kupanda Bajaji kwa kipaji cha sauti yake
Saida shule ndogo ndo tatizo.Ndio maana mnasisitizwa Elimu Elimu Elimu, Mutta aliweza kuutumia ujinga wa Saida kama fursa
Bora ingekuwa hivyo ulivyoandika. Mkataba wa Saida na Mzee Muuta umechukua haki zote za saidaa kwenye zile albam mbili za Chambua Karanga na Mapenzi kizunguzungu. Nyimbo zote kwenye Albam zile siyo za Saida ni za Fm Studiios alipewa hela kidogo akasign mkataba Mbovu.Ukishakuwa chini ya record label hayo ya Saida yanatokea sana! Wewe kama msanii unakuwa huna mchango wowote kwenye utengenezaji kazi zaidi ya talent yako ya uimbaji na labda uandishi na kutengeneza melody! Kinyume chake, unakuta label ndiyo inakugharamia wewe kwa kila kitu... kuanzia na kazi zako hadi maisha yanayoambatana na kazi zako! Unakua "hujui" hata gharama ya kurekodi wimbo wala gharama ya kufanya video! Inakuwa hujui gharama ya mavazi ya kazi wala gharama za hotel unapoenda kufanya show!!!
Kutokana na hilo na ukikosa entertainment lawyer, kuna uwezekano mkubwa sana kazi unazofanya zisiwe mali yako bali zitakuwa copyrighted kwa kampuni uliyopo! Hili likitokea, haki zako zinaweza ku-include % ya mauzo ya album, shows, singles n.k! Hata kama mkataba wenu umeshaisha, utakuwa na haki ya kupata mrabaha/royalty inapotokea matumizi ya nyimbo zako kwa namna moja au nyingine... kwa mfano, kv Diamond ame-sample Salome, yeye kama yeye amemlipa mwenye hati miliki lakini Saida nae anastahili kupata % ya malipo yaliyofanyika! And for what I know, Saida amepata 25% wakati Mzee Mutta kakomba kilichobaki!!!
Anyway, nilichosema sio standard bali hiyo ni moja ya aina za contracts unapokuwa chini ya label!
Ubaya mkubwa zaidi wa mikataba ya aina hii ni pale wakati unaingia msanii unaweza kudhani umelamba dume manake kila utakachotaka, utapewa tu! Utahudumiwa kwa kila kitu huku ukidhani unapewa bure kumbe wenzako wanaweka kumbukumbu kwa kila kitu! Hapa ndipo huwa inaanza migogoro mingi kati ya wasanii na mabosi wao! Siku ya siku album imenunuliwa au umepiga show ya pesa ndefu, unakuta jamaa anakata hadi pesa ulizokuwa unakunywa soda! Mwisho wa siku unakuta unapiga mark time tu cuz' baada ya gharama zote kutolewa, mgao wako unakuta imebaki pesa mboga tu!!!
Upo sawa Hakuna kiasi cha pesa kinachotosha kununua haki bunifu yoyote. Wanaohusika na haya ni Cosota siyo Basata Kama ulivyoandika ingawa mengi uliyosema ni sahihi sana.Kama yale Maneno ni yeye aliandika basi kwa haki miliki za miziki duniani ambazo hata sisi Tanzania chini ya BASATA kama sikosei tumeweka sahihi, Saida karoli anastahili pia kupata pesa yake bila kujali yeye na Muta waliweka sahihi vitu gani.
Wimbo kuna Instruments na Lyrics. Inategemea unachota wapi. Kama Saida aliimba tu na hayo maneno aliandikiwa basi hana haki yoyote katika huo wimbo wa Diamond. Kama Mama ndiye aliandika na anapewa fedha kidogo basi inabidi aende BASATA na bila kujali mikataba ilikuwaje, itabidi haki yake apewe. Haki miliki ziliwekwa ili kulinda Wasanii wasiojua sheria.
Mfano wimbo wa Mbumbe au The Lions Sleeps Tonight, ulitungwa na Solomon Linda wa South Africa. Akaja Mmarekani mmoja na kuununua haki miliki. Baada ya sheria kubadilika ilibidi haki miliki airudishe kwa Binti Mtoto wa Linda na hakurudishiwa fedha yake kwani walimwambia huwezi kununua HAKI MILIKI ya mtu hata utowe fedha gani.
The Lion Sleeps Tonight - Wikipedia, the free encyclopedia
Solomon Linda - Wikipedia, the free encyclopedia
Upo sahihi sana.'Ukipewa Kipaji lakini ukakosa Akili, kitakachotokea ni kutumikishwa tu'
Hicho ndicho kimemkuta Saida Karoli. Hakuna wa kumlaumu, wakujilaumu ni Saida Karoli mwenyewe.
Muta ni mtu mwenye Upeo na Akili, alikuwa anajua anachokifanya wakati ule akitumia muda na rasilimali zake ili kumtoa kimuziki Saida Karoli. Bahati mbaya sana Saida Karoli hakutaka kujua matokea ya Athari za kisheria katika mkataba wake na FM Studio(Muta) wakati ule.
Kilichomkuta Saida Karoli kimewahi kuwakuta pia Nakaaya(katika mkataba na Sonny), The Comedy (Katika mkataba na EATV), Hadija Kopa(Katika mkataba na TOT). Na ndicho hicho hicho huenda kikaja kuwakuta Ya moto Band(Katika mkataba wao na Saidi Fella), Dogo Janja(Na Tip Top Connection), Harmonize, Raymond, nk(Katika mkataba wao na Wasafi Classic..)
