Mzee Mwinyi [Ruksa] kukutana na wanahabari leo

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
Heshima mbele wanajamvi.

Rais wa awamu ya pili mzee A H Mwinyi maarufu mzee Ruksa atakutana na wanahabari leo nyumbani kwake kuzungumzia maendeleo na majukumu ya kamati iliyoundwa na NEC ya chama cha mapinduzi kufuatilia mienendo ya baadhi ya wabunge wa CCM wanaoishambulia serekali ya chama cha mapinduzi ndani ya bunge na nje ya bunge.

Ikumbukwe katika kikao cha CC na baadae NEC spika wa bunge la JMT mheshimiwa Samwel Sitta alishambuliwa na baadhi ya wajumbe kwa kuongoza vikao vya bunge kuizalilisha serekali ya chama cha mapinduzi.

Source: Jambo Afrika TBC1.
 
hawa nao wanakosa kazi ...hebu nikapate lunch mie
 
Hivi hilo suala mimi nilidhani ni lao wao CCM na kamati zao? Hadidu rejea zilimtaka kutoa taarifa kwa umma?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…