Wakati majuzi Mh. Rais JK akijimung`unya mdomo na kujidai ana kikohozi hadi kunywa maji wakati akijitayarisha kumfuta uwaziri Mh. Prof. Anna Tibaijuka, Rais mwenzie Mzee Julius Nyerere alimfuta kazi mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. Abdulnoor Suleman akiwa na yeye meza kuu.Ilikuwa hivi wakati Nyerere akiwa kwenye ziara mkoani Mwanza wazee walilalamika kwamba mkuu wa mkoa huyo alikuwa anajishugurisha na magendo kwenye inchi jirani kwa kutumia boti zake kwenye ziwa victoiria.
Akifanya majumuisho ya ziara yake Nyerere alitamka kumfukuza kazi mkuu mkoa huo akiwa nae pale meza kuu, hii ilikuwa mwaka 1978.
Eti Kikwete alikuwa anamwonea haya Mh. Tibaijuka kumfuta kazi wakati wala hawakuwa nae meza kuu, je angekuwepo.