Ushauri:
Kwa sasa Saida Karoli akubali tu kuwa alikosea na ujinga wake umemgharimu. Tukio hilo alione kama ni darasa kwake na kwa wasanii wengine katika mambo ya mikataba.
Tumsaidie jamani Saida Si MTU wa kupanda Bajaji kwa kipaji cha sauti yake
Hivi wasanii Fiesta wanalipwa ngapi?. Maana naskia malalamiko tuAkuna cha A-Town wala wapi? Mikataba aiangalii upuuzi wa A-Town wala wapi. Yoyote anapigwa uwe popote mbona kuna wasanii kibao wanapelekwa pelekwa katika matamasha ya Fiesta. Wanapewa mikataba ya kijinga na wanakubali ili mradi wasikose icho kidogo
Mfano mzuri awo Weusi wanapewa pesa ya kawaida na wanaimba katika Fiesta na Niki wa pili ni msomi ulaghai upo kila kona inategemea una njaa ya kiasi gani
Awo Mapacha wenyewe walisanda kwa awo clouds media.
Haya mambo ya mikataba yanategemea yamekukuta na njaa ipi?
FELICIAN MUTA (FM) Alipelekeshana pia na JONGWE (SUGU ),Wanasheria wamsaidie Saida karoli.Wana jamvi naomba tuweke michango yetu hapa..kwayeyote mwenye uelewa kuhusu hili jambo..Kama mambo tunayoyasikia ni ya kweli hivi inawezekanaje mtu unaimba nyimbo halafu unakosa haki ya kuzitumia na wakati sauti ni yako na kila mtu analitambua hilo,mfano nasikia SAIDA KAROLI hawezi kutumia nyimbo zake popote pale kama MZEE MUTA akigoma,hebu nipeni ufafanuzi kidogo hapo maana bado niko 3G kuhusu hilo.
Ndio maana mnasisitizwa Elimu Elimu Elimu, Mutta aliweza kuutumia ujinga wa Saida kama fursa
Ushauri pekee wa kumsaidia Saida Karoli ni huu.
1/Akubali kwanza kuwa alikosea mwenyewe.
2/Aache kulalamika ovyo kwenye mitandao.
3/Aende Kwa Muta na Kumshawishi ule mkataba upitiwe Upya ili uwe na maslahi mapana kwa pande zote(Na kama ikishindikana basi achukue hatua ifuatayo..)
4/Atafute wataalamu wa sheria za mikataba ili afungue shauri kwenye Vyombo husika(kama mahakamani, BASATA, COSOTA, Wizarani nk)
Anzia kusoma mwanzo wa thread, tutakua pamoja tu. UtaelewaWakuu tuelewesheni kilichotokea maana tumevamia tu story katikati
Hivi kumbe kina Rich Mavoko, Raymond na Harmonize wameliwa na WCB! Sijui kama wanalifahamu hili kwa undani kama ulivyoeleza.Ukishakuwa chini ya record label hayo ya Saida yanatokea sana! Wewe kama msanii unakuwa huna mchango wowote kwenye utengenezaji kazi zaidi ya talent yako ya uimbaji na labda uandishi na kutengeneza melody! Kinyume chake, unakuta label ndiyo inakugharamia wewe kwa kila kitu... kuanzia na kazi zako hadi maisha yanayoambatana na kazi zako! Unakua "hujui" hata gharama ya kurekodi wimbo wala gharama ya kufanya video! Inakuwa hujui gharama ya mavazi ya kazi wala gharama za hotel unapoenda kufanya show!!!
Kutokana na hilo na ukikosa entertainment lawyer, kuna uwezekano mkubwa sana kazi unazofanya zisiwe mali yako bali zitakuwa copyrighted kwa kampuni uliyopo! Hili likitokea, haki zako zinaweza ku-include % ya mauzo ya album, shows, singles n.k! Hata kama mkataba wenu umeshaisha, utakuwa na haki ya kupata mrabaha/royalty inapotokea matumizi ya nyimbo zako kwa namna moja au nyingine... kwa mfano, kv Diamond ame-sample Salome, yeye kama yeye amemlipa mwenye hati miliki lakini Saida nae anastahili kupata % ya malipo yaliyofanyika! And for what I know, Saida amepata 25% wakati Mzee Mutta kakomba kilichobaki!!!
Anyway, nilichosema sio standard bali hiyo ni moja ya aina za contracts unapokuwa chini ya label!
Ubaya mkubwa zaidi wa mikataba ya aina hii ni pale wakati unaingia msanii unaweza kudhani umelamba dume manake kila utakachotaka, utapewa tu! Utahudumiwa kwa kila kitu huku ukidhani unapewa bure kumbe wenzako wanaweka kumbukumbu kwa kila kitu! Hapa ndipo huwa inaanza migogoro mingi kati ya wasanii na mabosi wao! Siku ya siku album imenunuliwa au umepiga show ya pesa ndefu, unakuta jamaa anakata hadi pesa ulizokuwa unakunywa soda! Mwisho wa siku unakuta unapiga mark time tu cuz' baada ya gharama zote kutolewa, mgao wako unakuta imebaki pesa mboga tu!!!