Mzee Pathisa Nyathi - Mental Colonisation needs to be cleansed

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
Tatizo la waafrika wanajisikia sifa kuwa walitawaliwa na wageni toka bara ulaya na bara arabu .

Mwaafrika amekuwa roboti na hata ubongo wake unakuwa kama una chipu ya ki eletroniki imepandwa ktk ubongo wake na fikra zake huru kufutwa hivyo kuongozwa (controlled) kwa remote control toka kwa wageni walio mbali kabisa huko ulaya, Marekani, bara arabu, China na Japan.

Pamoja na kupata uhuru, na mkoloni huyo kuondoka au kupinduliwa lakini la kusikitisha ni kuwa bado wapo vichwani kwetu na tunaona fahari kuwa bongo pia Gila zetu zinaongozwa kigeni badala ya kuwa na fikra huru zilizovunja minyororo ya ukoloni, utumwa na imani za kigeni.

Mzalendo mzee Pathisa Nyathi anasema Afrika ilikuwa na wireless kwa karne na miongo elfu nyingi. Wakati watu wa bara lingine wamegundua wireless hivi karibuni. Sayansi ya kiasili ya kiafrika ya kuruka kwa ungo au kumuona mtu ktk bakuli la maji toka masafa marefu lakini tumeshindwa kuendeleza kwa kutekekeza uwezo huo kwa kuamini maneno ya wageni kuwa ni ushirikina.....

Mzee Pathisa Nyathi anashangaa wasomi wa vyuo vikuu vya Afrika wameshindwa kugeuza ungo wa 'kichawi' kuwa kifaa kinachoweza kuruka au kubadili bakuli ya kigae chenye maji kuwa televisheni.

Mzee Pathasi Nyathi anaendelea wazungu walikuwa na stori za kuruka kichawi lakini siyo kwa ungo bali kwa ufagio mkubwa, hata hivyo maono hayo ya kuruka wameyafanyia kazi sasa tunaona vifaa mbalimbali vikiruka angani.

Mzee Pathasi Nyathi anakazia, wenzetu ktk mabara mengine wanaruhusiwa kuota lakini sisi tukiota na kusimulia tunaambiwa ni uchuro au unaandamwa na mizimu unahitaji kugangaliwa.

Lakini Yusufu au Joseph wa kwenye enzi za tamaduni na utawala wa Farao ktk vitabu vya kiimani vya wageni wakiota, ndoto zake zinafanyiwa kazi tangu enzi za Farao hadi sasa iwe Silicon Valley. Sayansi siyo nature anabainisha Mzee Pathasi Nyathi, sayansi ni utamaduni, sayansi ni ndoto iwe ya Joseph wa enzi ya Farao au Albert Einstein wa bara ulaya n.k

Karne kibao zilizopita Tamaduni za Aztec, Maya, Zulu (kiAfrika), Kizungu, KiChina n.k wote walikuwa na ufahamu mmoja, lakini waafrika wakatosa uwezo wao wa kufikiri pale wageni walipokuja kuitawala Afrika kupitia ukoloni, dini za kigeni na utumwa.

Waafrika walikuwa huru hata watoto wa kiafrika kutoka wakiwa wadogo sana walifundishwa kuwa wanajitegemea kwa kufahamu mazingira yao, kuchunga ngombe, kuvua samaki, kulima n.k

Lakini waafrika wakatupa "mikoba ya wahenga'' kuhusu kujitegemea ktk nyanja za kiuchumi, imani zao, mafunzo ya jamii zao kujivunia uhuru ktk nyanja mbalimbali na wakakumbatia kitu kigeni kinachoitwa sheria za kulinda haki za mtoto.

Na sasa mtoto anakatazwa kufahamu ujuzi wa mazingira yake kwa kisingizio cha mtoto hawezi kufundishwa uwindaji, au kushiriki kilimo hivyo mpaka anamaliza chuo au elimu ya sekondari anakuwa tegemezi wa ajira za kupewa kwani anakuwa ni 'mgeni' kijijini kwao kwa maana kijana amekosa ile elimu ya kwao ya kujitegemea iwe kilimo, ufugaji, imani (dini)n.k wote wanataka kuwa wamachinga au kuajiriwa na kukimbilia mijini au kupanda maboti kukimbilia ulaya na bara arabu kutumikishwa.

Kupoteza lugha zetu, utamaduni wetu, ufahari wa kujitegemea tunakuwa roboti lisiloweza kujitegemea kifikra, kujitegemea, kujuamulia mambo yake wenyewe kwani hata tujifunze vipi lugha ya kigeni hatuwezi kuufahamu undani wa tamaduni, ufahari wa kujitegemea kwani siri hizo za wageni wanazilinda kwa wivu mkubwa.

Hivyo ili bara la Afrika liweze kuendelea inabidi ukombozi wa kifikra ipatikane.

Source: Wode Maya

Pathisa Nyathi is a published poet, playwright, historian and biographer. He is a columnist for the Sunday News, Umthunywa, The Sunday Mirror and Sky Host in Zimbabwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…