Mzee Mwinyi: Rais Magufuli aongezewe muda wa miaka 5 zaidi kama shukrani

Mzee Mwinyi: Rais Magufuli aongezewe muda wa miaka 5 zaidi kama shukrani

dosama

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2010
Posts
912
Reaction score
957
"Mimi ni mzee sasa na maneno yangu pengine hudhaniwa ndoto za uzee. Ningetamani mambo mawili, moja la hakika lingine la kufikiriwa. La hakika tuwashawishi watanzania Rais wetu asipate kura ya kumkataa, mwenye kumkataa atupe sababu. La kufikirika ni kwamba nchi yetu inaendeshwa kwa Katiba na lazima tuienzi.

Lakini twaweza kuiahirisha kwa muda ili kumpa Rais Magufuli kipindi kingine kimoja cha asante kisha baadaye tuendelee vilevile, kwa sababu kuna mengi aliyonayo Magufuli akiondoka (baada miaka kumi) nchi itayakosa” Ali Hassan Mwinyi, Rais wa pili wa Tanzania na Rais wa 3 wa Zanzibar.



PIA SOMA
- Hashim Rungwe: Kama tatizo ni muda, Rais Samia aongezewe muda ili tupate Katiba Mpya ndio tufanye Uchaguzi

- Deo Sanga aomba Rais Magufuli aongezewe muda hata asipotaka

- Ally Kessy: Katiba sio msaafu, Rais Magufuli akimaliza muda wake tutatengua Katiba aongezewe muda | Spika Ndugai amuunga mkono

- Zile kelele za Rais Magufuli aongezewe muda mbona hazipingwi kwa Rais Samia?

- Uchaguzi 2020 - Dkt. Magufuli aongezewe muda wa kutawala

- Rais Magufuli akifanya mambo haya, Watanzania watamlilia wenyewe aongezewe muda wa kutawala
 
Asante ya nini mzee wetu wakati ndugu zetu hajawateua kugombea uraisi Zanzibar?. Namishahara yetu kagoma japo kupandisha, kwako wewe uko sahihi kumpa asante maana mpaka vitukuu vyako vitaendelea kuneemeka na mema ya nchi, haliyakuwa sisi walalahoi hatujui hatima yetu ,licha yakuwaza watoto wetu.
 
Hii ikionyesha kua hata ndani ya CCM kwenyewe walobaki wote ni Vichwa maji ,minyooo kichwan kwa sababu hawana kabisaaa mbadala mwenye uwezo wakufanya zaidi ya huyu wanayemuona kafanya ili hali Watanzania wamezidi kua masikini.

Kwamba katika Watanzania zaidi ya milion 60 , hamnaa hamna?

Mwalimu Nyerere alihimiza kuyapima maendeleo kupitia maisha ya watu nasio miundo mbinu .

Kwa ufupi ktk kuyabadili maisha ya watu, JIWE KAFANYA SIFURI .

Kwenye Haki za watu JIWE KAFANYA SIFURI...hii ikimanisha kuendelea kwake kua madarakani, ni kuhalalisha Watu kuendelea kupotea, Kuuawa , Haki za watu kuminywa, Uhuru wa vyombo habari ukizidi kupotea, Uhuru wawatu kukosoa wazi ukizidi kupoteaaa.

Bila kusahau JF itaendelea kupata tabu

CCM nguruwe kweli, ACHENI USENGE ..
 
"Mimi ni mzee sasa na maneno yangu pengine hudhaniwa ndoto za uzee. Ningetamani mambo mawili, moja la hakika lingine la kufikiriwa. La hakika tuwashawishi watanzania Rais wetu asipate kura ya kumkataa, mwenye kumkataa atupe sababu. La kufikirika ni kwamba nchi yetu inaendeshwa kwa Katiba na lazima tuienzi. Lakini twaweza kuiahirisha kwa muda ili kumpa Rais Magufuli kipindi kingine kimoja cha asante kisha baadaye tuendelee vilevile, kwa sababu kuna mengi aliyonayo Magufuli akiondoka (baada miaka kumi) nchi itayakosa” Ali Hassan Mwinyi, Rais wa pili wa Tanzania na Rais wa 3 wa Zanzibar.!

View attachment 1503855
Mwinyi kaanza lini kunywa ugimbi?
 
"Mimi ni mzee sasa na maneno yangu pengine hudhaniwa ndoto za uzee. Ningetamani mambo mawili, moja la hakika lingine la kufikiriwa. La hakika tuwashawishi watanzania Rais wetu asipate kura ya kumkataa, mwenye kumkataa atupe sababu. La kufikirika ni kwamba nchi yetu inaendeshwa kwa Katiba na lazima tuienzi.

Lakini twaweza kuiahirisha kwa muda ili kumpa Rais Magufuli kipindi kingine kimoja cha asante kisha baadaye tuendelee vilevile, kwa sababu kuna mengi aliyonayo Magufuli akiondoka (baada miaka kumi) nchi itayakosa” Ali Hassan Mwinyi, Rais wa pili wa Tanzania na Rais wa 3 wa Zanzibar.


View attachment 1503855
Mzee Mwinyi pamoja na hizo "unthinkable anecdotes" zake, alipaswa kujiongeza na kufikiria nje ya kasha kuwa endapo Mkapa na Jakaya wangeimbiwa sifa hizo, na hata kumshawishiwa na wapambe wao ili nao wapewe kama hiyo asante, sijui hata huyo Magufuli angaliweza kumuona wapi!

Ni lazima muda uliowekwa na masharti ya katiba yetu uzingatiwe. Ni hapo ndipo tutaweza kuwaona "rising stars" wengine na kuyaona madudu ya huyu anayepita, ambaye anaminya uhuru wa kupata habari ili kuficha madhaifu yake.
 
Kile kitabu alichotunga Nyerere alimstahi Mwinyi kwa sababu alikuwa rahisi ila alisema wazi hakuwa chaguo lake lakini angekuwa bado hai hata mtoto wake asingepata uwaziri acha urais wala kina John wasingekuwa marais
 
Mzee kwa sababu kila siku anakula na kushiba, na mwanaye kapewa shavu kwa miaka nenda nasi anaona ana haki kabisa ya kutusemea mamilioni ya Watanzania jambo ambalo kimsingi ni utumbo kusemwa na mtu wa aina yake!

Kuna umuhimu wa kurekebisha vifungu vya Katiba ili Rais aliyemaliza muda wake, asiruhusiwe kujihusisha na mambo ya kisiasa kwa lengo la kulinda heshima yake.
 
Naona mzee Mwinyi ameamua kutoa shukrani zake mapema kweli, kwa zile kura za wajumbe wa bara zilizomuwezesha mwanae kuukwaa Urais wa Znz chini ya mwenyekiti wao.
 
Kuna mtu alisema kule Zanzibar kuwa siyo nchi ya utawala wa kifalme [emoji108]

Kwamba kila mtoto wa ex leader kuwa leader !

Neno!

Sijui alikuwa na maana gani huyu alosema haya!
 
Back
Top Bottom