Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
SAID CHAMWENYEWE KAPEWA MTAA KEKO
Mzee Said Chamwenyewe amepewa mtaa Keko.
Mwanae mmoja bado yupo hai anaitwa Fatima Chamwenyewe.
Haya ni katika mpango wa makazi uliotoa fursa ya kubadili majina ya mitaa na kuweka majina yenye maana na kuhifadhi historia ya wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika.
Lakini Said Chamwenyewe ni nani?
Said Chamwenyewe alikuwa mwanachama wa TAA, TANU na Mjumbe wa Baraza la Wazee wa TANU.
Soma makala hiyo hapo chini kutoka kitabu cha Abdul Sykes (1998) utamfahamu zaidi Said Chamwenyewe:
MWALIMU NYERERE NA CHANGAMOTO ZA KUSAJILI TANU JULAI HADI NOVEMBA 1954
Baada ya kuundwa kwa TANU Nyerere akiwa Rais wake ikaamuliwa kuwa aende kukisajili chama kwa Msajili.
Abdul, Ally Sykes na Nyerere wakakubaliana kuwa Nyerere akishakamilisha usajili wakutane nyumbani kwa Ally Mtaa wa Kipata.
Kisa hiki amenihadithia Bi. Zainab mbele ya mumewe Ally Sykes.
Bi. Zainab anasema Nyerere alipofika Kipata moja kwa moja akajitupa kwenye sofa hoi kachoka taaban.
Jua lilikuwa kali nje.
Uso wa Nyerere ulionesha kuwa mambo hayakwenda vizuri kwa Msajili.
Wote watatu wakawa wametulia wanangoja kumsikiliza Nyerere awake taarifa.
Msajili amekataa kuisajili TANU kwa kuwa Nyerere alikuwa hana rejesta buku la kuonyesha wanachama wa TANU.
Hapo hapo Abdul Sykes akatoa oda akasema niititieni Mzee Said Chamwenyewe.
Mzee Said Chamwenyewe akapewa kadi za TANU na rejesta buku Abdul akamwambia, "Mzee Chamwenyewe nenda Rufiji katuletee wanachama."
Hivi ndivyo ikawa kundi kubwa la wanachama wa mwanzo wa TANU walitoka Rufiji.
Rufiji ilikuwa moja ya himaya za Mufti Sheikh Hassan bin Ameir aliyekuwa pia ni Khalifa wa Quadiriyya.
Hapakuwa na shida ya kuwapata wanachama kwani bila shaka taarifa za TANU kutoka kwa Khalifa zimeshatangulia.
Kadhalika mbele ya Rufiji kuelekea Kilwa Shadhuly chini ya Sheikh Nurdin Hussein ilikuwa na wafuasi wengi na Sheikh Nurdin mwenyewe alikuwa karibu sana na Sheikh Hassan bin Ameir.
Kote huku TANU ilizoa wanachama.
Lakini nguvu hii maadui wa TANU iliwatia hofu wakaanza kueneza propaganda kuwa Waislam wanatayarisha Maji Maji nyingine dhidi ya Waingereza.
Waingereza walimzungusha sana Nyerere katika kutoa tasjila lakini ilipofika tarehe 30 November, 1954 Msajili alimkabidhi Mwalimu tasjila ya TANU.
Ally Sykes akachapisha kadi 1000 za kwanza za TANU kutoka mfukoni kwake kisha akachapisha kadi 2000 kutoka fedha alizokopa Tanganyika African Government Servant Association (TAGSA) yeye akiwa Secretary.
Kadi No. 1 alimwandikia Julius Kambarage Nyerere, TANU Territorial President, kadi no. 2 akajiandikia mwenyewe, kadi no. 3 akamwandikia kaka yake Abdulwahid, kadi no 4 Dossa Aziz, kadi no. 5 Dennis Phombeah kabila Mnyasa kutoka Nyasaland, kadi na 6 Dome Okochi Budohi Mluya kutoka Kenya na kadi no 7 Abbas Sykes.
Wazee wa Kiislam katika harakati kupigania uhuru wa Tanganyika walipokutana na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Agosti 1954. Kushoto waliosimama ni Said Chamwenyewe aliyekuwa msemaji wa wazee wa Dar es Salaam ndani ya Baraza la Wazee wa TANU. Watatu kutoka kushoto mstari wa kati ni Mohamed Jumbe Tambaza na mstari wa mbele wanne ni Sheikh Suleiman Takadir, Mwenyekiti wa Baraza la TANU na mwisho ni Clement Mohamed Mtamila Mwenyekiti wa TANU.