Baada ya Mzee Kikwete kuweka sawa mambo na kusema Mzee Mkapa hakupenda sifa pamoja na kufanya mambo mengi ambayo serikali hii bado wana jukumu la kuyakamilisha, mzee Mwinyi aliuchekesha umati wa waombolezaji kwa kuelezea jinsi alivyotoka mbali.
"Katika ujana wangu, nimevaa viatu mara mbili; mara ya kwanza wakati naenda jandoni, na mara ya pili nikiwa na miaka 13 baada ya kufanya kibarua cha kuchuma karafuu na kupata pesa. Ili viatu vyangu visichakae mapema, nilikuwa wakati mwingine navivua na kuvitundika begani huku nikitembea peku". Alisema Mzee Mwinyi.
Umati ulilipuka kwa kicheko na hii iliweka sawa mbavu za watu na kusaidia kuondoa huzuni baada ya zoezi la kumpunzisha Mzee Mkapa. Vijana tusikwame katika hali zetu duni za sasa, haya ni mapito tu na sio mwisho wa maisha yetu.